Njia 5 za Kuongeza Kasi na Usahihi wa Kuandika (Typing) kwa Kutumia Kompyuta - Fahamu Hili
Thursday, February 22Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Njia 5 za Kuongeza Kasi na Usahihi wa Kuandika (Typing) kwa Kutumia Kompyuta

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Kuandika kwa kompyuta

Kuandika kwa kasi na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta kuna manufaa mengi kama vile kuweza kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi, kuweza kuandika mambo mbalimbali kwa kutumia kompyuta na hata sifa ya kukuwezesha kupata kazi mbalimbali.

Hivyo, najua unatamani kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta; lakini tatizo bado hujaweza kuacha kasi ya kudonoa na kuweza kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi.

Karibu ufahamu njia 5 ambazo unaweza kuzitumia ili kuboresha uwezo wako wa kuandika kwa kutumia kompyuta.

1. Elewa na tumia baobonye (keyboard) vyema

Ili uweze kuongeza kasi yako ya kuandika pamoja na usahihi ni lazima uelewe baobonye vyema na kuitumia vyema. Zingatia haya yafuatayo:

  • Elewa mpangilio wa vitufe kwenye baobonye.
  • Panga vidole kulingana na vitufe stahiki. Katika utumizi sahihi wa baobonye vidole vinatakiwa vipangwe kwa kuzingatia vitufe ya herufi au alama. Hivyo kuna herufi za kidole fulani hadi kingine. Hakikisha kidole kinabonyeza herufi au vitufe vyake tu.Mpangilio wa vidole

Ukizingatia hili utaweza kukamilisha hatua moja muhimu ya kuelewa baobonye pamoja na upangaji wa vidole kama picha hapo juu inavyoonyesha.

2. Tazama kioo cha kompyuta

Ili uweze kuwa na kasi na usahihi unatakiwa kupanga vidole vyako vyema kwenye baobonye kiasi cha kuto kuhitaji kutafuta herufi wakati wa kuandika.

Hakikisha unajitahidi kutazama kiioo pamoja na au pale unaposoma wakati wa kuandika ili kuongeza kasi yako; kwani unapotazama baobonye pamoja na kioo kwa wakati mmoja unapoteza kasi.

3. Tumia mazingira na vifaa sahihi

Hakikisha unatumia vifaa sahihi ambavyo uko huru kuvitumia. Ikiwa utatumia vifaa vibaya au mazingira duni utashindwa kuandika kwa kasi na kwa usahihi. Unaweza kuzingatia haya yafuatayo:

  • Chagua baobonye nzuri ambayo unaweza kuitumia kwa uhuru.
  • Kaa vizuri; hakikisha mgongo wako umenyooka na umeegemea kiti; pia hakikisha mikono yako haijaegemea mahali.

    Kukaa
    Chanzo cha picha ni ToThePC

4. Fanya mazoezi mengi

Hakuna umahiri na ufanisi katika jambo lolote bila kukifanya kitu kwa kiasi kikubwa. Hivyo hakikisha unafanya mazoezi ya kuandika mara nyingi kadri uwezavyo.

Ikiwa huna kazi ya kuandika unaweza kuchukua gazeti na ukaanza kuandika habari fulani zilizoko; unaweza pia kuandika maandishi yanayopatikana kwenye vyanzo na programu mbalimbali za kujifunza kuandika kwa kompyuta.

5. Tumia programu na vyanzo vya kwenye mtandao

Intaneti ni rafiki mkubwa katika kujifunza mambo mbalimbali. Unaweza kutumia tovuti na programu mbalimbali kufanya mazoezi au kujifunza kuandika kwa kompyuta.

Vipo vyanzo mbalimbali vya kwenye mtandao unavyoweza kuvitumia kama vile: http://www.typingtest.com/, http://www.typingweb.com/tutor/, pamoja na http://www.typing.com. Kwa kutumia vyanzo hivi unaweza kujifunza vyema na kwa urahisi zaidi.

Neno la mwisho

Kumbuka kuwa uzoefu katika suala la kuandika kwa kompyuta (typing) linaletwa na mazoezi stahiki na ya kutosha.

Hakikisha unazingatia njia tajwa hapo juu kwa usahihi nawe kwa hakika utaona matokeo. Je kasi na usahihi wako ukoje kwenye kuandika?

Soma pia: Mambo 10 Usiyojua Kama Unaweza Kuyafanya kwa Kutumia Google.

Tafadhali tuandikie maoni au maswali yako hapo chini. Usisahau pia kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x