Mambo 5 ya Kufahamu Kabla ya Kulenga Kupata Pesa kupita Kazi za Kwenye Mtandao - Fahamu Hili
Friday, May 24Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 5 ya Kufahamu Kabla ya Kulenga Kupata Pesa kupita Kazi za Kwenye Mtandao

Washirikishe Wengine Makala Hii:

kazi za kwenye mtandao

Kila mtu anahitaji kupata pesa ili kumudu mahitaji yake ya kila siku kama vile kununua chakula, nguo, kulipia matibabu, usafiri, ujenzi wa nyumba, n.k.

Swali hapa ni kwa njia gani zitapatikana hizo pesa; kwani mara nyingi watu wanajikuta mishahara au kipato chao cha awali hakitoshi. Hivyo basi watu wanatafuta njia mbalimbali za kuwawezesha kuongeza kipato chao.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamepelekea kukua kwa ajira na biashara katika mtandao; takwimu zinaonyesha kuwa kuna watu wengi wanaoomba na kufanya kazi katika matandao.

Fuatana nami katika makala hii ili ufahamu mambo matano ya kuzingatia kabla ya kulenga kupata fedha kupitia kazi za kwenye mtandao.

1. Tovuti za matapeli

Hivi leo ni rahisi kuona tovuti zinazojinadi kuwawezesha watu kupa kipato kwa urahisi ndani ya muda mfupi. Swali ni je ni kwa namna gani tovuti hizi zinalenga kweli kuwawezesha watu kupata fedha?

Kulingana na scamwatch.gov.com wanadai kuwa zaidi ya dola 2,633,797 zimepotea kwenye kazi na uwekezaji wa kwenye mtandao. Ikizingatiwa watu hutapeliwa kwa kuwa wengi wana uelewa mdogo wa maswala haya, pia wengi wana uhitaji mkubwa wa pesa, hivyo wanachotazama ni pesa tu.

Nakushauri kabla ya kuomba kazi katika tovuti yoyote, kwanza chunguza uhalali na uhalisia wake; unaweza kufahamu hili kwa kupitia maoni ya watumiaji wengine (rivews) yanayohusu tovuti husika.

Pia epuka kutoa taarifa zako muhimu kama vile kadi ya benki, akaunti za benki, pasi ya kusafiria, namba za siri n.k. bila uchunguzi wa kutosha juu ya tovuti husika kwani unaweza kuibiwa fedha zako.

2. Mikataba na gharama zilizofichwa

Imekuwa ni jambo la kawaida kuona kazi inatangazwa kuwa ina ujira wa dola 500, lakini mwishoni ukapata dola 200 au 300 pekee. Watangazaji wengi wa akazi za kwenye mtandao huficha baadhi ya mikataba au makato ili kukuvutia kufanya kazi.

Nakumbuka rafiki yangu aliwahi kufanya kazi ya dola 700 lakini alilipwa dola 500 pekee. Hivyo basi, nakusisitizia kuchukua tahadhari mapema kabla haujatumbukia kwenye mikono ya matapeli.

3. Ni kazi kama kazi nyingine

Watu wamekuwa wakifikiri kwa kuwa ni kazi ya kwenye mtandao, basi ni rahisi kupata pesa za mteremko. Hakika ukifanya kazi hovyo hovyo kweye mtandao hutolipwa chochote au utalipwa kidogo sana.

Hivyo basi, kabla ya kuomba kazi yoyote hakikisha una maarifa na ujuzi wa kutosha wa kuifanya hiyo kazi vyema. Jitahidi kujenga jina na sifa njema ili upate kazi zaidi.

Mambo ya kuzingatia katika swala hili:

  • Hakikisha umeielewa vyema kazi husika
  • Hakikisha una vifaa vinavyohitajika
  • Hakikisha una muda wa kutosha wa kufanya kazi husika
  • Usitazame malipo bali tazama ubora wa kazi
  • Hakikisha unauwezo mzuri wa lugha ya kuwasiliana na mwajiri wako (Kiingereza hupendelewa zaidi)

Soma pia: Mbinu 10 za Uhakika za Kufahamu Kiingereza/English kwa Muda Mfupi.

4. Ushindani ni mkubwa

Kutokana changamoto mbalimbali za kiuchumi duniani hasa ukosefu wa ajira, watu wengi wanatafuta kazi kwenye mtandao.

Kwa mujibu wa Freelancers Union na Upwork wanadai kuwa takriban watu milioni 54 wanatafuta kazi kwenye mtandao ndani ya Amerka pekee. Je unaweza kumudu ushindani huu?

Mambo ya kuzingatia hapa:

  • Hakikisha una ujuzi wa kutosha kushindana na ushindani huu.
  • Usiombe kazi rahisi kuomba, kwani zinaombwa na watu wengi sana.
  • Upatapo kazi fanya kwa ubora wa hali ya juu ili ujenge jina.

5. Hakuna maslahi ya mfanyakazi

Makampuni mengi yamekuwa yakiweka kazi zao kwenye mtandao ili kuokoa gharama za wafanyakazi kama vile malipo ya uzeeni, matibabu, malipo ya uhamisho n.k.

Hivyo uombapo kazi katika mtandao usitegemee kupata kitu kingine zaidi ya malipo ya kazi husika. Nakushauri isiache kazi yako ya awali bali fanya kazi hizi za mtandaoni kama kitu cha kukuongezea kipato chako.

Neno la mwisho

Lengo langu hapa halikuwa kukukatisha tamaa au kukuambia kuwa kazi za kwenye mtandao ni mbaya, bali nililenga kukusaidia uweze kufanya maamuzi sahihi. Nakushauri kabla ya kufanya au kutafuta kazi kwenye mtandao zaingatia haya:

  • Usalama wako
  • Uhalali wa mwajiri na kazi husika

Ukizingatia haya utafurahia kazi za kwenye mtandao na zitakupa tija kubwa.

Soma pia: Tovuti 15 za Kufanya Kazi Kwenye Mtandao.

Je una swali au maoni yoyote? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe au kwa kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3 5 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x