Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda - Fahamu Hili
Friday, April 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda

Washirikishe Wengine Makala Hii:

alamu

Mambo yote katika maisha yetu yamefungwa kwenye muda, hivyo ni vyema kufahamu namna bora ya kutumia muda kwa njia yenye mafanikio.

Kutumia muda vyema siyo tu kutakuwezesha kufanya kazi vyema, bali kutakuwezesha kuishi maisha vyema. Ni muhimu kupata muda wa kufanya mambo yote ya muhimu kwenye maisha yako, kwani kila moja lina nafasi na umuhimu wake.

Hapa nitaeleza kanuni 9 yatakayokuwezesha kutawala muda vyema.

1. Anza na panga siku yako vyema

Usikimbilie kuanza majuku yako ya siku bila kukaa chini na kutumia dakika chache za kutafakari mambo kadhaa.

Tafakari ni jambo gani muhimu zaidi ili uweze kulipa kipaumbele katika siku yako.

Jifunze kujiwekea malengo, haya yatakuwezesha kujua nini unachotakiwa kukitimiza ndani ya siku yako. Kwa njia hii utaweza kukamilisha vitu kulingana na muda uliojiwekea.

Soma pia: Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani.

2. Gawanya kazi katika sehemu

Je uliwahi kusikia kanuni ya utawala wa wakoloni inayosema “gawanya na utawale”?

Hili pia lipo kwenye majukumu yako ya siku; unapogawanya kazi katika vipande vidogo vidogo ni rahisi kuzitawala na kuzifanya kwa wakati.

Kumbuka pia hata kazi ngumu huwa nyepesi kama itagawanywa katika sehemu ndogo ndogo kwani utaifanya kwa urahisi ndani ya muda uliopangwa vyema.

3. Weka vipaumbele

Jifunze kupanga kazi kulingana na vipaumbele vyake, usifanye kila kitu kwa sababu ni kazi bali fanya kwa kuongozwa na vipaumbele.

Jizoeze kusema “Hapana” kwa mambo, watu au kazi zisizokuwa na umuhimu. Ukifanya hivi utatumia muda wako vyema kwenye mambo ya muhimu kwanza.

Soma pia: Tabia 10 zitakazobadili maisha yako.

4. Gawa majukumu kwa watu wengine

Usifanye kila kazi kwa kuwa unaweza kuifanya. Kama una mtu au watu ambao unaweza kuwagawia majukumu fanya hivyo, kwani kwa njia hii kazi nyingi zitafanyika ndani ya muda mfupi.

Bainisha kazi zinazoweza kufanywa na wengine, andaa muongozo wa kuzifanya kisha acha watu wengine wazifanye.

5. Panga ratiba

Watu wengi hawana ratiba rasmi ya siku, huzoea kwenda kwa mazoea tu. Jifunze kujiwekea ratiba kisha uiheshimu na kuifuata vyema.

Panga muda wa kula, kupumzika, vikao, n.k. Hili litakuwezesha kuwa na mwongozo mzuri wa namna utakavyopanga kazi zako.

Epuka kufanya mambo yasiyokuwa kwenye ratiba; ukifanya hivi utatumia muda vyema na utakuwa na maisha yenye tija zaidi.

Soma pia: Faida 7 za Kuwa na Ratiba Binafsi.

6. Tenga muda wa kupumzika

Inawezekana unajitahidi kufanya kazi fulani kwa bidii ili uikamilishe kabla ya tarehe ya mwisho, lakini nini kitatokea kama utaendelea hivyo kwa muda mrefu?

Ni wazi kuwa mwili utachoka na ufanisi wako utapungua pia. Jifunze kutenga muda wa kupumzika, kwani hili litafanya mwili na akili yako kuwa katika hali bora zaidi yenye kukuwezesha kufanya kazi vyema.

Soma pia: Faida 10 za Kupumzika.

7. Jiwekee ukomo wa muda

Ili kutumia vyema muda, unaweza kutumia kanuni ya kujiwekea ukomo wa muda unaotakiwa kutumika kwa kila kazi.

Kwa mfano unaweza kuweka kuwa kazi X inatakiwa imalizike baada ya saa 2. Ukizingatia njia hii bila kuikiuka utajikuta unatumia muda uliojiweka vyema kukamilisha kazi husika.

8. Panga kesho leo

Kila siku fahamu kuwa kesho huandaliwa leo. Hivyo ni vyema ukaweka mikakati kadhaa ya kazi zitakazofanyika siku ya kesho.

Bainisha kitakachoanza kesho, kama kuna kazi haikukamilika leo basi panga kuikamilisha kesho kwanza.

Soma pia: Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako.

9. Ondoa vitu vinavyokuvuruga

Kuna shunguli na vitu mbalimbali vinavyoweza kuingilia utendaji wako wa kazi pamoja na matumizi yako ya muda.

Maswala kama vile mitandao ya kijamii, televisheni, miziki na filamu, mazungumzo na marafiki n.k. Ni baadhi ya mambo ambayo yasipodhibitiwa yanaweza kukupotezea muda mwingi.

Hivyo ni vyema ukajitahidi kuondoa mazingira yenye vitu tajwa hapo juu ili utumie muda wako vyema kufanya kazi zenye tija.

Soma pia: Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako.

Neno la Mwisho

Muda ni rasilimali muhimu sana ambayo tunatakiwa kuitumia vyema ili tufanikiwe.

Naamini makala hii imekusaidia kwani hutopoteza tena muda wako bali utaweza kuutumia vyema kwa njia yenye tija.

Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini. Pia usisahau kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook pamoja na kuwashirikisha wengine makala hii.

4.6 11 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

6 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Frank Nkingwa
Frank Nkingwa
4 years ago

Barikiwa kwa makala hii

Oscar mushi
Oscar mushi
3 years ago

Asante sn

Johanes Trojanus
Johanes Trojanus
1 year ago

Nimefaidi mambo mengi sana kutoka humu.. Mwandaaji Mungu aendelee kukutia maarifa zaidi Good job big up sana🔥

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x