Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako - Fahamu Hili
Saturday, April 20Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Afro_amer

Mtu wa kwanza anayekuzuia kufanikiwa ni wewe mwenyewe; sio jamii, siyo serikali au mtu mwingine yeyote katika maisha yako. Ni kweli kuwa baadhi ya watu huanza maisha katika mazingira rafiki zaidi, lakini ninaamini kila mmoja ana nafasi na uwezo ya kufanikiwa.

Haya ni baadhi mambo ambayo watu wengi wamekuwa wakiyafanya na kujiambia na yamewatenga na mafanikio yao.

1. Ninahitaji shahada ya chuo kikuu ili kufanikiwa

Unahitaji shahada kupata kazi katika ofisi fulani lakini si kuwa majasiriamali katika ofisi yako wewe mwenyewe.

Ipo mifano kadha wa kadha duniani ya watu waliofanikiwa na kuwa mabilionea wakubwa bila kuwa na shahada ya chuo kikuu. Mfano wa watu hao ni Mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg. Hivyo basi fanya maamuzi leo ili ufikie kiwango bora cha maisha kwani kizuizi pekee ni wewe.

Soma pia: Kitu Muhimu Mark Zuckerberg Alichokijenga Harvard.

2. Sina muda wa kutosha

Hili ni swala ambalo watu wengi hulalamikia kila siku kuwa hawana muda kutosha. Fahamu kuwa hakuna binadamu duniani mwenye zaidi ya saa 24. Hivyo kama unapata muda wa kutumia mitandao ya kijamii, kucheza michezo ya kompyuta au kuchati kwa simu basi una muda mwingi mno kuliko unavyofikiri.

Badilisha fikra zako leo, jifunze kutumia muda wako vyema ukijiwekea vipaumbele na malengo ya kukamilisha kila siku.

Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

3. Umri wangu umeenda sana

“Haujachelewa kuwa ambaye ungeweza kuwa.”

George Eliot

Watu wengi wamekuwa wakihofia swala la umri, hasa pale wanapotazama na kuona kuwa hawapo kwenye miaka kati ya 20 hadi 30. Lakini ukweli ni kwamba umri sio kizuizi bali fikra zako ndiyo kizuizi.

Usikubali kuacha ndoto na malengo yako yafifie gizani. Amka!, amka sasa na ufanye maamuzi tekelevu juu ya maono na mipango yako.

4. Ni vigumu kuanza

Ni kweli kuwa hata wahenga walisema “mwanzo ni mgumu” lakini hilo sio kanuni. Kila mtu duniani angewaza mwanzo ni mgumu nafikiri tungekuwa bado kwenye zama za ujima.

Jifunze kwa waliofanikiwa, walianzaje? walizikabili vipi changamoto? Siku zote jifunze kuona mafanikio kabla ya changamoto, hili litakupa hamasa na kiu ya kufanya bidii hata kuzishinda changamoto.

Soma pia: Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo.

Neno la mwisho: Chukua hatua ya kwanza leo

Inasikitisha kuona kuwa watu wengi hawafikii malengo yao kwa sababu ya mambo wanayojiambia au kujiwazia wenyewe. Ninakuhamasisha kuwa, kama unapumua basi unaweza kufanikiwa. Inaweza kuchukua muda lakini ukiamua unaweza.

Soma pia: Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa.

Je umenufaika kutokana na makala hii? Tafadhali tuandikie maoni yako kisha washirikishe wengine makala hii. Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3 6 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

2 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Ngowi
Michael Ngowi
4 years ago

Naomba ushauri Nina 30000 nimrmelza kidato cha NNE 2018 nimeshindw kuendelea nifanye nn na hii pesa

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x