Kikombe cha Kisasa Kinachozuia Vitu Kumwagika - Fahamu Hili
Thursday, March 28Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Kikombe cha Kisasa Kinachozuia Vitu Kumwagika

Washirikishe Wengine Makala Hii:
mightmug
Kikombe cha MightMug
Chanzo cha picha: http://www.jennifermcgrail.com

Lengo kubwa la teknolojia ni kurahisisha maisha pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi. Kila siku kumekuwa kukibuniwa teknolojia mbalimbali hasa kwa lengo la kutatua matatizo mbalimbali yanayomkabili mwanadamu.

Inawezekana umewahi kupoteza nyaraka zako muhimu au hata kuharibu vifaa vyako vya thamani kama vile simu au kompyuta kutokana na kumwagikiwa vimiminika kama vile maji, kahawa au chai.

Teknolojia kutoka MightyMug inakuja na kikombe maalumu ambacho huzuia kinywaji kilichoko ndani yake kumwagika.

Inawezekana una mtoto mkorofi au unafanya kazi kwenye eneo lenye mitikisiko mingi; sasa kwa kutumia kikombe kutoka MightyMug utaepusha vitu vyako vya thamani kumwagikiwa vimiminika.

Sifa  za kikombe cha MightyMug

  • Kikombe cha MightyMug kina uwezo wa kujishikiza kwenye meza au dawati ambalo  kimewekwa. Hili hukifanya kisianguke kinapoguswa.
  • Kikombe cha MightyMug kina uwezo wa kutunza joto kwa saa 6 na baridi kwa saa 14.
  • Kikombe cha MightyMug hakitoi majimaji kwa nje. Kimetengenezwa kwa teknolojia inayokifanya kiwe kikavu muda wote.
  • Kikombe cha MightyMug kimetengenezwa kwa namna ambayo kinabebeka kirahisi, kina kifuniko kizuri na kinaweza kuwekwa kwenye sehemu ya kikombe kwenye gari bila shida.
  • Kimetengenezwa kwa mali ghafi bora isiyokuwa na kemikali hatari kama vile BPA inayopatikana kwenye vifaa vya plastiki.

Soma pia: Athari 5 za Kutumia Vyombo vya Chakula vya Plastiki

Unaweza kutazama video hii kuhusu kikombe cha MightMug

Upatikanaji wa kikombe cha MightyMug

Kikombe cha MightyMug kinauzwa kuanzia dola 16 kwenye tovuti ya watengenezaji ya MightyMug au tovuti ya Amazon.

Neno la mwisho

Naamini sasa hakuna haja ya kuharibu nyaraka au vifaa vyako vya thamani kutokana na kumwagikiwa vitu. Hauhitaji tena kutumia nguvu kubwa kulinda mtoto au mtu mwingine asimwage kinywaji chako; unachotakiwa kufanya ni kununua kikombe hiki, kuweka kinywaji chako na kukifurahia hadi tone la mwisho.

Je una swali au maoni? Tafadhali tuandikie maoni yako kisha washirikishe wengine makala hii. Unaweza kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x