Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka - Fahamu Hili
Wednesday, February 28Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka

Washirikishe Wengine Makala Hii:

maji

Kwanini ni muhimu kunywa maji?

Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo.

Ninawezaje kutumia maji kama tiba?

Unaweza kutumia maji kama tiba ya matatizo mbalimbali kwa kufanya haya yafuatayo:

  • Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka.
  • Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni.
  • Kama huwezi kunywa angalau bilauri 4 za maji basi anza na moja kisha ongeza taratibu kadri mwili wako unavyomudu.

Karibu ufahamu faida 8 za msingi za kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka.

1. Huondoa sumu mwilini

Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema. Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.

Soma pia: Njia 12 za Kuondoa Sumu Mwilini.

2. Huboresha metaboli

Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) ili kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema.

Kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka huufanya utumbo kuwa tayari kufyonza virutubisho. Kumbuka, maji ni muhimu kwa ajili ya watoto na watu wazima pia.

3. Husaidia kupunguza uzito

Wapo watu wanaopenda kupunguza uzito wa miili yao kwani uzito mkubwa si jambo zuri kiafya. Yakupasa kukumbuka kuwa unapoamka na kuanza kutumia vinywaji kama vile soda na juisi (sharubati) vitachangia sana kuongeza uzito wako wa mwili.

Utafiti unaonyesha kuwa soda ina sukari gramu 35 na gramu 140 za kalori ikilinganisha na maji ambayo vyote ni sifuri. Hivyo basi, ni vyema ukapendelea kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vingine.

4. Huondoa kiungulia na matatizo ya umeng’enyaji wa chakula

Kunywa maji kutakusaidia kuzimua asidi inayopatikana tumboni ambayo ndiyo hupelekea tatizo la kiungulia. Sanjari na hayo unywaji wa maji utarahisisha na kuhimiza mchakato mzima wa umeng’enywaji wa chakula.

Hivyo basi, kama unakabiliwa na matatizo haya ni vyema kuzingatia unywaji wa maji kabla ya kutumia dawa mbalimbali.

5. Huboresha na kuimarisha ngozi

Utafiti unaonyesha kuwa kunywa maji takriban mililita 500 kunarahisisha mzunguko mzuri wa damu katika ngozi. Hivyo basi, hili hupelekea kuondoa sumu mbalimbali katika ngozi na kuiacha ngozi yako katika hali nzuri kiafya.

Soma pia: Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu.

6. Huhamasisha ukuaji wa nywele bora zenye afya

Upungufu wa maji mwilini una madhara makubwa sana kwa afya yako. Utafiti unaonyesha kuwa ¼ ya uzito wa nywele zako ni maji. Hivyo kutokunywa maji yakutosha kutakufanya kuwa na ukuaji duni wa nywele; pia kutafanya nywele zako kuwa dhaifu.

Kwa ajili ya afya na mwonekano bora wa nywele zako jidahidi kunywa maji yakutosha hasa unapoamka asubuhi.

7. Huzuia mawe kwenye figo

Unywaji wa maji huzimua asidi inayosababisha mawe kwenye figo ambayo hupatikana tumboni. Unywaji wa maji ya kutosha kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na matatizo ya figo.  Ili kurahisisha utendaji kazi wa figo zako pamoja na afya yake, zingatia kunywa maji ya kutosha hasa asubuhi.

Soma pia: Rangi 11 za Mkojo na Maana Zake Kwenye Mwili wako.

8. Huongeza kinga ya mwili

Kujijenga kwa kinga mwili hutegemea sana maji katika mwili wako. Hivyo ni vyema kuhakikisha unaongeza kinga ya wili wako kwa kunywa maji ya kutosha hasa kabla ya kula kitu chochote.

Neno la mwisho

Ninakuhimiza kujenga utamaduni wa kujali na kulinda afya yako ili uweze kuwa mtu mwenye mafanikio zaidi. Tumeona swala la unywaji wa maji lilivyo na umuhimu; swala hili ni wewe kuamua tu kulifanyia kazi kwani halina gharama yoyote.

