Madhara 12 ya Pombe Kiafya - Fahamu Hili
Thursday, April 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Madhara 12 ya Pombe Kiafya

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Pombe

Siyo siri kuwa pombe husababisha matatizo makuwa ya kiafya, yakiwemo magonjwa ya moyo, ini pamoja na majeraha yatokanayo na ajali zitokanazo na ulevi. Ni dhahiri kuwa vinywaji halisi vilivyotengenezwa kwa matunda bila kilevi ni bora zaidi kwa afya yako kuliko vile vyenye kilevi.

Licha ya kuwepo kwa kampeni kadha wa kadha zinazopinga matumizi ya pombe, bado watu wengi wameendelea kushikilia kinywaji hiki bila kufahamu athari zake kwenye afya zao. Fuatilia hapa chini athari 12 za pombe kiafya.

1. Matatizo ya moyo

Unywaji mkubwa wa pombe husababisha  matatizo mbalimbali ya moyo kama vile cardiomyopathy, ambapo mishipa ya moyo hudhoofika na kushindwa kusukuma damu. Jambo hili huweza kusababisha damu kuganda na kusababisha kiharusi (stroke). Pombe huchangia sana katika kudhoofisha mishipa ya moyo hivyo kupelekea ugonjwa huu wa cardiomyopathy na mengine hatari.

2. Tatizo la ini

Unywaji wa pombe unaweza kusababisha maradhi ya ini yajulikanayo kama Cirrhosis; ambayo ni maradhi ya ini kushindwa kufanya kazi yake kutokana na uharibifu wa muda mrefu. Uharibifu huu husababisha seli za ini kuwa makovu na kushindwa kufaya kazi vyema. Utafiti umebaini kuwa pombe huchangia sana katika kuharibu seli hizi za ini.

3. Shinikizo la damu

Unywaji wa pombe hasa kupitiliza umedhibitishwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maradhi ya shinikizo la damu. Imebainikia kuwa pombe huathiri mfumo wa usukumaji wa damu mwilini jambo ambalo hupelekea shinikizo la damu na baadye matatizo mengine kama kushindwa kwa figo, ini n.k.

4. Magonjwa ambukizi

Mara nyingi mtu anapokunywa pombe hupoteza uwezo wa kutawala mwili na maamuzi yake. Hivyo ni rahisi baada ya mtu kunywa pombe akafanya au akajiingiza kwenye matendo hatarishi yanayoweza kumfanya kuambukizwa magonjwa kama vile UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.

5. Ugonjwa wa anemia

Anemia ni ugonjwa unaotokana na kushindwa kwa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha kwenda kwenye mwili. Hivyo unywaji wa pombe hupunguza uwezo wa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha hivyo kupelekea ugonjwa wa anemia.

6. Saratani

Utafiti uliofanywa na daktari Jurgen Rehm, PhD, wa chuo cha Toronto umebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani kutokana na unywaji wa pombe. Utafiti huu ulieleza kuwa tatizo huanza pale ambapo mwili hubadili kilevi (alcohol) kuwa kemikali iitwayo “acetaldehyde”.

Saratani huweza kutokea kwenye koo, shingo, mdomo na mapafu. Pia aliongeza kuwa atari inaongezeka pale ambapo mtumiaji wa pombe pia ni mvutaji wa sigara.

7. Kusinyaa kwa ubongo

Kadri umri wa mtu unavyozidi ndivyo na ubongo wake unavyozidi kusinyaa. Hivyo unywaji wa pombe huharakisha kusinyaa kwa ubongo kwa silimia 1.9. Hili hupelekea matatizo yatokanayo na kusinyaa kwa ubongo kama vile kupoteza au kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu.

8. Msongo wa mawazo

Pombe huathiri mchakato wa kikemikali wa ubongo (Kemia ya ubongo). Kutokana na utafiti uliofanywa, imebainika kuwa watu wanaokunywa pombe nyingi hukabiliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Msongo wa mawazo ni chanzo cha maradhi mbalimbali kama vile shinikizo la damu, matatizo ya akili, matatizo ya moyo na wakati mwingine kifo.

