Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua - Fahamu Hili
Thursday, March 28Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Intaneti

Hivi leo kuna mambo mengi kuhusu intaneti, lakini hapa nitakuonyesha baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuvutia na kukushangaza. Historia ya intaneti inaanzia miaka ya 1950 ikienda sambamba na maendeleo ya kompyuta.

Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners-Lee. Kuundwa kwa intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kulibadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi.

Tunapotazama intaneti leo, ni wazi kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo. Karibu ufuatilie makala hii ili ufahamu mambo 18 ya kushangaza kuhusu intaneti usiyoyajua.

1. Tovuti ya kwanza bado ipo

Tovuti ya kwanza kutengenezwa bado ipo na inafanya kazi hadi leo. Jambo pekee ni kuwa tovuti hiyo inaonekana vile vile kama ilivyokuwa zamani. Unaweza kutembelea hapa ili kuiona.Tovuti ya kwanza

2. Takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kwa siku

Kampuni ya Radicati inakadiria kuwa takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kila siku. Inaelezwa kuwa asilimia 90 ya barua pepe hizo ni barua pepe hatarishi (SPAM) na Virusi, hivyo kuwa makini na barua pepe unazofungua.Barua pepe

3. Tweet ya kwanza ilichapishwa Machi 21, 2006 na Jack Dorsey

Nani alifahamu kuwa Twitter ingekuwa maarufu duniani kama ilivyo leo? Mnamo Machi 21, 2006 Jack Dorsey aliandika tweet ya kwanza iliyokuwa inasema, “Just setting up my twttr.” lakini hivi leo Twitter imeshakuwa na mamilioni ya watumiaji ulimwenguni kote.Twitter

4. Video iliyotazamwa kuliko zote kwenye mtandao ni Despacito

Wimbo wa Despacito ulioimbwa na Luis Fonsi na Daddy Yankee ni wimbo unaoongoza kwa kutazamwa na watu wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Wimbo huu umeshatazamwa mara bilioni 3.55 hadi sasa.

5. Mgunduzi wa intaneti Tim Berners-Lee alipewa cheo cha Knight na malikia Elizabeth

Kutokana na ugunduzi mkubwa alioufanya Tim Berners-Lee, malikia Elizabeth wa Uingereza alimpa cheo cha Knight kwenye serikali yake mwaka 2003.Mwanzilishi wa Intaneti

6. Saa 300 za video hupakiwa kila dakika kwenye YouTube

YouTube ni mtandao maarufu ambao wengi wanaufahamu kama mtandao wa kusambaza na kutazama video kwenye mtandao. Lakini je unajua kuwa kwa muda wa dakika moja video zenye jumla ya urefu wa saa 300 hupakiwa katika mtandao huu? Tovuti hii hupokea video kutoka kwa watumiaji mbalimbali duniani kote.YouTube

7. Neno kuperuzi mtandao (Surfing the internet) liliundwa mwaka 1992

Kabla ya mwaka 1992 neno (surfing the internet) halikuwa linafahamika hadi pale Jean Polly alipoandika makala iliyosomwa sana na kupakuliwa na watu wengi na kusababisha kusambaa kwa neno hili.

8. Mitandao ya kutafuta wapenzi inazalisha takriban dola bilioni 2.2 kila mwaka

Teknolojia imebadili mfumo wa maisha. Watu hutafuta wapenzi au wenzi wa maisha kwenye mtandao. Hili limepelekea tovuti za kutafuta wapenzi kuzalisha zaidi ya bilioni 2.2 kwa mwaka 2014 pekee.

9. Asilimia 10 ya wahalifu wa kijinsia wanatumia mitandao ya kutafuta wapenzi

Kutokana na umbali au kutokufahamiana vyema, wahalifu wengi wa kijinsia hutumia mitandao ya kutafuta wapenzi kufanya uhalifu wao.

