Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara - Fahamu Hili
Sunday, December 3Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara

Washirikishe Wengine Makala Hii:

ofisi

Uteuzi wa jina la biashara ni hatua muhimu kama ilivyo kwa jiwe la pembeni katika nyumba. Watu wengi wamekuwa hawatilii maanani mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua jina la biashara au kampuni.

Nimekuwa nikishuhudia makapuni mengi yakitumia majina ya ajabu ajabu yasiyoendana na biashara zao. Kwa sehemu kubwa kufanikiwa na kujulikana kwa biashara yako kunategemea jina la biashara yako.

Fuatana nami katika makala hii ambayo nitakueleza mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua jina la biashara.

1. Uhusiano wa jina na bidhaa au huduma

Je unafahamu kwamba jina la biashara linatakiwa liakisi huduma au biashara unayoifanya? Ni jambo jema kutumia jina linaloakisi kile unachokifanya. Kwa mfano jina kama vile “Samelctro” lifaa kwa kampuni ya vifaa vya kielektroniki, “Pamba LTD” lifaa kwa kampuni ya upambaji au mavazi.

Itakuwa ni jambo la kushangaza kutumia “Samelctro” kwenye mavazi au kutumia “Pamba LTD” kwenye vifaa vya kielektroniki. Ukizingatia hili mapema utaweza kuitambulisha bidhaa au huduma yako vyema kwa kupitia jina la biashara yako.

2. Jina fupi linalovutia na kueleweka

Uchaguapo jina la la biashara au kampuni yako kaa chini tafuta jina fupi lenye mvuto na linaloeleweka.

Usitumie majina magumu na marefu kama vile “matunda bora ya shamba”, “rextymyshoes” “mauaborasana”, “John Noe na Rose Mewa Beauty Saloon”, n.k. Chagua jina fupi linalovutia ambalo pia ni rahisi kwa watu kulikumbuka.

3. Zingatia mahitaji ya kimtandao

Katika swala hili nimeshuhudia watu wengi wakichukua majina ya biashara au kampuni bila kujali swala la matumizi ya mtandao. Kwa mfano mtu anaweza kusajili kampuni inayoitwa hope, smart, green nk.

Majina haya huwezi kuyatumia kwenye mtandao kwani tayari yameshatumika katika mambo mengi sana; hapa hutoweza kupata huduma kama vile anwani ya tovuti au baruapepe inayoendana na jina la kampuni yako.

Hivyo basi tumia huduma kama vile (Whois) kutazama kama unaweza kupata anwani ya matandao inayoendana na jina la kampuni au laa.

Kumbuka haina maana kampuni kuitwa Moja LTD halafu ikawa na tovuti inayoitwa “http://mbili.com”; hapa utapoteza watu, hawataweza kuifikia tovuti yako vyema.

4. Upekee

Kama nilivyoeleza katika hoja zilizopita hapo juu ni muhimu kuhakikisha unabuni jina lenye upekee kwa ajili ya biashara yako. Epuka kutumia majina yanayofanana na majina mengine.

Kumbuka zipo shereia za kimataifa zinazolinda majina ya kibiashara (Brands) za kampuni mbalimbali; majina kama vile Microsofti, Thetoyota, Delli, Vodacomu n.k yatakupelekea kuingia kwenye mgogoro wa kisheria na makampuni husika kwani majina haya yanalandana sana na majina ya kampuni zao.

Soma pia: Makosa 10 ya Kuepuka Unapotengeneza Logo au Nembo.

5. Zingatia mahitaji ya baadaye

Inawezekana jina la kampuni au biashara linalofaa leo lisifae tena kwa ajili ya biashara yako baadaya ya miaka mitano. Hivyo ni vyema kuchagua jina ambalo utadumu nalo katika kampuni yako.

Kwa mfano mtu akiita kampuni yake 3GNetworks au 4GNetworks, baada ya mika mitano 3G na 4G kwenye jina hazitakuwa za maana tena kwani tutakuwa tayari tuna teknolojia mpya za 5G n.k.

Hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa jina unalolichagua leo litakufaa pia kwa upanuzi na matumizi ya baadaye ya biashara yako.

Hitimisho

Kwa kuhitimisha ninapenda kukushauri kuzingatia umakini na utafiti wa kutosha katika kuchagua jina la biashara yako. Hakikisha kama unahusisha watu wengine katika machakato huu wawe ni wale wanaoilelewa vyema biashara au kampuni yako.

Je bado umekwama katika hatua hii ya uchaguzi wa jina la biashara au kampuni? Tafadhali tuandikie maoni na maswali yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii.

3.8 8 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

26 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Noely chambua
Noely chambua
5 years ago

Naomba kutafhtiwa jina la biashara

Zainab
Zainab
4 years ago

Naomba jina

malik
malik
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Bro kwema,samahani naomaba unichagulie jina la saloon, mimi nilitaka kuandika mama akram beauty saloon, je unanishauri vipi au niandikaje tafadhali

Kaduma
Kaduma
Reply to  Kornelio Maanga
1 year ago

Halooo…
HONGERA sana kijana mwenzang
Kutupa madini MUHIMU..

Abubakari
Abubakari
4 years ago

Naomba kusaidiwa kupata jina zuri la kikundi chetu tulichomaliza shule kwa pamoja mwaka 2015 nataka likae kwenye nembo yetu ya kikundi

Amos simion
Amos simion
4 years ago

Ndio mm ni amos simion nashindwa namna ya kuazisha jina la biashara ambalo nitatumia kwenye kanpuni

Amos simion
Amos simion
4 years ago

Ndio mm nashindwa nitumie jina gani

Petro Madaha
Petro Madaha
4 years ago

Naomba jina la biashara yangu ya kuuza maji

Sabby
Sabby
4 years ago

Nikefanikiwa kupata mlango wa ofisi nataka niuze fresh juice aina zote na pafyum… Je nitumie jina gani? Msaada please

Fatuma athuman
Fatuma athuman
3 years ago

Naomba unisaidie kupata jina nimefungua biashara ya uuzaji vifaa vya ushonaj cherehan na urembo kama lotion mafuta nk.

Izack mwageni
Izack mwageni
3 years ago

Nimewakubali sana kwa maelezo yetu Mungu awabariki

Witness
Witness
3 years ago

Msaada mi nimsanii natamani nipate jina ntakaloweza kulitumia kwenye ka I zangu na hata kampuni yangu ya baadae

Jisandu kuyeka
Jisandu kuyeka
5 months ago

Asante Sana mwalimu hakika nimejifunza jambo

26
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x