Kompyuta Archives - Fahamu Hili
Thursday, April 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tag: Kompyuta

Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua

Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua

Maarifa, Teknolojia
Hivi leo kuna mambo mengi kuhusu intaneti, lakini hapa nitakuonyesha baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuvutia na kukushangaza. Historia ya intaneti inaanzia miaka ya 1950 ikienda sambamba na maendeleo ya kompyuta. Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners-Lee. Kuundwa kwa intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kulibadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi. Tunapotazama intaneti leo, ni wazi kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo. Karibu ufuatilie makala hii ili ufahamu mambo 18 ya kushangaza kuhusu intaneti usiyoyajua. 1. Tovuti ya kwanza bado ipo Tovuti ya kwanza kutengenezwa bado ipo na inafanya kazi hadi leo. Jambo pekee ni ku...
Njia 4 za Kujilinda Unapofanya Miamala au Manunuzi Kwenye Mtandao

Njia 4 za Kujilinda Unapofanya Miamala au Manunuzi Kwenye Mtandao

Teknolojia
Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari mawasiliano (TEHAMA), mfumo wa biashara pia umebadilika. Hivi leo ni rahisi kutuma na kupokea pesa, kuuza au hata kununua bidhaa kwa njia ya mtandao. Watu wengi hupenda kufanya manunuzi na mauzo ya bidhaa kwenye mtandao kutokana na urahisi wa upatikanaji wa bidhaa na huduma kupitia mtandao. Pamoja na nafasi hii kubwa ya mtandao katika maswala yanayohusu fedha, zipo changamoto mbalimbali zinazoandamana na miamala na manunuzi ya kwenye mtandao. Fahamu jinsi unavyoweza kujilinda unapofanya miamala au manunuzi mbalimbali kupitia mtandao. 1. Tumia kinga-virusi (antivirus) bora Mtandao wa intanet ni chanzo kikubwa cha virusi na wadukuzi. Hivyo ni vyema ukatumia programu madhubuti kwa ajili ya kukukinga na virusi na wadukuzi mara unapofanya manu...
Njia 8 za Kutambua Bidhaa Feki au Bandia

Njia 8 za Kutambua Bidhaa Feki au Bandia

Tija
Mara nyingi tunanunua vitu na bidhaa mbalimbali bila kuzifahamu au kuzichunguza vyema. Hili limepelekea watu wengi kununua bidhaa zisizofaa kwao au zenye madhara kwenye afya zao. Kutokana na ukosefu wa elimu pamoja na kuishi kwa mazoea, watu wengi hawajui wala hawachunguzi vyema bidhaa wanazozinunua ili kuhakikisha ubora wake. Madhara ya kutumia bidhaa feki au bandia: Matatizo ya kiafya kama vile saratani na ulemavu. Upotevu wa fedha. Ajali (Milipuko, shoti ya umeme, n.k). Huathiri uchumi. Ni wazi kuwa yapo madhara mengi yatokanayo na matumizi ya bidhaa feki. Hivyo ni vyema ukafahamu njia za kubaini bidhaa hizi. 1. Ofa na matangazo yasiyo ya kawaida Wahenga walisema “Chema chajiuza kibaya chajitembeza”; ni vyema ukawa makini na bidhaa zenye punguzo kubwa la bei ku...
Programu 6  za Kuondoa Makosa Katika Uandishi wa Kiingereza

Programu 6 za Kuondoa Makosa Katika Uandishi wa Kiingereza

Tija
Kama wewe ni mwandishi wa machapisho au wa blogu, unafahamu jinsi ilivyo muhimu kuandika makala zenye ubora. Wengi wetu hutumia muda mwingi kuandika, kubuni na hata kupangilia makala au machapisho yetu kuliko muda tunaotumia kuhariri. Kuhariri ni sehemu muhimu katika uandishi wowote ili kukuwezesha kuandika makala yenye ubora. Kwa kutambua umuhimu huu nimekuandalia orodha ya programu 6 za kompyuta zitakazokuwezesha kupunguza kama siyo kuondoa kabisa makosa katika uandishi wa Kiingereza Soma pia: Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora. 1. Grammarly Hii ni programu maarufu sana yenye uwezo wa kubaini makosa mengi ambayo usingeweza kuyabaini kwa njia ya kawaida. Kiunganishi: Grammarly 2. Polishmywriting Hii ni programu nzuri ya kuhariri inayoonyesha makosa kwa rangi tatu. Nyekundu ni mako...
Mambo 8 ya Kufanya ili Kuwa na Nywila (password) Imara na Salama

