
Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka
Kuanza biashara kutoka kiwango cha sifuri siyo kazi rahisi. Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua. Unapokuwa kwenye biashara ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako; ili ujitahidi kuyaepuka ama kuyapunguza kadri iwezekanavyo. Ni dhahiri kuwa wajasiriamali wengi wamekwama kutokana na kupuuzia au kutofahamu makosa haya 15 ambayo hata wewe unatakiwa kuyafahamu na kuyaepuka.
1.Kujifanya unafahamu kila kitu
Usijifanye unajua kila kitu, hasa kama ndiyo umeingia kwenye ulimwengu wa kibiashara. Kwanini? Kwa sababu kuendesha biashara ni kujifunza na kupata uzoefu. Jitahidi ku...