
Njia 8 Rahisi za Kupunguza Matumizi ya Umeme
Matumizi hayaepukiki kwenye maisha lakini kubana matumizi inawezekana. Yapo mambo mengi ambayo hugarimu fedha ili kuyamudu yakiwemo huduma kama maji, umeme, gesi na mafuta. Ni dhahiri kuwa ili kupunguza ugumu na changamoto za maisha ni vyema kujifunza namna ya kutumia vitu vyema. Unaweza kuokoa fedha nyingi ambazo zingepotea kwa kulipia gharama zisizo na sababu za matumizi ya umeme. Hivyo fahamu njia 8 rahisi za kupunguza matumizi ya umeme.
1. Zima taa na vifaa visivyokuwa na uhitaji
Mara nyingi umeme mwingi hupotea kutokana na kuacha vifaa mbalimbali vikiwa vimewashwa bila sababu. Si jambo la kustajabisha watu kusahau taa za nje ya nyumba hadi saa sita mchana; au hata kuacha vifaa kama vile redio, televisheni au kompyuta vikiwa vimewashwa mchana au usiku kucha bila sababu ya m...