Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara - Fahamu Hili
Friday, September 29Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Majasiri

Inawezekana una wazo zuri sana la biashara na unatamani kulitekeleza haraka kadri iwezekananavyo. Pengine umeajiriwa katika taasisi au ofisi fulani na unashauku kubwa ya kuacha kazi ili uweze kuanzisha kampuni au biashara yako.

Kabla hujafanya maamuzi yoyote ni vyema ukae chini na utafakari mambo kadhaa ambayo yatakuwa na manufaa makubwa kwako.

Katika makala hii nitakueleza mambo 7 muhimu ambayo utahitajika kuyafanya kabla ya kuanza biashara yako.

1. Chagua wazo la biashara vyema

Katika eneo ambalo watu wengi hukosea wakati wanapoanzisha kampuni au biashara ni uchaguzi wa wazo la kibiashara.
Unapochagua wazo baya au usilolimudu, ni wazi kuwa hutoweza kulitekeleza na kupata faida. Hakikisha wazo unalolichagua unalimudu vyema pia linatekelezeka.
Epuka kuchagua wazo pana sana au kuchagua wazo kwa sababu mwingine analifanya. Kwa kuwa wewe unaanza ni vyema ukachagua wazo unalolipenda, kulimudu vyema na linaloweza kukupa faida.
Soma pia: Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara.

2. Fanya utafiti

Kabla ya kuacha kazi yako au kile unachokifanya ili uanzishe kampuni yako, ni vyema ukafanya utafiti wa kina juu ya biashara utakayofanya.

Mambo ya kufanyia utafiti ni:

  • Elewa biashara yako na huduma utakayotoa
  • Fahamu wateja wako
  • Fahamu ushindani
  • Wafahamu watu utakaofanya nao kazi
  • Fahamu njia bora ya mauzo ya bidhaa au huduma yako

3. Andaa mpango wa biashara

Baada ya kufanya utafiti, sasa weka wazo au mpango wako katika karatasi. Mpango huu utakuwezesha kukuongoza katika kufikia malengo yako.

Kimsingi mpango wako wa biashara utajumuisha mambo kama vile:

  • Mwonekano wa jumla wa kampuni
  • Muundo wa utawala
  • Ufafanuzi/Maelezo ya kampuni
  • Malengo, Maono na mikakati
  • Maelezo juu ya soko na tasnia unayoingia kufanya biashara
  • Uendeshaji
  • Mpango wa matumizi ya fedha
  • Pamoja na taarifa nyingine za msingi zinazohusiana

4. Bainisha chanzo cha fedha

Ni lazima kubaini chanzo cha fedha utakazozitumia kuanzisha biashara au kampuni yako. Je fedha hizo zitatokana na mkopo, akiba yako au msaada?

Kumbuka uendeshaji wa kampuni unahitaji fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile matumizi ya ofisi, usafiri, malipo ya huduma, mishahara n.k. Ni vyema kulishughulikia hili mapema ili usije ukakwama katika biashara yako.

5. Bainisha muundo wa kampuni au biashara

Unatakiwa kubainisha muundo wa biashara au kampuni yako kabla hujaianzisha. Je kampuni au biashara yako itakuwa ni ya shirika, ubia au binafsi?

Unapochagua muundo zingatia yafuatayo:

  • Ugumu wa uendeshaji kwa kila mfumo.
  • Gharama za uendeshaji.
  • Kodi.
  • Sheria na vibali.
  • Manufaa ya muundo husika.
  • Mtaji.

Unapozingatia haya hakika utaweza kuchagua muundo wa kampuni au biashara wenye tija zaidi kwako.

6. Tafuta ofisi

Watu wengi wamekuwa wakianzisha kampuni kwa mazoea bila kuzingatia kuwa ofisi ni muhimu kwa biashara au kampuni zao. Tafuta ofisi utakayo mudu gharama zake, pia yenye kukidhi mahitaji ya kampuni au biashara yako.

Kama utaamua kufanyia kazi nyumbani, basi hakikisha unatenganisha mambo binafsi na yale ya ofisini.  Kumbuka kuepuka kuchagua ofisi ya kifahari au ya gharama kubwa bila sababu ya msingi.

7. Bainisha changamoto

Changamoto zipo kila mahali; hivyo yakupasa kuzifikiria kabla ya kuanza kampuni au biashara yako. Kama unajidanganya kuwa utafanya biashara bila kukutana na changamoto yoyote unajidanganya.

Zitambue changamoto mapema ili uweze kuweka mikakati mapema ya namna utakavyo pambana nazo.

Soma pia: Sababu 13 za Kwa Nini Biashara Nyingi Hufa.

Hitimisho:

Naamini makala hii imekupa mwongozo juu ya mambo unayotakiwa kuyafanya kabla ya kuanzisha kampuni au biashara yako. Naamini ukiyafanya haya utaweza kuanzisha kampuni au biashara itakayokuwa na mafanikio makubwa.

Je una maoni au swali lolote? Karibu utuandikie hapo chini; pia usisahau kuwashirikisha wengine makala hii. Karibu pia ufuatilie ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

 

4.1 22 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

21 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Bertha cyprian
Bertha cyprian
4 years ago

Naweza kuwa na kiasi gani cha kianzishia kampuni.?

David joseph
David joseph
Reply to  Kornelio Maanga
4 years ago

Kornel nakupata sana naweza kupata mawasiliano yako nahtaji unishaur Nina idea ya kuanzisha kampuni na ninauhakika nayo lakn nashindwa njia kadhaa ili nifanikishe tafadhali nikipata mawasiliano yako nitafurah sana

John mfoi
John mfoi
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Naenda sanaaaa

khalifa
khalifa
Reply to  Bertha cyprian
1 year ago

kiasi chochote unaweza kuanza nacho kulingana na eneo ulilopo wewe

Dioniz Ruta
Dioniz Ruta
3 years ago

Nahitaji ushauri WaPo kuhusu ujasiliamali

Idan
Idan
3 years ago

hakika kila nikipita katika ukurasa huu huwaa najifunza mengi sana maana nipo kwenye mchakato wakutaka kufungua kampuni

Esther
Esther
3 years ago

Natamani kuanzisha biashara za mikopo ila bado kimtaji siko vizur naweza kuanza na shingapi?

Juma
Juma
3 years ago

Nahitaji kujua jins ya kuanzisha kampuni ya kupamba maharusi

Abdul
Abdul
3 years ago

Upo vizuri

Zulqufly tarky
Zulqufly tarky
2 years ago

Tunawezaje kufanikisha ili?

Antony Elias Ndinga
Antony Elias Ndinga
7 months ago

Je unaweza kuanzisha kampuni ikiwa Elimu yako ni darssa la saba

Hemedyjrjunior
Hemedyjrjunior
7 months ago

Safi sana kwa kazi nzuri

21
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x