
Tovuti 20 Ambazo Ungetamani Kuzijua Mapema
Unaweza ukawa unajiuliza tovuti hizo ni zipi? Intaneti imejaa tovuti nyingi sana, za maana na zisizo za maana. Hata hivyo bado tovuti za maana na zenye manufaa zimeweza kujibainisha wazi kati ya zile zisizofaa. Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe tovuti 20 ambazo kwa namna moja au nyingine zitakufaa katika maisha yako ya kila siku.
1. Have I Been Pwned?
Tovuti: https://haveibeenpwned.com/ Hii ni tovuti nzuri sana kwa ajili ya kukagua kama barua pepe yako imeshavuja kwenye taarifa za siri zilizoibiwa. Hivi leo kuna makampuni na tovuti nyingi zinazodukuliwa na kuibiwa taarifa za watumiaji wake. Hivyo unaweza kuwa ni moja kati ya watu ambao barua pepe zao ziliibiwa. Ikiwa utaambiwa kua barua pepe yako imeonekana kwenye taarifa zilizodukuliwa basi badili neno la siri hara...