9. Maumivu ya miguu (gout/jongo)

Gout au jongo ni ugonjwa wa miguu unaotokana na kukusanyika kwa asidi kwenye viungio vya mifupa. Mara nyingi ugonjwa huu hujitokeza sana majira ya baridi. Pamoja na vyanzo vya sababu za kurithi za ugonjwa huu, pombe imedhihirika kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ugonjwa huu.

10. Uharibifu wa mfumo wa fahamu

Hivi leo pombe mbalimbali hutengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali, kemikali hizi kwa kiasi kikubwa huwa na athari kwenye mfumo wa fahamu. Pombe huathiri mifumo na utendeji kazi wa mfumo mzima wa fahamu na kusababisha matatizo kama vile udhaifu wa misuli na matatizo katika milango la fahamu.

Hii ndiyo sababu mtu anayekunywa pombe kali anashindwa kuhisi landa za vitu kama vile chumvi au pilipili vyema; hivyo hujikuta akitumia kwa kiasi kikubwa.

11. Kusinyaa kwa uso na macho

Unywaji mkubwa wa pombe husababisha kusinyaa kwa uso na macho hasa kwa wale wanaokunywa usiku. Mara ngingi uwatazamapo wanywaji wakubwa wa pombe utaona hata sura zao zimebadilika na kuonekana zimezeeka au kuchoka kuliko awali.

Ni dhahiri umewahi kumwona kijana mlevi wa miaka 25 lakini anaonekana kama mzee wa mika 40. Hii ni kutokana na athari zinazosababishwa na unywaji mkubwa wa pombe.

12. Huathiri mifumo ya uzazi

Kumekuwa na mawazo kadha wa kadha kuhusu pombe na maswala ya uzazi. Wengine huamini kuwa pombe huboresha maswala ya uzazi huku wengine wakiamini kuwa pombe huathiri maswala ya uzazi. Ukweli ni kuwa pombe ina madhara kadha wa kadha kwenye maswala ya uzazi kama ifuatavyo:

  • Husababisha kukutana kimwili kusiko salama.
  • Huathiri nguvu za kiume.
  • Huathiri mtoto aliye tumboni kwa mama.
  • Husababisha watu kufanya matendo binafsi au ya aibu hadharani.

Je bado unatamani kuendelea kukumbatia pombe katika maswala ya uzazi? Naamini utafanya uamuzi sahihi sasa.

Soma pia: Njia 12 za Uhakika za Kuacha Pombe.

Neno la Mwisho

Maamuzi ya kujenga au kubomoa maisha yako kutokana na pombe ni ya kwako. Naamini umefahamu madhara kadha wa kadha ya pombe kiafya. Kumbuka kuwa yapo pia madhara ya kijamii, kiuchumi na hata kiimani kwa wale waaminio.

Usauri wangu kwako ni kuwa hakuna mtu aliyewahi kufa kutokana na kuacha kutumia pombe. Hivyo jenga mwili wako kwa lishe bora ili uwe mwenye tija zaidi.

Soma pia: Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka.

Je una swali au maoni yoyote kutokana na makala hii? Tafadhali tuandikie maoni yako kisha washirikishe na wengine.

3 7 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

10 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Thomas Nkaina
Thomas Nkaina
4 years ago

Ni kweli pombe inamadhara makubwa sana kiafya na mfumo mzima was uzazi

Kornelio Maanga
Reply to  Thomas Nkaina
3 years ago

Ni kweli, mwenye sikio la kusikia asikie, jitahidi kuiepuka ndugu ili ulinde afya na baadaye yako. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Coletha pius
Coletha pius
1 year ago

Pombe n hstar

Kornelio Maanga
Reply to  Coletha pius
1 year ago

Hakika ni hatari. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Philemon Shija
Philemon Shija
1 year ago

Nitumie Makala nyingi zaidi

Kornelio Maanga
Reply to  Philemon Shija
8 months ago

Tutafanya hivyo. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

bene
bene
1 year ago

andiko zuri sana nimejifunza sana

Kornelio Maanga
Reply to  bene
8 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Elia
Elia
10 months ago

Sihitaji Tena pombe na Mungu awe Nani..🙏🏻🙏🏻

Kornelio Maanga
Reply to  Elia
8 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

10
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x