Sababu 6 za Kwanini Hutakiwi kununua Followers na Likes - Fahamu Hili
Thursday, March 28Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Sababu 6 za Kwanini Hutakiwi kununua Followers na Likes

Washirikishe Wengine Makala Hii:

fb

Nitatumia maneno haya kwenye makala hii:

Followers – Wafuatiliaji

Likes – Penda au Poa

Post – Chapisho

Comment – Maoni

Kumbuka! Nitatumia pia ukurasa wetu wa Facebook kwa mifano ili uelewe kwa uhalisia zaidi.

Inawezekana umeanzisha ukurasa wa Facebook au Twitter, na unashauku kubwa ya kuuendeleza. Lakini tatizo ni kuwa unauona ni dhaifu kutokana na kukosa likes au followers.

Mara moja wazo linalokuja kwenye akili yako ni kutafuta njia za kuongeza likes na followers, ama kwa kununua au kwa njia nyingine.

Unapofikiri hivyo jiulize maswali haya:

  • Maana ya likes na followers kwenye ukurasa wangu ni nini?
  • Je lengo langu ni nini?
  • Je likes na followers vitanisaidia kufikia lengo?
  • Je followers au likes za kununuliwa zinatokana na nini?
  • Je kurasa au watu wengine waliofanikiwa huwa wananunua likes na followers?

Ukijiuliza maswali haya, utaweza kufikiri vyema kabla ya kununua au kutafuta njia ya kuongeza likes na followers.

Hivyo basi, kabla hujachukua maamuzi ya kununua likes au followers, karibu nikufahamishe madhara 6 yatokanayo na kununua likes au followers.

1. Unapunguza ushiriki (engagement)

Mara nyingi likes za kununua zinakuwa siyo za watu halisi. Unaweza kuona ukurasa una likes 600,000 lakini posts zina like na comment moja au mbili.

gn
Ukurasa wenye likes na followers wengi bandia.

Huu ni ukurasa wenye likes na followers zaidi ya 600,000 lakini post zake zina comments na likes kati ya 1 hadi 10.

fahamuhili
Ukurasa wetu wenye likes na followers wachache halisi.

Hii ni post kutoka kwenye ukurasa wetu wa Facebook ambao makala ilipokuwa inaandikwa ulikuwa na likes na followers halisi 200 tu, lakini ona ushiriki wake ulivyo mzuri kuliko hata ule wenye likes na followers 600,000.

Je unapenda kuwa na namba kubwa ya followers ambao hawalike wala hawatoi maoni yoyote kwenye ukurasa wako? Kwa hakika likes au followers wa kununua wanakudidimiza zaidi kuliko kukusaidia.

Ni bora kuwa na likes 100 halisi ambazo zinaushiriki mzuri kuliko 600,000+ ambazo ni bandia.

2. Hupunguza kiwango cha kuaminika

Hebu fikiri watu wakifahamu kuwa unajifanya una likes nyingi au followers wengi kumbe ni bandia.

Ni wazi kuwa wataona hata kile unachokifanya siyo cha kweli. Kumbuka kuwa na likes nyingi siyo hoja; bali likes hizo au followers hao wanaushiriki kwa kiwango gani na wanakuwezeshaje kukamilisha lengo.

3. Hupoteza pesa

Maswala ya kununua likes na followers ni maswala yaliyobuniwa na watu kupata hela. Hii ni kutokana na watu wanaouza likes kutumia mbinu bandia za kuongeza likes na followers ambazo hazitarejesha fedha zako.

4. Ni ukiukwaji wa sera za mitandao husika

Mitandao takriban yote imepiga marufuku michakato mingi ya kuongeza followers au likes.

Hivyo kufanya haya kunaweza kukusababishia kufungiwa ukurasa au akaunti zako ikiwa utabainika.

5. Huharibu takwimu zako muhimu

Katika maswala ya kutathimini ukuaji wa wasomaji au walengwa, takwimu sahihi ni muhimu sana.

Unaponunua likes au followers utashindwa kutathimini kwamba ukurasa au blog yako imekua kwa kiasi gani kwa sababu ya kuwa na takwimu bandia.

6. Machapisho yako hayatawafikia walengwa

Watafiti wa mambo wanaeleza kuwa asilimia 20 hadi 30 ya followers wako ndiyo huona posts zako, tena kama zina ubora wa hali ya juu sana; la sivyo ni asilimia 10 pekee ndiyo wataziona.

Hivyo kuwa na followers bandia kutasababisha asilimia hii 10 iishie kwenye wale bandia. Inamaanisha kuwa wale halisi hawataweza kuona posts zako.

Kufika
Post kufikia walengwa pamoja na ushiriki katika ukurasa wetu.

Wakati makala hii inaandikwa, ukurasa wetu ulikuwa na likes na followers 200, lakini unaona post zetu zinafika kwa watu wengi zaidi vyema (Post reach 1,877). Ushiriki nao umeongezeka kwa asilimia 30.

Website Clicks ni 0 kwa sababu hizi huhesabiwa pale mtu anapofungua ukurasa mkuu wa tovuti kwa kupitia Facebook na si kurasa nyingine zatovuti. Kiuhalisia watu wanaofungua ukurasa mkuu kupitia Facebook ni nadra sana kuwapata.

click

Neno la mwisho pamoja na ushauri

Mara nyingi watu wanaotafuta kununua followers au likes ni wale wasiokuwa na lengo au kufahamu madhara ya kufanya hivyo.

Kumbuka katika ulimwengu huu, namba kubwa ya followers au likes ambayo haiwi wateja au wasomaji wako wa kudumu, haina maana yoyote.

Kwa mfano tovuti ya https://scottiestech.info, ina wasomaji wengi hadi kukubaliwa na Google kuweka matangazo yake lakini ukurasa wake wa Facebook una wanachama 125 tu hadi wakati makala hii inaandikwa.

sco
Tovuti ya Scottiestech.info

Ni bora kuwa na  likes au followers 100 bora ambao wanashiriki kikamilifu kukuwezesha kufikia lengo lako.

Kumbuka kuwa njia pekee na bora ya kukuza ukurasa wako ni kwa kuweka vitu vyenye tija na bora kwa wasomaji. Kwani kwa njia hii watu watasambaza post za ukurasa wako au hata kuwakaribisha wengine.

Je bado unataka kununua au kuongeza likes bandia? Naamini hutotaka tena.

Je una swali lolote au maoni? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Ili kufahamu mengi zaidi unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe hapo chini au kwa kulike ukurasa wetu wa Facebook.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x