Kama wewe ni mwandishi wa machapisho au wa blogu, unafahamu jinsi ilivyo muhimu kuandika makala zenye ubora. Wengi wetu hutumia muda mwingi kuandika, kubuni na hata kupangilia makala au machapisho yetu kuliko muda tunaotumia kuhariri. Kuhariri ni sehemu muhimu katika uandishi wowote ili kukuwezesha kuandika makala yenye ubora. Kwa kutambua umuhimu huu nimekuandalia orodha ya programu 6 za kompyuta zitakazokuwezesha kupunguza kama siyo kuondoa kabisa makosa katika uandishi wa Kiingereza
Soma pia: Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora.
1. Grammarly
Hii ni programu maarufu sana yenye uwezo wa kubaini makosa mengi ambayo usingeweza kuyabaini kwa njia ya kawaida.
Kiunganishi: Grammarly
2. Polishmywriting
Hii ni programu nzuri ya kuhariri inayoonyesha makosa kwa rangi tatu. Nyekundu ni makosa ya tahajia(spelling), Bluu makosa ya kimuundo, na kijani ni makosa ya kisarufi.
Kiunganishi: Polishmywriting
3. Ginger
Ginger ni programu inayokaribiana na Polishmywriting lakini ina uwezo mkubwa zaidi. Hii kukuwezesha kubaini makosa ya matumizi ya for, a, an, the, have, has, n.k kwa urahisi zaidi.
Kiunganishi: Ginger
4. Slick Write
Programu hii haibainishi tu makosa bali hukuonyesha uchambuzi wa kina wa ubora wa makala yako. Pia hurekodi taarifa kadri unavyozidi kuboresha uwezo wa uandishi.
Kiunganishi: Slick Write
5. PaperRater
Hii ni programu ambayo ina uwezo wa kuchunguza makosa mbalimbali pamoja na maswala mengine yahusianayo na uandishi bora.
Kiunganishi: Paperrater
6. 1checker
1checker ni programu nzuri na ya bure yenye uwezo wa kubaini makosa na kuchunguza vipengele mbalimbali vya kiuandishi katika andiko lako. Programu hii hukuwezesha pia kuboresha na kutumia misamiati bora.
Kiunganishi: 1checker
Ni aibu kuandika andiko/matini ya Kiingereza iliyojaa makosa. Ikumbukwe kuwa hariri na usomaji prufu hufanywa na wataalamu kwa gharama kubwa; lakini unaweza kupunguza au kuondoa makosa ya kiuandishi katika maandiko ya kiingereza kwa kutumia programu hizi.
Pamoja na hayo kumbuka kuwa akili ya binadamu haiwezi kubadiliwa na akili bandia (artificial intelligence), hivyo ni vyema pia kumtumia mmahiri wa lugha kukusaidia kuhariri kama unaweza kumpata.
Je una swali au maoni yoyote kuhusiana na makala hii? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Hizi program za kusaidia katika uandishi zinaweza kutumika katika uhariri wa vitabu vya kiswahili?
Hapana; hizi ni kwa ajili ya uandishi wa Kiingereza pekee, lakini tutaandaa makala kwa ajili ya uandishi wa Kiswahili.