
Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda
Mambo yote katika maisha yetu yamefungwa kwenye muda, hivyo ni vyema kufahamu namna bora ya kutumia muda kwa njia yenye mafanikio. Kutumia muda vyema siyo tu kutakuwezesha kufanya kazi vyema, bali kutakuwezesha kuishi maisha vyema. Ni muhimu kupata muda wa kufanya mambo yote ya muhimu kwenye maisha yako, kwani kila moja lina nafasi na umuhimu wake. Hapa nitaeleza kanuni 9 yatakayokuwezesha kutawala muda vyema.
1. Anza na panga siku yako vyema
Usikimbilie kuanza majuku yako ya siku bila kukaa chini na kutumia dakika chache za kutafakari mambo kadhaa. Tafakari ni jambo gani muhimu zaidi ili uweze kulipa kipaumbele katika siku yako. Jifunze kujiwekea malengo, haya yatakuwezesha kujua nini unachotakiwa kukitimiza ndani ya siku yako. Kwa njia hii utaweza kukamilisha vitu kulingana na muda...