Je unatafuta njia ya kujipatia pesa kwenye mtandao ambayo siyo ya utapeli? Blog ni njia moja wapo unayoweza kuitumia kujipatia fedha huku ukifanya kile ukipendacho. Katika makala hii nitakushirikisha njia 14 unazoweza kuzitumia kupata pesa kwa kutumia blog yako.
Kumbuka! Hizi si njia za kupata pesa za mteremko haraka haraka kwa usiku mmoja. Kamwe usidanganywe na matangazo ya kuwa utafanywa kuwa tajiri mkubwa siku moja. Mambo hayaendi hivyo.
Awali ya yote utahitaji kuwa na blog yako; pia utahitajika kuwekeza rasilimali ya muda au pesa kiasi fulani ili kuweza kuona matokeo kutokana na blog yako.
1. Kuwa wakala
Unaweza kupata pesa kwenye blog yako kwa njia ya kuwa wakala wa wauzaji wa bidhaa au huduma mbalimbali. Mara mtu anunuapo kitu kwa kukifikia kupitia blog yako basi utapata gawio.
Unaweza kujiunga na huduma hizi ili kuwa wakala:
Baada ya kuchagua bidhaa ya kuitangaza unaweza kutumia ThirstyAffiliates kutawala matangazo hayo.
2. Jiunge na Google Adsense
Kama una watembeleaji wengi kwenye blog yako kuanzia 1,000 au zaidi kwa siku, unaweza kujiunga na huduma hii na ukapata pesa kutokana na matangazo yatakayowekwa na Google kwenye blog yako.
Aina za utangazaji wa Google Adsense:
CPC – Cost Per Click ni matangazo ambayo utalipwa kadri watumiaji wa blog yako wanavyobofya au kuclick tangazo husika. Kiwango cha malipo kwa click hutegemea kiwango kilichowekwa na mtangazaji.
CPM – Cost Per Thousand impressions ni matangazo ambayo utalipwa kutokana na tangazo kuonwa mara 1,000.
Soma pia: Mambo 9 ya Kuzingatia Wakati Wa Kuchagua Kampuni ya Matangazo Kwenye Blog
3. Njia ya kuweka matangazo moja kwa moja
Unaweza kukubaliana na kampuni husika moja kwa moja kuweka tangazo lao kwenye nafasi fulani ya blog yako. Kwa njia hii unaweza kupata pesa zaidi kuliko kutumia huduma nyingine ambazo ndizo hukubaliana na makampuni husika au mtangazaji.
4. Andika posti iliyodhaminiwa
Hii ni post inayoandikwa kwa lengo la kufafanua au kutangaza huduma au bidhaa fulani. Kampuni husika itakulipa kwa kuandika post inayoelezea na kutangaza bidhaa au huduma yao.
5. Uza blog
Kuuza blog? Ndiyo, kuuza blog kunaweza kukupatia kipato kizuri kabisa. Kama unajua kusanifu na kutengeneza blog, basi unafahamu kitu cha ziada. Kuna watu wengi wanahitaji kununua blog zilizotengenezwa tayari. Unaweza kutafuta anwani nzuri (domain) na kuitengenezea blog kisha ukaiuza kupitia tovuti kama vile Flippa na kujipatia pesa.
6. Tengeneza maudhui ya wanachama
Unaweza ukatengeneza maudhui kwenye blog yako ambayo yanaweza kufikiwa na wanachama waliojisajili tu. Unaweza kupata pesa kwa njia ya kuwatoza ada ya usajili au uwanachama wale wote wanaohitaji kujisajili kwenye blog yako. Kwa njia hii utajipatia kipato moja kwa moja kutokana na wanachama watakaojisajili ili kusoma maudhui hayo.
7. Uza vitabu pepe
Kama una maarifa fulani unaweza kuyaweka kwenye mfumo wa vitabu pepe (e-books) na kuuza vitabu hivyo ili kujipatia pesa. Unaweza ukatengeneza kitabu chako katika mfumo wa PDF na kuwatoza watu kiasi fulani cha pesa ili kuweza kukipakua.
Soma pia: Mbinu 7 za Uandishi Bora wa Vitabu
8. Uza kozi za kwenye mtandao
Kama ilivyo kwenye swala la vitabu, unaweza pia ukandaa kozi za kuwafundisha watu mambo mbalimbali unayoyafahamu. Andaa kozi vizuri na kwa ubora, zitangaze kwenye blog yako na watu wanaweza kujiunga kwa kulipa ada fulani ambayo itakupatia pesa.
9. Tafuta kazi kwa kuuza ujuzi wako
Kama una ujuzi wa kufanya kazi au jambo fulani unaweza kutumia blog yako kujitangaza na ukajipatia kipato cha kutosha. Watu wanapotembelea blog yako wanaweza kuvutiwa na ujuzi wako hivyo wakakuajiri ili uwafanyie kazi fulani.
