Utafiti: Karatasi Zinazobandikwa Ukutani Zinaweza Kusababisha Ugonjwa - Fahamu Hili
Thursday, April 25Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Utafiti: Karatasi Zinazobandikwa Ukutani Zinaweza Kusababisha Ugonjwa

Washirikishe Wengine Makala Hii:

kitchen

Utafiti umebaini kuwa sumu zinazozalishwa na kuvu(fangus) zinazojizalisha kwenye karatasi za ukutani katika nyumba zetu zinaweza kuharibu hewa na kuiingia mwilini kwa urahisi, na kusababisha “maradhi ya jengo;”.

Maradhi ya jengo hutumiwa kuelezea hali ambayo wakazi wa jengo wanajihisi madhara makubwa ya afya ambayo yanaonekana kuwa yanahusishwa moja kwa moja na wakati waliotumia katika jengo fulani.

“Tulionyesha kwamba sumu ya mycotoxins inaweza kuhamishwa kutoka vifaa vya vilivyo ukutani kwa hewa, katika ya hali ambayo inaweza kukutana na binadamu katika majengo,” alisema Jean-Denis Bailly, Profesa katika Shule ya Veterinary School ya Toulouse nchini Ufaransa.

“Kwa hiyo, mycotoxins inaweza kuvutwa na binadamu na inapaswa kuchunguzwa kama vigezo vya kupima ubora wa hewa ya ndani ya nyumba, hasa katika nyumba zilizo na uchafuzi wa vimelea unaoonekana,” alisema Baily.

Chanzo cha utafiti huo ni upungufu wa data juu ya hatari za kiafya kutokana na mycotoxins zinazozalishwa na kuvu zinazojijenga ndani ya nyumba.

Watafiti walijenga dawati la majaribio ambalo linaweza kuiga hewa iliyo juu ya kipande cha karatasi ya ukutani iliyoharibika, kisha kudhibiti kasi hewa. Kisha wao wakapima uchafuzi uliosababishwa na kipande hicho katika hewa.

Watafiti hao walibaini kuwa wingi wa sumu katika hewa hiyo ulitokana na kuvu. Lakini pia walibaini uwepo wa chembechembe ndogo zinazotokana na karatasi zilizoharibika mabazo ni rahisi kuingia mwilini kwa kuvutwa katika hewa.

Watafiti walitumia aina tatu za vimelea katika utafiti wao: Penicillium brevicompactum, Aspergillus versicolor na Stachybotrys chartarum.

Aina hizi, ambazo zimechunguzwa kwa muda mrefu kama vyanzo vya uchafu wa chakula, pia ni “uchafu wa mara kwa mara ndani ya numba,” alisema Bailly.

Bailly aliongeza kuwa ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia vifaa vinavyookoa nishati unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha kuvu wanaotengeneza mycotoxins.

Aliongeza kuwa utumiaji wa vifaa vinavyozalisha maji na mvuke kunaweza kuchangia kuzaliana zaidi kwa kuvu wanaotengeneza sumu hizi.

Bailly alihitimisha kuwa “Kuwapo kwa mycotoxins ndani ya nyumba kunapaswa kuzingatiwa kama kigezo muhimu cha ubora wa hewa,”.

Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la Applied and Environmental Microbiology.

Je una maoni gani kutokana na utafiti huu? Tuandikie maoni yako kisha washirikishe wengine.

1 1 vote
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x