Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya - Fahamu Hili
Tuesday, January 21Maarifa Bila Kikomo

Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Nazi

Watafiti wa afya nchini Marekani wamesema matumizi ya mafuta ya nazi si salama kwa afya kama ilivyo kwa nyama ya ng’ombe na siagi.

Shirika la Moyo la Marekani (AHA), limeeleza kuwa mafuta yaliyoko kwenye nazi yanaweza kuongeza lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa AHA, wanadai kuwa kuna mafuta 82% katika nazi. Kuna zaidi ya 63% kwenye siagi, 50% kwenye nyama ya ng’ombe na 39% kwenye nyama ya nguruwe. Wataalamu hao wameongeza kuwa mafuta hayo yanaweza kusababisha lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu.

Baadhi ya watu hudai kuwa ulaji wa mafuta ya nazi una manufaa kwa afya ya mlaji lakini AHA wamesema madai hayo hayajadhibitishwa.

Wamependekeza kuwa, watu wajitahidi kupunguza kiasi cha mafuta yenye lehemu wanayoyatumia kila siku katika maisha yao.

Katika hatua nyingine huko Uingereza mamlaka ya afya ya uma imeshauri wanaume kula gramu 30 za mafuta pekee huku wanawake wakishauriwa kutumia gramu 20 pekee za mafuta yanayochangia lehemu katika mwili.

Habari hii inakuja kwa mshangao baada ya miaka mingi ya kusikika uzuri wa vitu vingi vitokanavyo na nazi kuwa vyenye msaada kiafya. Kwa hakika sasa unaweza kupata mafuta ya nazi katika kila kitu kuanzia dawa za nywele hadi dawa za meno.

Wataalamu wa lishe wanasema kuwa mafuta ya nazi yanaweza kuwa mazuri kutumika juu ya mwili wako tu, na sio ndani ya mwili wako.

Je una maoni gani juu ya utafiti huu? Wakazi wa pwani ambao ni watumiaji wakubwa wa nazi wanakubaliana na utafiti huu? Tafadhali, tupe maoni yako pia washirikishe wengine.

Washirikishe Wengine Makala Hii:

2
Tafadhali tuandikie maoni yako:

avatar
1 Comment threads
1 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
2 Comment authors
Kornel M.EZRONI SAMWEL Recent comment authors
newest oldest most voted
EZRONI SAMWEL
Guest
EZRONI SAMWEL

duh!!!
Baada ya hilo kuthibitishwa jamii ipewe tahadhari maana matumizi ya mafuta ya nazi ni makubwa sana Tanzania haswa kwa wakazi wa pwani na zanzibari.
Mamlaka husika hazina budi kutimiza wajibu wake.

Kornelio Maanga
Admin

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com