Je wewe huwa unakunywa maji? Kiasi gani na saa ngapi? Tupe maoni yako kisha washirikishe wengine makala hii. Karibu pia ulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3.7 38 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

34 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Amina
Amina
5 years ago

Thanks so much indeed I have learned alot

Kornelio Maanga
Reply to  Amina
5 years ago

Asante sana; karibu tena Fahamuhili.com

Kulwa Alphonce
Kulwa Alphonce
5 years ago

Nimependa makala zenu ni nzuri na zinaelimisha iwapo mtu ataamua kuzifatilia kwa umakini mzuri Asanteni sana kwa elimu nzuri
Swali Kunywa maji wakati wa asubuhi ni lazima uwe ujasukutua tu
Au hata ukiwa umeishasukutua nayo ni nzuri? naomba jibu

Kornelio Maanga
Reply to  Kulwa Alphonce
4 years ago

Nashukuru sana kwa kutembelea blog yetu ya Fahamuhili; tunashukuru pia kwa maoni yako mazuri. Jambo muhimu ni kuzingatia kunywa maji ya kutosha asubuhi: haijalishi ni baada ya kusukutua au la. Karibu sana Fahamuhili.com

Tatu khalid
Tatu khalid
Reply to  Kulwa Alphonce
3 years ago

Asante san kwa nakala nzuri cha kuongezea ni kuwa tunashauliwa kabla ya kulala tupige mswaki kisha asubuh kabla ya kupiga mswaki tunywe maji kwani bacteria wanaokuw kinywani muda uo wanafaida mwilini na kusaidia kutibu maradhi kama malaria nk shukran

said
said
4 years ago

asanteni sana kwa kutuelimisha

Kornelio Maanga
Reply to  said
4 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Baraka
Baraka
Reply to  Kornelio Maanga
1 year ago

Maji ni muhimu sana ndomana Mungu amesema katika Kitibu chake kitakatifu Qur an. Amejaalia kutojana na maji uhai.

John uo
John uo
4 years ago

Nashukuru sana

Kornelio Maanga
Reply to  John uo
4 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

John uo
John uo
4 years ago

Nimeelewa sana unywaji wa maji ingawa watu hulipuuza

Kornelio Maanga
Reply to  John uo
4 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Teckla mgani
Teckla mgani
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Samahani nauliza hayo ya kunywa Asb je yanatakiwa yawe uvuguvugu au ya kawaida

Kornelio Maanga
Reply to  Teckla mgani
3 years ago

Tofauti yake ni ndogo kimatokeo; bali nafasi ya maji ni ile ile ndugu; kunywa aina ile ambayo unaona inakupendeza zaidi. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Greyson
Greyson
4 years ago

Naitaj kujua maji hayo ambayo tunatakiwa kunywa ni ya moto au baridi

Kornelio Maanga
Reply to  Greyson
3 years ago

Yale ambayo unaona unapendezwa nayo, nafasi ya maji mwilini ni ile ile. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Gitonga
Gitonga
4 years ago

tupemegine mengi utusaidie

Kornelio Maanga
Reply to  Gitonga
3 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Glory mwanga
Glory mwanga
3 years ago

Makala nimeipenda kwa kweli

Kornelio Maanga
Reply to  Glory mwanga
3 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani kwetu; karibu sana Fahamuhili.com

EDGAR
EDGAR
3 years ago

Asante sana kwa uponyaji!

Kornelio Maanga
Reply to  EDGAR
2 years ago

Utukufu kwa Mungu; Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Yassin
Yassin
3 years ago

mi huwa nakunywa maji takribani lita moja na nusu kwa siku

Kornelio Maanga
Reply to  Yassin
2 years ago

Hongera sana; Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Abdalla Omar Abdalla
Abdalla Omar Abdalla
2 years ago

Mimi nakunywa maji asubuhi nikisha swali kabla ya kula kitu, nakua nakunywa glasi 2 tu.

Kornelio Maanga
Reply to  Abdalla Omar Abdalla
2 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

kiruibenvin@gmail.com
kiruibenvin@gmail.com
2 years ago

Asante nilikuwa na hofu Kwa sababu Mimi nanywa maji.mingi

Kornelio Maanga
Reply to  kiruibenvin@gmail.com
1 year ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Darudaru
Darudaru
1 year ago

Samahani nataka kuuliza unaweza kunywa maji asubuhi ukachanganya na limao? Je, kuna madhara yoyote kiafya na pia kuna faida gani kiafya.

Annastazia michael
Annastazia michael
1 year ago

Asante sana kwa kutupatia mambo muhimu kama hayo

Kornelio Maanga
Reply to  Annastazia michael
6 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Myco Stanford Sekachu
Myco Stanford Sekachu
1 year ago

Takribani nina siku4 nimeanza kunywa maji, ila siku zote nilikua nakunywa nusu lita ila leo ndio nimekunywa lita moja
Nikaona vyema niingie mtandaoni kujua zaidi faida za kunywa maji
Kifupi mko vizuli na maeleweka na mungu awabariki sana

Kornelio Maanga
Reply to  Myco Stanford Sekachu
1 year ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Saidi Mustapha
Saidi Mustapha
1 year ago

Hallow nina swali hapa, nini kinacho sababisha joto kali sana baada ya kunywa pombe kali kesho yake asubuhi na kuendelea.

34
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x