Uongozi ni dhamana; tena ni nafasi ya kipekee inayopaswa kutumiwa vyema. Tuna viongozi wengi katika jamii yetu lakini siyo wote ni viongozi bora.
Baadhi hutumia uongozi kama silaha, chanzo cha kipato au hata kichaka cha kuficha maovu. Kwa hakika kila kiongozi anatakiwa kujitambua na kupata maarifa stahiki ya uongozi. Ikiwa unapenda kuongeza maarifa yako au unataka kufahamu zaidi kuhusu uongozi; basi karibu nikufahamishe nukuu 30 za uongozi.
“Kiongozi ni yule anayefahamu njia, anakwenda kwenye njia hiyo, na anaonyesha njia.”
“Pasipo na maono, hakuna tumaini.”
“Ubora wa kiongozi unadhihirishwa na viwango alivyojiwekea yeye mwenyewe.”
“Siogopi jeshi la simba linaloongozwa na kondoo; Ninaogopa jeshi la kondoo linaloongozwa na simba.”
“Usitafute kosa, bali tafuta suluhisho.”
“Ubunifu unatofautisha kati ya kiongozi na mfuasi.”
“Kujimudu wewe mwenyewe, tumia kichwa chako, kumudu wengine, tumia moyo wako.”
“Kiongozi mashuhuri siyo yule anayefanya vitu vikubwa sana. Bali ni yule anayewawezesha watu kufanya vitu vikubwa sana.”
“Usiwaambie watu jinsi ya kufanya vitu, bali waambie ni nini cha kufanya na waache wakushangaze kwa matokeo yake.”
“Uongozi ni sanaa ya kumfanya mtu mwingine afanye unachohitaji kifanyike kwa sababu mtu huyo anahitaji kukifanya.”
“Usimamizi ni kufanya kwa usahihi; uongozi ni kufanya vitu sahihi.”
“Kuwa mfano siyo kitu kikuu cha kuwahamasisha wengine; bali ni kitu pekee.”
“Siwezi kumwamini mtu asiyeweza kujitawala yeye mwenyewe atawale wengine.”
“Sanaa ya uongozi ni kusema hapana, sio ndiyo. Ni rahisi sana kusema ndiyo.”
“Uongozi ni tendo na siyo nafasi.”
“Kiongozi huwafikisha watu pale ambapo wasingefika wao wenyewe.”
“Kuwa aina ya kiongozi ambaye watu watamfuata kwa hiari, hatakama huna cheo au nafasi.”
“Mtu mashuhuri huvutia watu mashuhuri na anafahamu jinsi ya kuwashikamanisha pamoja.”
“Yeye ambaye hajawahi kujifunza kutii hawezi kuwa muamrishaji mzuri.”
“Uongozi ni ushawishi.”
“Ufunguo wa uongozi wenye mafanikio leo ni ushawishi, siyo mamlaka.”
“Viongozi hufikiri na kuzungumzia suluhisho. Wafuasi hufikiri na kuzungumzia matatizo.”
“Tunapotazama karne mpya, viongozi watakuwa wale wanaowawezesha wengine.”
“Elimu ni mama wa uongozi.”
“Viongozi bora hawatambuliki kwa kukosa madhaifu, bali kwa kuwa na nguvu dhahiri.”
“Uongozi na kujifunza ni muhimu kwa kila kimoja.”
“Unachofanya kina matokeo makubwa kuliko unachosema.”
“Uongozi ni kuufanya uwezo wa watu kuwa bora.”
“Uongozi ni ufunguo wa asilimia 99 ya jitihada zote za mafanikio.”
“Mtu anayetaka kuongoza bendi ya mziki ni lazima awageuzie mgongo watazamaji.”
Soma pia: Sifa 10 Zitakazokufanya Kuwa Kiongozi Bora
Je wewe ni kiongozi? Je umejifunza kitu kutokana na nukuu hizi za uongozi? Tafadhali andika maoni yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Blog hii ni nzuri sana tena ni ya kipekee, tangu nilivyoanza kusoma na kufuatilia masomo kwenye blogs sijaona blog nzuri kama hii. Asante nashukuru sana kwa masomo mazuri sana ambayo nilikuwa siyajui. Mungu akubariki ndugu yangu. Yes good.
Ninashukuru sana kwa maoni yako mazuri yenye kutia moyo; karibu sana tukufahamishe zaidi.
Nimeipenda sana kwakweli, mmejitahidi, na Mungu awabariki mfanye vizuri zaidi na watu wawatuambue zaidi kwani upendo wenu kwa jamii ni mkubwa na mnastahili pongezi kwakweli. keep it up.
Nashukuru sana kwa maoni yako mazuri yenye kutia moyo; Karibu sana Fahamuhili.com
Yes
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Mmetisha
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com