10. Kuwa mshauri au kocha
Kama unauwezo wa kuwashauri watu au kuwahamasisha juu ya maswala mbalimbali ya maisha, unaweza kutumia blog yako kufikia wateja wako. Unaweza ukawahudumia kupitia mtandao au ukawaalika moja kwa moja ofisini kwako. Maswala haya yanaweza kuwa tiba, mahusiano, elimu, uchumi, malengo, maono n.k. Unaweza kuwatoza gharama fulani kutokana na huduma husika na ukajipatia pesa. Mfano mzuri wa blog ya namna hii ni blog ya fadhilipaulo.com
11. Anza duka la kwenye mtandao
Kama unatumia WordPress kwenye blog yako unaweza kutumia WooCommerce plugin kuanzisha duka la kwenye mtandao na ukauza bidhaa mbalimbali. Kwa njia hii unaweza kuuza bidhaa zako au za watu wengine na ukajipatia kiasi kizuri cha pesa.
Soma pia: Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao
12. Uza mavazi yenye chapa yako
Kama unachapa (brand) maarufu ama ya blog au kampuni yako unaweza kuitumia kuuza mavazi na ukajipatia pesa. Unaweza kuuza mavazi yenye chapa yako kama vile tisheti, kofia, mikanda, bangili, mikoba, viatu n.k kupitia blog yako.
13. Uza kazi ya usanifu mtandao
Kama unajua kutengeneza plugins za wordpress, extension za Joomla, violezo (themes/templates) n.k unaweza kuvizua kupitia blog yako na ukajipatia kiwango kizuri cha pesa.
14. Pokea msaada
Hii ni njia ambayo si maarufu sana lakini inaweza kukuwezesha kupata pesa. Umewahi kufikiri tovuti kama wikipedia inajiendeshaje? Inajiendesha kwa kutegemea michango ya misaada ya wasomaji wake. Kama unatoa maarifa au huduma fulani nzuri bila malipo kwanini usiombe msada kwa mtu anayependa kufanya hivyo? Unaweza ukapata kiwango kizuri cha fedha kupitia njia hii.
Hitimisho
Naamini umeweza kufunguka macho na kuona fursa ambazo hukuwa umeziona ua kuzielewa vyema mwanzoni. Ni vyema ukafahamu kuwa hakuna njia ya mkato kupata pesa. Ni vyema ukajitahidi kufanya bidii na kuwekeza muda au fedha kiasi fulani kwenye blog yako ili uweze kujipatia kipato kizuri.
Je una swali au unafahamu njia nyingine bora zaidi ya hizi zilizowekwa hapa? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe na wengine.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Nimependa sana makala yako mkuu.. Great work.
Asante sana Mkuu; karibu sana huku pia; nimefurahi sana kukutana na wewe huku pia.
Nimefurahi kukutana na makala yako mkuu, umenifungua macho sana naweza pata contacts zako my email mlayfadhil@gmail.com
Karibu: korneliomaanga[at]gmail.com. Asante sana; karibu sana Fahamuhili.com
Safi sana kwa makala yako
Mimi nina swali hivi hawa wanaoweka music kwenye blog zao wanapataje pesa pia kuna watu wanajibu maswali mbalimbali ya past papers wanapataje hela
Ningeweza kuona mfano wa hizo blogs ningeweza kukubainishia wanapataje pesa. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Nafurahi kuijua blog hii… Najuta kwakuchelewa,,, nimepata mwanga kwani nami ni mdau wa blogs
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Naamin katika biashara nyingi tunapokwama ni pamoja na kuwa na blog.
Nashukuru kwa kunifungua akili pia hongera kwa kutengeneza blog
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Asante Sana natak nifungue bloger natakiwa kuwa na sh ngap ya kuanzia
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Mawasiliano:
Email: fahamuhili[at]gmail.com
Simu: 0758 444 771
Ni mzuri sana
Asante sana kwa maoni yako ya thamani kwetu; karibu sana Fahamuhili.com
Yes
Asante sana kwa maoni yako; karibu sana Fahamuhili.com
nawezaje kupata blog yangu?
Wasiliana nasi kupitia fahamuhili@gmail.com. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Nimeelewa ila naomba kukuuliza nifanyeje ili nami niweze kufungua blog nimejaribu kila mara lakini na.kwma nitumie njia ili nami niweze kuwa na blog yangu binafsi
Karibu kwa ushauri fahamuhili@gmail.com. Asante
Join
Asante sana. Karibu sana Fahamuhili.com
Nmeipenda sana ni nzuri
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com