Wanasayansi Wagundua Rangi inayotumia Jua Kuzalisha Nishati - Fahamu Hili
Thursday, April 25Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Wanasayansi Wagundua Rangi inayotumia Jua Kuzalisha Nishati

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Timu ya wanasayansi nchini Australia imegundua rangi ya sola ambayo inaweza kuzalisha nishati kwa ajili ya matumizi ya majumbani na magari. Timu hiyo iliyoongozwa na Torben Daeneke imesema kuwa inaamini kuwa njia hiyo itatoa nishati nafuu na safi kwa dunia.

Nishati kwa ajili ya magari siku za mbeleni

Inaweza kufikiriwa kuwa, kuendesha gari kwa nishati itokanayo na rangi ni kichekesho lakini wanayansi hao wamesema inawezekana. Wamesema kwa kuchanganya katalisti yenye rangi nyeupe inayotumika kwenye dawa ya meno, wanasyansi waliweza kutengeneza rangi ambayo ikikutana na jua inabadili maji kuwa hydrojeni ambayo itatumika kuendesha gari.

Wamesema changamoto waliyonayo ni namna ya kuhamisha nishati hiyo na kuitumia kwenye gari; pamoja na hili wamesema wameshapata njia kadhaa wanazozifanyia majaribio.

Wamesema pia hivi sana kuna magari mengi yanayotumia nishati ya hydrojen na nishati jua, hivyo kupatikana kwa niashati hii kutaokoa gharama pia itatunza mazingira kwa kupunguza utoaji wa hewa ukaa.

Nishati kwa ajili ya majumbani

Wanasayansi hao wameongeza kuwa rangi hii itaweza pia kutumika majumbani kama paneli za kawaida za sola. Wamesema upatikanaji wake utaoka ama kupunguza matumizi ya umeme wa kawaida.

Changamoto inayojitokeza hapa ni kuwa rangi hiyo ni nyeupe pekee; hivyo wapenzi wa rangi nyingine watakosa chaguo lao.

Makapuni ya kibiashara yatanufaika pia kwa kutumia rangi hii kwenye maofisi kwani itawaokoloea gharama za umeme mwimgi unaotumika maofisini.

Ratiba ya rangi hii ya sola

Wataalamu hawa wamesema wanatarajia ndani ya miaka mitano ijayo rangii hii itaanza kupatikana.  Mbali na hayo Daeneke amefahamisha kuwa rangi hiyo itakapokamilika itapatika kwa bei nafuu ambayo watu wataimudu.

Je wewe ungependa kutumia rangi hizi zitakapokamilika? Tuandikie maoni yako kisha washirikishe (share) na wengine.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x