Sababu 10 za Kwa nini Unatakiwa Kuacha Kuvuta Sigara - Fahamu Hili
Sunday, December 3Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Sababu 10 za Kwa nini Unatakiwa Kuacha Kuvuta Sigara

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Uvutaji wa sigara

Kuna baadhi ya tabia kuzianza ni rahisi sana, lakini kuziacha kunakuwa ni kugumu. Watu wengi hasa vijana, hushawishiwa na marafiki kuingia kwenye tabia kama vile unywaji wa pombe, uvutaji sigara au kutumia madawa ya kulevya bila kufahamu madhara yake.

Hakika kuna madhara mengi sana yatokanayo na uvutaji wa sigara kiafya, kiakili, kijamii na kiuchumi.

Ikiwa basi unataka kufahamu sababu za kwanini unatakiwa kuacha kuvuta sigara, basi karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe sababu 10 za kuacha kuvuta sigara.

1. Unaokoa pesa

Moja kati ya mambo yanayowapotezea watu pesa ni tabia kama vile uvutaji wa sigara.

Kwa kuacha kuvuta sigara utaweza kuokoa pesa ambazo huwa unazitumia kwa ajili ya kununua sigara, na kuzitumia kufanya mambo mengine yenye manufaa kwako.

Soma pia: Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema

2. Unarudisha afya yako

Uvutaji wa sigara huathiri afya ya mwanadamu kwa namna mbalimbali. Hivyo kuacha kuvuta sigara kutakuepusha na maradhi kama vile shambulio la moyo, saratani ya mapafu, kuzeeka kwa ngozi, matatizo ya ubongo, n.k.

3. Utaishi muda mrefu

Nicotine inayopatikana kwenye sigara huathiri mishipa ya damu kwa kuifanya iwe miyembamba na kusababisha damu kutokupita vizuri.

Ikiwa damu haitasafiri sawasawa, sehemu za mwili kama vile ubongo utakosa kiwango cha kutosha cha damu, jambo linaloweza kusababisha kiharusi na hatimaye kifo.

4. Unalala vizuri

Ikizingatiwa kuwa nicotine ni kichochezi (stimulant) ambacho hufanya ubongo wako kutokutulia na kukuruhusu kulala vyema.

Hivyo kuacha uvutaji wa sigara kutakuwezesha kupata usingizi mzuri na hatimaye kuwa na afya njema.

Soma pia: Njia 13 za Kupata Usingizi Mzuri/Kulala Vizuri

5. Unapona vidonda mapema

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo Kikuu cha Washington mwaka 2007, unaeleza kuwa uvutaji wa sigara huchelewesha kwa kiasi kikubwa kupona majeraha ya vidonda.

Hivyo hakuna haja ya kuvuruga mchakato wa wewe kupona majeraha kwa sababu ya kutumia sigara.

Soma pia: Mambo Matano ya Kufanya ili Kuharakisha Kupona Majeraha

6. Unaweza kujitawala

Sigara hukufanya kuwa mtawaliwa (addicted). Mara nyingi mtu anayevuta sigara hushindwa kujitawala, anaweza kuvuta hata usiku wa manane, hosipitalini, maeneo yenye mikusanyiko, n.k. bila kuweza kujizuia.

Hivyo kuacha sigara hukufanya uweze kujitawala tena na si kutawaliwa na sigara.

7. Unalinda wanaokuzunguka

Moshi wa sigara una zaidi ya kemikali 4,000 na 43 kati yake zinafahamika wazi kusababisha saratani za aina mbalimbali. Hivyo uvutaji wa sigara haukuathiri tu wewe bali hata wale wanaokuzunguka, hasa wanafamilia.

Kuacha sigara kutalinda afya yako na wale wanaokuzunguka kwa ujumla.

8. Unalinda afya ya akili

Uchunguzi uliofanyika mwaka 2010 kwa watu wenye umri mkubwa ambao walikuwa wavutaji wa sigara, ulibaini kuwa walikabiliwa na matatizo ya akili kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wale wasiovuta sigara.

Kutokana na utafiti huu ni ukweli kuwa uvutaji wa sigara huathiri afya ya ubongo na hatimaye kupelekea matatizo ya akili.

9. Unalinda afya ya uzazi

Utafiti uliofanyika mnamo mwaka 2007 ulibaini kuwa uvutaji wa sigara una athari kubwa kwenye afya ya uzazi ya mwanaume na mwanamke pia.

Inaelezwa kuwa sigara huharibu mbegu za kiume, husababisha kutoka kwa mimba, huharibu mayai ya uzazi ya wanawake pamoja na kuathiri viungo vya uzazi kwa ujumla. Hivyo kuacha sigara ni kulinda afya yako ya uzazi.

10. Unaondoa harufu mbaya

Watu wanaovuta sigara wamekuwa wakiwakera watu wengi kutokana na harufu mbaya inayotokana na uvutaji wa sigara. Wengine wamekuwa wakitumia dawa mbalimbali ili kukabili harufu hiyo bila mafanikio.

Kwa hakika suluhisho la uhakika la kukabili harufu mbaya ya sigara ni kwa kuacha kuvuta sigara pekee na si vinginevyo.

Hitimisho

Kwa hakika kuna kila sababu ya kuacha uvutaji wa sigara leo. Ikiwa unataka kuacha sigara inakupasa kufanya maamuzi sahihi pamoja na kuweka mikakati stahiki ya kufanya hivyo. Unaweza pia kutafuta msaada kutoka kwa wataalamu wa tiba au washauri nasaha ili kuweza kutimiza lengo lako.

Je bado unatamani kuendelea kuvuta sigara? Ninakushauri uache kwa ajili ya manufaa ya afya yako sasa.

Soma pia: Mbinu 9 za Kuacha Tabia Mbaya

Je una maoni au maswali? Tafadhali tunadikie hapo chini. Unaweza kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

1.5 2 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x