
Njia 4 za Kujilinda Unapofanya Miamala au Manunuzi Kwenye Mtandao
Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari mawasiliano (TEHAMA), mfumo wa biashara pia umebadilika. Hivi leo ni rahisi kutuma na kupokea pesa, kuuza au hata kununua bidhaa kwa njia ya mtandao. Watu wengi hupenda kufanya manunuzi na mauzo ya bidhaa kwenye mtandao kutokana na urahisi wa upatikanaji wa bidhaa na huduma kupitia mtandao. Pamoja na nafasi hii kubwa ya mtandao katika maswala yanayohusu fedha, zipo changamoto mbalimbali zinazoandamana na miamala na manunuzi ya kwenye mtandao. Fahamu jinsi unavyoweza kujilinda unapofanya miamala au manunuzi mbalimbali kupitia mtandao.
1. Tumia kinga-virusi (antivirus) bora
Mtandao wa intanet ni chanzo kikubwa cha virusi na wadukuzi. Hivyo ni vyema ukatumia programu madhubuti kwa ajili ya kukukinga na virusi na wadukuzi mara unapofanya manu...