Mambo 8 ya Kufanya ili Kuwa na Nywila (password) Imara na Salama

Teknolojia
Katika ulimwengu wa leo nywila au password si jambo geni. Mara kadhaa umeona au kutumia password katika vitu na maendeo kadhaa kama vile benki, simu, kompyuta n.k. Jambo la kushangaza ni jinsi watu wanavyotumia nywila bila kujali umuhimu wake katika eneo husika. Mtazamo wa ujumla juu ya nywila (password) Nywila ni ufunguo wa kufungua na kufunga sehemu husika; hivyo aliye nao ndiye atakayeweza kufungua na kufunga. Nywila ngumu = usalama zaidi; nywila rahisi = uslama kidogo. Mhalifu anaweza kutumia nywila kufanya uhalifu. Hivyo basi ni muhimu kufahamu namna ya kutengeneza nywila imara na salama kwa ajili ya kifaa au akaunti yako. Fuatilia makala hii ili uweze kujifunza mambo kadhaa ya kufanya ili kutengeneza nywila imara. 1. Epuka namba na maneno rahisi Wengi wetu hatu...
Njia 3 za Kutengeneza Pesa kwa Kutumia YouTube bila Adsense

Njia 3 za Kutengeneza Pesa kwa Kutumia YouTube bila Adsense

Kipato, Tovuti na Blogu
Watengenezaji wengi wa video wanajua jisi ilivyo vigumu kutengeneza pato la uhakika kupitia Youtube kwa kutumia Adsense pekee. Watengenezaji wengi wa video wamekuwa wakifikiri kuwa kupakia video zenye ubora sana kwenye mtandao wa YouTube kutawafanya kupata fedha lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo. Ni vigumu kujua ni kiasi gani unaweza kupata kutokana na Adsense kwenye YouTube, lakini unaweza kukadiria kwa video kutazamwa mara elfu moja utapata takribani dola moja. Kiasi hiki ni kidogo ukilinganisha na kazi utakayokuwa umeifanya ili kukipata. Tazama njia tatu nitakazokueleza zitakazokuwezesha kupata fedha kwenye mtandao wa YouTube bila kutumia Adsense. 1. Mshirika au Wakala Unaweza kupata fedha kwenye YouTube kwa njia ya kuwa mshirika au wakala wa makapuni mbalimbali yanayozalis...
Usalama wa Msingi wa Kompyuta: Jinsi ya Kujilinda na Virusi, Wadukuzi na Wezi

Usalama wa Msingi wa Kompyuta: Jinsi ya Kujilinda na Virusi, Wadukuzi na Wezi

Teknolojia
Watu wengi hufikiri kuwa usalama wa kompyuta ni swala gumu lenye changamoto kubwa. Inaweza kuwa hivyo kama hukuchukua hatua sahihi mapema. Katika makala hii utafahamu hatua tano muhimu ambazo zitakuwezesha kujilinda na virusi, wadukuzi na wezi katika kifaa chako cha kielektroniki. 1. Wezesha automatiki sasishi (automatic updates) Programu mbalimbali za kompyuta hutoa masasisho (updates) mara kwa mara ili kuziba mianya mbalimbali hasa ya kiusalama iliyobainika katika matoleo ya awali. Program kama Microsoft Window, Mozilla na Chrome ni baadhi ya programu muhimu zinazohitajika kusasishwa kwa wakati. Hivi leo programu mbalimbali huja na usasishaji wa automatiki lakini watu wengi hupenda kuuzima usasishaji huu bila kuzingatia umuhimu wake wa kiusalama. Hivyo basi, ili kuwa salama zing...