China kujenga “mji msitu” ambao utakuwa na mamilioni ya mimea na miti 40,000. Kazi hii inatarajiwa kutekelezwa kwenye Mji Msitu wa Liuzhou ulioko katika milima ya kusini mwa Guangxi kabla ya 2020.
Mji huu uliobuniwa na msanifu majengo Stefano Boeri unatekelezwa sasa, ambapo nyumba, ofisi, shule na hosipitali zitafunikwa kabisa na miti na mimea mingine.
Mjii huu unatarajiwa kuchukua eneo la hekta 175, na utakapokamilika utaweza kuchukua watu takriban 30,000. Mji huo utakapokamilika utatumia usafiri wa treni ya umeme kutoka Liuzhou. Mji huo pia utatumia nishaji ya joto ardhi (geothemal) kwa matumizi ya ndani nyumba pamoja na umeme jua (solar).
Wanaamini kuwa kupanda miti zaidi kutanyonya tani 10,000 za hewa ukaa (C02) na tani 75 za hewa chafuzi nyingine, wakati huo ikizalisha tani 900 za oksijeni.
Utafiti uliofanyika mwaka 2015 unaonesha kuwa watu 4,000 hufa kila siku kutokana na uchafuzi wa hewa huko China; hivyo basi wanaamni kuwa mji huu utakuwa ni suluhisho la tatizo hili.
Miradi mingine mitatu kama hii inaendelea katika miji mingine ya China
Je una maoni gani kuhusu teknolojia na maendeleo haya yaliyofikiwa na China? Je teknolojia hii inaweza kuusaidia ulimwengu? Tupe maoni yako kisha washirikishe wengine.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.