Nukuu (Quotes) 50 Zitakazokuhamasisha Maishani Mwako - Fahamu Hili
Friday, April 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Nukuu (Quotes) 50 Zitakazokuhamasisha Maishani Mwako

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Hamasa

Yale tunayoyawaza na kuyatafakari kwenye fikra zetu yana nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu. Ikiwa tunataka kufanikiwa basi ni lazima tufikiri na kutafakari juu ya kufanikiwa.

“Tunakuwa kile tunachofikiri”

Earl Nightingale

Vivyo hivyo ikiwa tunahitaji kuhamasika kufanya mambo mbalimbali maishani, ni lazima tusome, tusikilize, tutazame na hata tutafakari vitu vitakavyotuhamasisha.

Karibu nikufahamishe nukuu 50 (quotes) ambazo zitakuhamasisha katika maswala mbalimbali unayoyafanya maishani mwako.

 1. “Chochote ambacho akili ya binadamu inaweza kuumba na kufikiri, inaweza kukikamilisha pia.”

  Napoleon Hill
 2. “Njia ya kuanza ni kuacha kuzungumza na kuanza kutenda.”

  Walt Disney
 3. “Usiruhusu jana itawale sana leo.”

  Will Rogers
 4. “Kama unafanyia kazi kitu kinachokusisimua na unachokijali kweli, hauhitaji kusukumwa. Maono yako yatakusukuma.”

  Steve Jobs
 5. “Kufahamu haitoshi, ni lazima tuweke kwenye matendo, Kutamani haitoshi, ni lazima tufanye.”

  Johann Wolfgang
 6. “Tunatengeneza hofu tunapokaa bila kufanya kitu. Tunaishinda hofu kwa matendo.”

  Dr. Henry Link
 7. “Ikiwa unafikiri unaweza au huwezi, uko sahihi.”

  Henry Ford
 8. “Mtu mwenye kujiamini ndani yake, anapata kujiamini kwa wengine.”

  Hasidic Proverb
 9. “Fanya kile unachoweza kwa vyote ulivyonavyo, popote ulipo.”

  Theodore Roosevelt
 10. “Akili ni kila kitu. Unavyofikiri ndivyo unavyokuwa.”

  Buddha
 11. “Muda mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita. Lakini muda mwingine mzuri wa pili ni sasa.”

  Chinese Proverb
 12. “Muda wako ni mdogo, usiupoteze kuishi maisha ya mtu mwingine.”

  Steven Jobs
 13. “Kushinda siyo kila kitu, lakini kutaka kushinda ni kila kitu.”

  Vince Lombardi
 14. “Huwezi kuvuka bahari kama huna ujasiri wa kuacha kuona ufukwe.”

  Christopher Columbus
 15. “Kisasi kizuri ni mafanikio makubwa.”

  Frank Sinatra
 16. “Kuna njia moja tu ya kuepuka kukosolewa: usifanye kitu, usiseme kitu na usiwe chochote.”

  Aristotle
 17. “Anzia ulipo. Tumia kile ulichonacho. Fanya kile unachokiweza.”

  Arthur Ashe
 18. “Anguka mara saba simama mara ya nane.”

  Japanese Proverb
 19. “Mlango mmoja wa furaha ukifungwa, mwingine unafunguliwa, lakini mara nyingi tunautazama sana ule uliofungwa na kushindwa kuona ule uliofunguliwa kwa ajili yetu.”

  Helen Keller
 20. “Kila kitu kina uzuri wake, lakini siyo kila mtu anaweza kuuona.”

  Confucius
 21. “Changamoto zinafanya maisha yavutie na kuzishinda ni kufanya maisha kuwa na maana.”

  Joshua J. Marine
 22. “Kama unataka kujiinua mwenyewe juu, mwinue mwingine juu kwanza.”

  Booker T. Washington
 23. “Ili kufanikiwa, shauku yako ya mafanikio ni lazima iwe kubwa kuliko hofu yako ya kushindwa.”

  Bill Cosby
 24. “Kila siku ninajitahidi kufanya vizuri zaidi kuliko nilivyo fanya jana.”

  Reginald Mengi
 25. “Mtu ambaye hajawahi kufanya kosa hajawahi kujaribu kitu chochote.”

  Albert Einstein
 26. “Mtu anayesema hawezi kufanya hatakiwi kumwingilia mtu anayesema ninaweza kufanya.”

  Chinese Proverb
 27. “Haujachelewa kuwa ambaye ungeweza kuwa.”

  George Eliot
 28. “Unakuwa kile unachoamini.”

  Oprah Winfrey
 29. “Jenga ndoto zako wewe mwenyewe, la sivyo mtu mwingine atakuajiri kujenga zake.”

  Farrah Gray
 30. “Ota ndoto kubwa na dhubutu kushindwa”

  Norman Vaughan
 31. “Badili kufikiri kwako na utakuwa umebadili ulimwengu.”

