Kwa kawaida kilimo kinahitaji maji, urdhi ya kutosha, jua n.k. Lakini hali ni tofauti kwa kampuni ya AeroFarms ambayo imekuja na mawazo tofauti ya kulima mazao mbalimbali bila kutumia udongo, jua wala maji mengi.
Kilimo chao hufanyika ndani ya nyumba tena kwenye ghala la zamani; hii ina maana kuwa kilimo hiki kinaweza kufanyika popote bila kuathiriwa na hali ya hewa.
Wazo hili lilianzishwa na Ed Harwood, ambaye ni profesa kwenye Chuo cha kilimo cha Cornel aliyetaka kupanda vitu bila kutumia vitu vinavyokuza vitu.
Kilimo bila ardhi au udongo
AeroFarms wametengeneza vitu kama rafu au shelfu ambavo zina vitambaa maalumu ambavyo mbegu husiwia juu yake badala ya udongo. Mizizi ya mmea husika hujishikiza katika kitambaa hicho kuelekea chini kujipatia virutubisho na maji.
Rafu/Mashelfu ya aeroponic
Kilimo bila maji mengi
AeroFarms hawatumii maji mengi kama ilivyo kwa kilimo cha kawaida ambacho hutumia zaidi asilimia 70 ya maji; kwani wao hutumia ukungu wenye virutubisho vinavyohitajika na mmea. Teknolojia hii inajulikana kama kupanda mimea bila udongo wala maji mengi “aeroponics”; hii ina maana kuwa mimea hii hutumia maji kidogo kuliko ile ya kilimo cha kawaida.
Mchoro wa teknolojia ya aeroponic.
Kilimo bila jua
Katika kilimo hiki AeroFarms hawatumii jua kukuza mimea yao bali hutumia taa maalumu za LED ambazo pia zinaokoa nishati. Kwa njia hii wanaweza kutawala kiasi cha mwanga, rangi ya mazao, virutubisho, na hata ladha na ubora wake.
Je kilimo hiki kina tija?
Kwa mujibu wa AeroFarms wanadai kuwa mavuo katika kilimo hiki ni mara 130 zaidi kwa mita za mraba ukilinganisha na shamba la kawaida. Pia wanadai hutumia asilimia 95 pungufu ya maji na asilimia 40 pungufu ya madawa ukilinganisha na kilimo cha kawaida. Taarifa zinaonesha kuwa AeroFarms wameshapata faida zaidi ya dola milioni 100 hadi sasa.
Bidhaa zilizokamilika
Je una maoni gani kuhusu kilimo hiki? Je kinafaa kwa mazingira yetu ili tutunze mazingira? Tuuandikie maoni yako kisha washirikishe wengine.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Nnimefurahishwa sana na kilimo hiki je! nawezaje kupata maelekezo zaidi? nitashukuru endapo nitapata mwongozo juu ya kilimo hiki. asante
Tunashukuru kwa maoni yako mazuri; tutafanyia kazi suala lako na kutoa maelezo na ufafanuzi zaidi wa kilimo hiki. Asante.