Application/Programu 10 Muhimu za Kuwa Nazo Kwenye Simu (2017) - Fahamu Hili
Saturday, April 20Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Application/Programu 10 Muhimu za Kuwa Nazo Kwenye Simu (2017)

Washirikishe Wengine Makala Hii:

App za simu

Ni wazi kuwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la matumizi ya simu za mkononi hasa simu za kisasa (smartphone). Ni ukweli usiopingika kuwa yapo matumizi mengi ya simu za mkononi pamoja na programu zake (applications) ambayo bado hayajafahamika vyema kwa watumiaji wake.

Fuatilia makala hi ufahamu programu 10 muhimu kuwa nazo kwenye simu yako ili uwe mwenye tija zaidi.

1. Google Drive

driveGoogle drive ni zaidi ya hazina ya mafaili. Google Drive inakuwezesha kutengeneza ofisi yako ndogo yenye uwezo mzuri wa kuunda, kupanga, kuhariri na hata kusambaza mafaili mbalimbali kadri upendavyo.

2. Android Device Manager

ndroUkizingatia kwamba simu ni muhimu sana kwenye maisha yetu, tunahitaji kitu cha kutusaidia ikiwa jambo litakwenda vibaya. Android Device Manager itakuwezesha kufanya mambo kama vile kuibaini simu yako utakapo sahau ulipoiweka, kubadili nywila au neno la siri n.k.

3. Any.do

doWatu wengi huishi bila mpango. Ni vyema ukawa mtu mwenye mpango kwenye maisha na katika yale unayoyafanya. Kwa kutumia application hii unaweza kupangilia kazi na ratiba zako vyema.

Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

4. Avast Mobile Security

vastNi vizuri kutambua kuwa usalama ni jambo la kwanza. Kutokana na kuwepo kwa hatari mabalimbali hasa kwa simu zinazotumia Android, ni vyema ukajikinga kwa kutumia Kinga-virusi (antvirus) ya Avast. Avast ni nzuri kwani itakagua mafaili, WiFi, App na hata kuongeza kasi ya RAM ya simu yako.

Som pia: Fahamu Njia 6 za Kulinda Akaunti Zako za Mitandao ya Kijamii.

5. Google Chrome

chromGoogle Chrome ni kivinjari (browser) nzuri unayoweza kuitumia kuperuzi kurasa mbalimbali kwenye simu yako. Badala ya kutegemea kivinjari cha msingi au Firefox unaweza kutumia Google Chrome kwa urahisi zaidi.

6. Google Maps

mapTeknolojia imekuwa na imerahisisha maisha. Unaweza kwenda mahali popote sasa kwa kutumia tu mwongozo kutoka kwenye simu yako na kufika bila matatizo. Unaweza kuweka Google Maps kwa ajili ya kujifunza au hata kupata mwongozo wa eneo unalotaka kwenda.

7. Google photos

photoKama wewe ni mpenzi wa picha basi Google photos ni kwa ajili yako. Unaweza kuhifadhi, kupanga au hata kuzifikia picha zako kwenye Google photos bila tatizo lolote.

8. Minti

Kutunza pesa hasa kujiwekea bajeti kunaweza kuwa ni jambo gumu kwa watu wengi. Sasa unaweza kupanga na kusimamia matumizi yako kwa urahisi na karibu zaidi kwa kutumia app ya Mint kwenye simu yako.

Soma pia: Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema.

9. Snapseed

Kama wewe ni mpenzi wa kuhariri picha basi sanapseed inakufaa. Unaweza ukahariri picha kwa kutumia zana mbalimbali zinazopatikana kwenye Snapseed bure kabisa.

10. Facebook, Snapchat, Instagram, YouTube

Nimekusanya mitandao maarufu ya kijamii pamoja hapa uchague unaoupenda. Kama wewe ni mtumiaji wa Facebook basi pakua app ya Facebook ili uweze kutumia Facebook kwa ubora, urahisi na hata usalama zaidi. Pia unaweza kufanya hivi kwa mitandao yako mingine.

Soma pia: Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako.

Neno la Mwisho:

Ni wazi kuwa kwa sasa simu ni zaidi ya kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe mfupi. Naamini hutobaki tena nyuma kwenye kutumia simu yako kwa namna yenye tija baada ya kufahamu app hizi. Nikukumbushe kuwa zipo app nyingi sana lakini siyo zote zenye tija kwako; ni vyema pia ukachunguza usalama, ubora wa app na uwezo wa simu yako kabla hujaiweka app kwenye simu yako.

Je wewe unatumia app gani hapa? Je una swali au maoni? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine. Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

[picha za apps zimetoka pastemagazine]

5 1 vote
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x