
Njia 8 za Kuokoa Mafuta Unapoendesha Gari
Ni wazi kuwa gari linahitaji mafuta ili kusafiri toka sehemu moja hadi nyingine. Lakini swali ni je, unaweza kutawala kiwango cha mafuta kinachotumika? Ndiyo, unawea kutawana kiwango cha mafuta na kupunguza garama za matumizi ya mafuta zisizokuwa na ulazima. Kama unapenda kuokoa kiasi cha mafuta yanayopotea bila sababu ya msingi katika gari lako, basi tumia njia hizi 8 zifuatazo.
1. Kabili upepo
Unapoendesha gari upepo hukinzana na gari; hivyo kadri gari linavyokinzana zaidi na upepo ndiyo pia unavyotumia mafuta mengi zaidi. Hivyo basi, usipende kuweka mizigo juu ya gari kwa nje (carrier) au kufungua vioo kwani kutasabisha ukinzani zaidi kati ya gari na upepo. Kwa kukabili upepo vyema utapunguza ukinzani na kuokoa mafuta ambayo yangetumika kukabili ukinzani huo wa upepo.
2. Pu...