Tovuti 15 za Kufanya Kazi Kwenye Mtandao - Fahamu Hili
Friday, April 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tovuti 15 za Kufanya Kazi Kwenye Mtandao

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Mara nyingi milango ya matumizi ya fedha ni mingi kuliko milango ya mapato. Hivyo ni vyema kufikiri namna ya kuongeza milango mingi zaidi ya kipato. Inawezekana wewe ni mwajiriwa, mjasiriamali, mwanafunzi au hujaajiriwa bado; ni vyema ukafahamu kuwa zipo kazi zinazopatikana kwenye mtandao ambazo zinaweza kukuzalishia kipato kizuri.

Hakuna sababu ya kukaa na maarifa au ujuzi ulionao ambao ungeweza kuutoa na ukajipatia kipato. Kufanya kazi kwa njia ya mtandao ni rahisi zaidi na kunakupa uhuru mkubwa wa mazingira ya kufanyia kazi. Fahamu kuwa unaweza kupata kazi nzuri zenye kipato kizuri katika tovuti 15 nilizoziorodhesha hapa.

Soma Pia: Mambo 5 ya Kufahamu Kabla ya Kulenga Kupata Pesa kupita Kazi za Kwenye Mtandao.

1. Upwork

Upwork ni tovuti ambayo awali ilifahamika kama Odesk, kwa sasa ina takriban zaidi ya waajiri milioni 1.5. Ndani ya upwork unaweza kufanya kazi takribani zote; za muda mfupi, za muda mrefu, za saa n.k. Inategemea tu ujuzi wako ulionao ili kuweza kumudu na kupata kazi ndani ya upwork.

Tovuti: https://upwork.com

2.Toptal

Toptal ni tofauti na tovuti nyingine za kazi za kwenye mtandao kwani hii huwasaili wale wanaotafuta kazi ili kuwapata wale walio bora zaidi. Kufanikiwa katika usaili wa Toptal kutakufungulia fursa ya kupata kazi kwenye makampuni kama vile (JPMorgan, Zendesk, Airbnb, n.k.)

Tovuti: https://toptal.com/

3. Freelancer

Tofauti na tovuti nyingine Freelancer ina mamilioni ya kazi. Freelancer inaruhusu kushindana na wafanyakazi wengine (freelancers) ili kudhibitisha uwezo wako. Kwa kufanya hivi utaweza kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata kazi zenye tija zaidi.

Tovuti: https://freelancer.com/

4. Fiverr

Fiverr nayo ni tofauti kidogo na tovuti nyingine kwani hapa yule anayefanya kazi ndiye huchapisha kazi anayofanya pamoja na bei. Hapa kazi huwekwa kwa mfumo unaoitwa Gigs unaonzia kwa malipo ya dola 5. Mwajiri humfikia mfanya kazi kwa kutafuta jambo linaloendana na Gigs zake. Hapa kuna watu wanaofanya kazi mbalimbali zaidi ukilinganisha na tovuti nyingine.

Tovuti: https://www.fiverr.com/

5. Craigslist

Watu wengi wanaifahamu Craigslist kama tovuti ya kuuza na kununua vitu, lakini pia kwa kupitia tovuti hii unaweza kupata kazi nzuri. Unaweza kutafuta kazi katika miji mabalimbali na kuzifanya kwa njia ya mtandao.

Tovuti: https://craigslist.org/

6. Guru

Guru ni tovuti inayokuwezesha kuonyesha uwezo wako wa awali ambao pia utakuwezesha kupata kazi. Kama una kipaji na uwezo basi hii ni nafasi yako.

Tovuti: https://guru.com/

7. 99designs

Ni tovuti kwa ajili ya wabunifu; watu hushindana na kupata mrejesho kutokana na uchaguzi wa mteja. Kama wewe ni mbunifu na una kipaji, unaweza kuomba kazi katika tovuti hii.

Tovuti: https://www.99designs.com/

8. Peopleperhour

Peopleperhour ni tovuti kwa ajili ya wasanifu wa kimtandao; kama wewe unajua kutengeneza tovuti, unajua Search Engine Optimization (SEO), n.k. Basi tovuti hii ni kwa ajili yako.

Tovuti: https://peopleperhour.com/

9. Freelance Writing Gigs

Kama wewe ni mwandishi, bloga, mhariri au mchapishaji basi tovuti hii inakufaa. Tovuti hii inawafaa wale wote wanaojihusisha na shughuli za uandishi.

Tovuti: http://freelancewritinggigs.com/

10. Demand Media

Demand Media ni tovuti inayowafaa wale wanaotafuta kazi za kibunifu; ubunifu wa picha, video n.k. Unaweza kutengeneza kitu cha kipekee na kukiweka kwa ajili ya kujitangaza.

Tovuti: http://demandmedia.com/

11. College Recruiter

Kama lilivyo jina lenyewe College Recruiter ni tovuti hasa kwa ajili ya wanafunzi au wale waliohitimu hivi karibuni. Tovuti hii imekuwa ni chanzo kikubwa cha kazi za muda; pia ni mahali pa kuanzia kujenga uzoefu wako.

Tovuti: https://www.collegerecruiter.com/

12. GetACoder

GetACoder ni moja kati ya tovuti zinazotoa kazi za kwenye mtandao zikiwemo za ubunifu na usanifu tovuti pamoja na uandishi. Ni mahali pia pakupata kazi ndogo ndogo.

Tovuti: http://getacoder.com/

13. iFreelance

iFreelance tofauti na tovuti nyingine hukuwezesha kupata asilimia karibu 100 ya mapato yako. Hapa unaweza kupata kazi mbalimbali kama za uandishi na ubunifu.

Tovuti: https://www.ifreelance.com/

14. Project4hire

Project4hire ni tovuti inayokuwezesha kuperuzi miradi/kazi mbalimbali na kubainisha inayokufaa kwa urahisi zaidi.

Tovuti: http://project4hire.com/

15. SimplyHired

SimplyHired ina sifa nyingi ambazo zinashabihiana na tovuti zilizotajwa hapo awali. Unaweza pia kutumia ujuzi na uwezo wako kuomba na kufanya kazi hapa.

Tovuti: http://simplyhired.com/

Ni dhahiri kuwa sasa umefahamu tovuti ambazo zinaweza kukuzalishia kipato kutokana na maarifa uliyo nayo. Nikukumbushe kuwa pamoja na kuwepo kwa tovuti hizi ni lazima ufahamu kuwa kazi hizi ni kazi kama kazi nyingine. Utahitaji maarifa na uwezo wa kufanya kazi husika ili uweze kulipwa na kutambulika. Pia kumbuka kuwa makini na kazi zinazowekwa na matapeli.

Je una swali au maoni? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

2 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
hudson odai
hudson odai
5 years ago

naomba kazi ya mtandao plz

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x