  Norman Vincent Peale
 32. “Andika kitu chenye manufaa kusomwa au fanya kitu chenye manufaa kuandikwa.”

  Benjamin Franklin
 33. “Njia pekee ya kufanya kazi nzuri ni kupenda kile unachokifanya.”

  Steve Jobs
 34. “Ikiwa unaweza kuliota, unaweza kulifanikisha.”

  Zig Ziglar
 35. “Ndoto zetu zote zinaweza kutokea ikiwa tuna ujasiri wa kuzifuata.”

  Wale Disney
 36. “Usilie juu ya kile ambacho huna; tumia vizuri kile ulichonacho.”

  Reginald Mengi
 37. “Mambo mazuri huja kwa watu wanaosubiri, lakini mambo bora huja kwa wale wanaoondoka na kwenda kuayachukua.”

  Hajulikani
 38. “Fursa hazitatokea, unatakiwa kuziunda.”

  Chris Grosser
 39. “Usijaribu kuwa mtu wa mafanikio, bali jaribu kuwa mtu wa thamani.”

  Albert Einstein
 40. “Akili kubwa hujadili mawazo, akili ya wastani hujadili matukio, akili ndogo huzungumzia watu.”

  Eleanor Roosevelt
 41. “Ikiwa hauthamini muda wako, hata wengine hawatauthamini. Acha kupoteza muda na vipaji vyako sasa – anza kuvifanyia kazi”

  Kim Garst
 42. “Mtu mwenye mafanikio ni yule anayeweza kujenga msingi imara kwa kutumia matofali yaliyotupwa na wengine.”

  David Brinkley
 43. “Usiinue sauti yako, boresha hoja yako.”

  Hajulikani
 44. “Ninaamini kwamba ujasiri pekee mtu yeyote anaouhitaji ni ujasiri wa kufuata ndoto zako mwenyewe.”

  Orarah Winfrey
 45. “Fursa zina aibu, zinakusubiri uzikimbilie.”

  Reginald Mengi
 46. “Ubunifu unatofautisha kati ya kiongozi na mfuasi.”

  Steve Jobs
 47. “Hofu ni mojawapo ya adui mkubwa kwa mafanikio.”

  Reginald Mengi
 48. “Wengi wetu hatuishi ndoto zetu kwa sababu tunaishi hofu zetu.”

  Less Brown
 49. “Hatua ya mwanzo ya mafanikio yoyote ni matamanio.”

  Napoleon Hill
 50. “Baadaye inamilikiwa na wale wote wanaoamini kwenye uzuri wa ndoto zao.”

  Eleanor Roosevelt

Naamini umehamasika na kufurahia nukuu hizi za hamasa. Ni wazi kuwa kila kitu kinaanza kwenye fikra zetu – tunavyowaza ndivyo tunavyokuwa.

Je una swali, maoni au nukuu nyingine ambayo ungependa tuiweke hapa? Karibu utushirikishe kwa kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook pamoja na kuwashirikisha wengine makala hii.

4.3 10 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

21 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Abeid shehoza
Abeid shehoza
3 years ago

Nimaoni yanayojengakutazauhamasishowamaisha

Peter Michael
Peter Michael
3 years ago

Mambo mbona kimya Sana

Eliud Timothy
Eliud Timothy
3 years ago

Nimezipenda sana hizi nukuu! Zinahimiza na kutia moyo.
Nimezidi kujifunza siku kwa siku na kuwafunza wengine

Salehegae
Salehegae
3 years ago

Hello, samahani Mimi kwa majina naitwa Salehe gae Salum Mwangalamo. Ni muandishi mchanga wa nukuu, naombeni msaada wenu ili nitimize ndoto zangu za kuwa muandishi wa nukuu zangu mwenyewe..

rashiku
rashiku
3 years ago

good

said suleiman said
said suleiman said
2 years ago

naomba kuunganishwa kwenye group la whtsapp kamalipo

Renatus Kaizirege Remigius
Renatus Kaizirege Remigius
2 years ago

Mnyama unayempenda zaidi huzibeba sifa zako.

Saimon joseph
Saimon joseph
2 years ago

Nimepata funzo kwenye hizi nukuu nimejikuta navaa ujasiri mkubwa sana naimani ndoto zangu bado zinawezekana

Makaranga s makaranga
Makaranga s makaranga
1 year ago

Amizing quote
Mungu akubariki kwa kutukumbusha
Wanadamu ni wepesi Sana wa kusahau, ni kutokana na changamoto za maisha ya mazoea.

Mary
Mary
1 year ago

Nukuu nzuri Asante sana nazidi kujifunza

Nickson M Hamisi
Nickson M Hamisi
1 year ago

Shida ya macho ilipata kwa sababu ya kusoma makasha usiku kucha kwa kutumia koroboi. Safari ya ufanisi si rahisi, ina miba mirefu njia yake. Inahitaji uvumilivu na kujitolea.

21
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x