10. Takriban Watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kupitia Match.com

Mtandao wa match.com unadai kuwa takriban watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kwenye tovuti hiyo ya kutafuta wapenzi.Mtoto

11. China ina kambi za kutibu waathirika wa kutawaliwa na mtandao (internet addict)

Wakati china ikiwa na watumiaji wa intaneti wapatao zaidi ya milioni 721, inaaminika kati yao milioni 23 ni waathirika wa kutawaliwa na mtandao. Hivyo wameanzisha kambi mbalimbali za kuwasaidia watu hawa.

12. Watumiaji wengi wa intaneti ni roboti na programu haribifu (malware)

Wakati mwingine unaweza kufikiri watumiaji wa mtandao ni watu pekee. Lakini asilimia kubwa ni roboti na programu haribifu zilizobuniwa na watu mbalimbali ili kutimiza shughuli fulani.Roboti

13. Tweets milioni 500 zinatumwa kila siku

Kutokana na Twitter kuwa na watumiaji milioni kadhaa, inaaminika kuwa zaidi ya tweets milioni 500 hutumwa kila siku.

14. Huwa unatumia kisehemu kidogo tu cha mtandao

Ni wazi kuwa sehemu unayoitumia kwenye intaneti ni sehemu ndogo sana ambayo inaonekana kwenye injili pekuzi (search engines). Ipo sehemu nyingine ambayo imefichwa kwenye injini pekuzi (dark web); sehemu hii inajumuisha taarifa binafsi za watu, taasisi na makampuni mbalimbali. Unaweza kuperuzi sehemu iliyofichwa ya intaneti kwa kutumia kivinjari (browser) ya Tor.

Soma pia: Sehemu ya Mtandao wa Intaneti Iliyofichwa (Deep web na Dark web).

15. Tovuti 30,000 zinadukuliwa kila siku

Kutokana na kuongezeka kwa uhalifu wa kwenye mtandao, inakadiriwa kuwa zaidi ya tovuti 30,000 hudukuliwa na wadukuzi kila siku.

Soma pia: Usalama wa Msingi wa Kompyuta: Jinsi ya Kujilinda na Virusi, Wadukuzi na Wezi.

16. IMDb ilikuwepo tangu miaka ya 1990

Tovuti maarufu ya kutafuta video, filamu, vipindi vya televisheni pamoja na michezo ya video ilianzishwa mnamo Oktoba 21, 1990, na Col Needham. Baada ya miaka minne ilipata jina lake la IMDb ambalo imedumu nalo hadi leo.

17. Tovuti milioni 7 zilifungwa mwaka 2009

Huduma ya GeoCities ya Yahoo iliyokuwa inawaruhusu watu kutengeneza tovuti zao binafsi ilifungwa mwaka 2009 na kupelekea kufutwa kwa zaidi ya tovuti milioni 7. Tovuti hizi zilifutwa kutokana na kuwepo kwa tovuti nyingi zilizokuwa na ubora duni.

18. Watu takriban asilimia 100 wa Iceland  wanatumia intaneti

Nchi nzima ipo kwenye mtandao? Ndiyo, nchi ya Iceland ina wakazi wapatao 331,778 ambao takriban wote wanatumia mtandao wa intaneti. Je nchi yako ni ya ngapi? Unaweza kutazama hapa.Iceland

Hitimisho

Naamini umejifunza mambo kadhaa mapya kuhusu mtandao wa intaneti. Ni wazi kuwa safari ya maendeleo yaliyofanyika kwenye mtandao wa intaneti ni ndefu na ina mabo mengi sana ya kusisimua.

Je una maoni, maswali, au mapendekezo? Tafadhali tuandikie hapo chini; pia usisahau kuwashirikisha wengine makala hii. Unaweza pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

2 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Max Ernest
Max Ernest
4 years ago

Ahsante kwa Makala nzuri, nitazifuatilia na kushare kuanzia now, ufike mbali

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x