
Makosa 8 ya Kuepuka Kabla na Wakati wa Kujenga Nyumba
Nyumba ni hitaji muhimu kwa watu wote. Kila mmoja anatamani na ana ndoto za kununua au kujenga nyumba nzuri na ya kisasa. Ni kweli kuwa ujenzi wa nyumba unahitaji rasilimali nyingi hasa fedha. Pamoja na gharama hizi za ujenzi wa nyumba bado watu wengi wamekuwa wakishindwa kupata nyumba nzuri huku wakiwa tayari wamepoteza kiasi kikubwa cha pesa. Ni wazi kuwa yapo makosa mbalimbali yanayosababisha hali hii yakiwemo yale ya ukosefu wa elimu pamoja na uzembe wa aina mbalimbali. Karibu ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu makosa 8 unayoweza kuyaepuka wakati wa kujenga nyumba ili hatimaye uwe na nyumba bora.
1. Kutozingatia kanuni za kununua kiwanja
Watu wengi hawafahamu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wanaponunua kiwanja. Hivyo hujikuta wakiingia katika matatizo mbalimbali kama vile ku...