
Tovuti 15 za Kufanya Kazi Kwenye Mtandao
Mara nyingi milango ya matumizi ya fedha ni mingi kuliko milango ya mapato. Hivyo ni vyema kufikiri namna ya kuongeza milango mingi zaidi ya kipato. Inawezekana wewe ni mwajiriwa, mjasiriamali, mwanafunzi au hujaajiriwa bado; ni vyema ukafahamu kuwa zipo kazi zinazopatikana kwenye mtandao ambazo zinaweza kukuzalishia kipato kizuri. Hakuna sababu ya kukaa na maarifa au ujuzi ulionao ambao ungeweza kuutoa na ukajipatia kipato. Kufanya kazi kwa njia ya mtandao ni rahisi zaidi na kunakupa uhuru mkubwa wa mazingira ya kufanyia kazi. Fahamu kuwa unaweza kupata kazi nzuri zenye kipato kizuri katika tovuti 15 nilizoziorodhesha hapa. Soma Pia: Mambo 5 ya Kufahamu Kabla ya Kulenga Kupata Pesa kupita Kazi za Kwenye Mtandao.
1. Upwork
Upwork ni tovuti ambayo awali ilifahamika kama Odesk, k...