Mambo 8 ya Kufanya ili Kuwa na Nywila (password) Imara na Salama - Fahamu Hili
Friday, March 29Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 8 ya Kufanya ili Kuwa na Nywila (password) Imara na Salama

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Nywila au password

Katika ulimwengu wa leo nywila au password si jambo geni. Mara kadhaa umeona au kutumia password katika vitu na maendeo kadhaa kama vile benki, simu, kompyuta n.k. Jambo la kushangaza ni jinsi watu wanavyotumia nywila bila kujali umuhimu wake katika eneo husika.

Mtazamo wa ujumla juu ya nywila (password)

  • Nywila ni ufunguo wa kufungua na kufunga sehemu husika; hivyo aliye nao ndiye atakayeweza kufungua na kufunga.
  • Nywila ngumu = usalama zaidi; nywila rahisi = uslama kidogo.
  • Mhalifu anaweza kutumia nywila kufanya uhalifu.

Hivyo basi ni muhimu kufahamu namna ya kutengeneza nywila imara na salama kwa ajili ya kifaa au akaunti yako. Fuatilia makala hii ili uweze kujifunza mambo kadhaa ya kufanya ili kutengeneza nywila imara.

1. Epuka namba na maneno rahisi

Wengi wetu hatupendi kuumiza vichwa ili kupa maneno au tarakimu ngumu zitakazotumika kwenye nywila. Hili ni kutokana na watu kupenda nywila ambazo ni rahisi kukumbukwa. Kwa mfano watu hutumia nywila kama vile: mzee, mama, diamond, pesa, siri; au namba kama vile 1234, 1122, 7777 n.k. Namba au maneno kama haya ni rahisi kubuniwa na wezi au mtu mwenye nia mbaya.

2. Usitumie Miaka

Ukifanikiwa kuona nywila 5, basi 2 hadi 3 zitakuna na miaka. Watu wengi hupenda kutumia miaka kadha wa kadha katika nywila zao ili kurahisisha uwezo wa kuzikumbuka. Mara nyingi watu wanatumia nywila zenye mwaka wa kuzaliwa, harusi, kupata mtoto nk. Kwa mfano 1990, rose1990, king2001, love1980, n.k. Hii ni mafano tu ya kuepukwa kwani nywila kama hizi ni rahisi kubuniwa na mtu mwovu au hata programu za kidukuzi za kompyuta.

3. Usitumie majina ya utani au ndugu

Matumizi ya majina ya utani au ndugu katika nywila imekuwa ni sababu kubwa ya watu wengi kudukuliwa na wahalifu mbalimbali. Watu hutumia majina yao ya utani au ya watu wao wa karibu kama vile mume, mke, baba, mama mtoto nk. Mifano dhahiri ni: kide, mjeda, jembe, mkaliwao, mzee, Injinia, Joni, Rozi, Pita, cheupe, n.k.

4. Usitumie programu maalumu za kutengeneza nywila

Kuna programu zijulikanazo kwa lugha ya kiingereza kama (Password Generators) ambazo hutumika kutengeneza nywila imara. Hivi karibuni utafiti umebaini kuwa baadhi ya wadukuzi wamegundua alogaridhimi inayotumiwa na programu hizi; hivyo ni rahisi kwao kugundua nywila iliyotengenezwa kwa progamu hizi.

5. Usiandike nywila mahali

Unaweza kufikiri njia rahisi ya kuikumbuka nywila ni kwa kuiandika; lakini je ulishawahi kufikiri ikiwa mtu mbaya ataona ulipoandika nywila yako? Jibu ni kuwa ataipata nywila yako na kuitumia kihalifu; hivyo basi jitahidi kuikumbuka kichwani mwako na si kuiandika mahali.

6. Usitumie nywila moja kila mahali

Zipo sehemu na vitu mbalaimbali vinyohitaji nywila; hivyo ni rahisi kurahisisha kwa kutumia nywila moja kila mahali. Tatizo hapa linatokea pale ambapo mdukuzi au mwizi atapa nywila hiyo; kwani atakuwa amepata ruhusa ya kuingia kila mahali nywila hiyo inapotumika. Hivyo basi jitahidi kutotumia nywila moja katika sehemu zaidi ya moja.

7. Usimpe mtu nywila yako

Mara nyingine watu huwa na mazoea ya kuaminia kupita kiasi hata kufikia hatua ya kushirikishana nywila. Swala hili si jema kwani huwezi kujua mtu unayempa nywila ataitumiaje au naye atampa nani. Ili kuhakikisha usalama wa nywila yako ni vyema ukaepuka kumpa mtu mwingine yeyote nywila yako.

8. Badili nywila yako kila baada ya muda

Je umetumia nywila yako zaidi ya mwaka? Ni wakati wa kuibadili sasa. Hakikisha unabadili nywila yako mara kwa mara ili kuongeza kiwango cha ugumu wa kuzoeleka kwake na mtu yeyote anayeidadisi. Hakikisha unabadili nywila yako katika vipindi tofauti tofauti ili kuepuka mtu yeyote yule kuibaini.

Hitimisho

Swala la usalama wa kifaa au akaunti yako ni muhimu sana. Hivyo jitahidi kutunza nywila yako mahali salama. Epuka mambo tajwa hapo juu ambayo yanaweza kupunguza usalama wa nywila yako.

Je una swali au maoni yoyote kuhusiana na makala hii? Tafadhali tuandikie maoni yako kisha washirikishe wengine.

5 1 vote
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x