Mambo 7 ya Kuzingatia ili Kulinda Tovuti Yako Dhidi ya Wadukuzi - Fahamu Hili
Friday, June 2Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 7 ya Kuzingatia ili Kulinda Tovuti Yako Dhidi ya Wadukuzi

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Usalama wa tovuti

Kutengeneza tovuti ni jambo moja na kuilinda ni jambo la pili. Kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia, kumepelekea kukua na kushamiri kwa uhalifu kwa njia ya mtandao.

Visa kadha wa kadha vimeripotiwa vikieleza juu ya udukuzi uliofanyika kwenye makampuni mbalimbali na kusababisha hasara kubwa. Kwa mfano kampuni ya Sony ilidukuliwa mnamo mwaka 2014 na kupata hasara ya takriban dola milioni 15 za Marekani.

Ni muhimu kulinda tovuti au blog yako dhidi ya wadukuzi ili kuepusha hasara na uharibifu unaoweza kutokea. Ikiwa unataka kulinda tovuti yako, basi fahamu mambo 7 ya kufanya ili kulinda tovuti yako dhidi ya wadukuzi.

1. Hakikisha unazingatia usasishaji (updating)

Ikiwa unatumia programu yoyote katika website yako, hakikisha unaisasisha kwa wakati.

Programu kama vile WordPress, Joomla, Durpal pamoja na vipanuzi vyake (extensions na plugins) zinahitaji kusasishwa mara kwa mara ili kupokea maboresho na kuondoa madhaifu ya kiusalama yaliyobainika.

Hivyo basi, kufanya usasishaji kwa wakati sahihi kutakuwezesha  kuziba mianya ambayo inaweza kutumiwa na wadukuzi.

2. Tawala viwango vya ruhusa

Hakikisha watu unaowaruhusu kuingia kwenye tovuti yako umewatawala vyema. Hakikisha hautoi ruhusa kubwa sana au ya kipekee kwa mtu ambaye siyo sahihi.

Kwa mfano hakuna haja ya kumfanya kila mtu kuwa msimamizi mkuu (adimin); kwani mtu huyo anaweza kutoa au kupoteza taarifa zake za siri na zikatumiwa kudukua tovuti yako.

3. Tumia web host bora

Siyo kila web host ni salama dhidi ya wadukuzi. Web host nyingi hasa zile za bei rahisi hutumia mifumo duni ya usalama, hivyo ni rahisi kudukuliwa.

Ni muhimu kuhakikisha unachagua web host bora na salama ili kuepusha tovuti yako kudukuliwa.

Soma pia: Mambo 9 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Web Host

4. Tumia SSL

SSL ni teknolojia ya kiusalama inayohusika na kulinda mawasiliano na taarifa za watumiaji wa mtandao. Taarifa zinazotumwa kwenye tovuti yenye SSL hufichwa na haziwezi kuonwa na wadukuzi.

Hivyo ili kulinda taarifa muhimu kama vile nywila pamoja na taarifa za miamala ya fedha, ni muhimu kutumia SSL kwenye tovuti yako.

Kila web host bora inatakiwa kuwa na huduma ya SSL, kuna SSL za kulipia au ya bure.

5. Backup

Kuweka backup kutakuwezesha kuwa na nakala ya tovuti au blog yako mara ipatapo shida. Web host bora hutoa huduma ya backup moja kwa moja, hivyo upatapo shida watakusaidia kurejesha tovuti yako katika hali ya awali.

Hata hivyo unaweza kuweka backup wewe mwenyewe na ukaihifadhi mahali salama ili uitumie mara tovuti yako itakapopata shida.

6. Tengeneza fomu salama

Fomu za kwenye mtandao hutumika kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa mtumiaji; lakini pia ni mlango wa wadukuzi kuingia kwenye tovuti yako.

Hakikisha huruhusu kupakia mafaili (file uploading) hovyo au kuruhusu fomu kujijaza (form autofill). Kwa kutofanya hivi utatoa mwanya wa wadukuzi kuingilia tovuti yako.

Soma pia: Makosa 25 ya Kuepuka Unapotengeneza Tovuti (website) au Blog

7. Tumia mbinu na zana za usalama

Kuna mbinu, hatua pamoja na zana mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa kulinda tovuti yako dhidi ya wadukuzi.

Kwa mfano kama unatumia wordpress unaweza kuzuia idadi ya kujaribu kuingia (login attempt), ukaficha anwani ya kuingia kwenye ukurasa wa msimamizi mkuu (admin area), au kuweka plugin ya usalama kama vile Wordfence.

Kwa kuchukua tahadhari hizi utaweza kulinda tovuti yako dhidi ya hatari mbalimbali za kiusalama.

Hitimisho

Ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya madhara hayajatokea; tovuti yako ikidukuliwa inaweza kukusababishia hasara kubwa. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia mambo yaliyoelezwa hapa ili kulinda tovuti yako dhidi ya wadukuzi.

Je una swali au maoni yoyote? Je wewe huwa unalindaje tovuti yako? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini kisha usisahau kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mambo mengi zaidi.

5 1 vote
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x