Mambo 9 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Web Host - Fahamu Hili
Tuesday, February 27Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 9 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Web Host

Washirikishe Wengine Makala Hii:

seva

Kuna mahali ambapo kila tovuti au blog hutunzwa, mahali hapo ndipo hufahamika kama web host. Web host bora ni muhimu sana kwa ajili ya tovuti au blog yako.

Watu wengi wamekuwa wakifanya makosa wakati wa kuchagua web host kutokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa web host bora pamoja na njia za kubaini web host bora.

Madhara ya web host duni ni:

  • Kasi ndogo ya tovuti yako au blog.
  • Athari ya kudukuliwa kutokana na miundombinu duni ya usalama.
  • Kukosa huduma bora na muhimu.
  • Kutokupatikana kwa tovuti yako kila wakati.

Ikiwa unataka kuchagua web host bora kwa ajili ya tovuti au blog yako, basi fahamu mambo 9 muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua web host.

1. Bainisha mahitaji yako

Kabla ya kuchagua web host ni muhimu ubainishe mahitaji yako kwanza. Je tovuti au blog yako itakuwa na watembeleaji wangapi? Itatumia programu au teknolojia zipi?

Hii ni kutokana na baadhi ya web host kuwa na uwezo wa kuhudumia tovuti za aina zote huku nyingine zikiwa na uwezo wa kuhudumia za aina fulani pekee. Hivyo hili litakusaidia kubaini web host itakayokidhi mahitaji yako.

2. Huduma zinazopatikana

Kila web host ina huduma zake inazotoa, hivyo ni muhimu uchague web host ambayo ina huduma za kutosha na za kisasa.

Hakikisha pia huduma zote za msingi unaweza kuzipata bila kulipia gharama za ziada. Unaweza kuchunguza huduma kama hizi zifuatazo:

  • Domain na hosting unayoimudu
  • Huduma za barua pepe (email service)
  • SSL Certificate
  • Backup
  • Script installer (Softaculous, n.k)
  • Bandwidth na Disk space ya kutosha

Huduma kama hizi ni za msingi kwa kila web host bora kuwa nazo.

3. Bei

Bei hutofautiana kati ya web host moja na nyingine, hii ni kutokana na huduma wanazotoa. Ni muhimu kuhakikisha unachagua web host ambayo unamudu gharama zake.

Hakikisha pia njia za malipo zinazotumiwa na web host husika unaweza kuzitumia kufanya malipo. Kumbuka! Usidanganywe na gharama rahisi bali hakikisha ubora wa huduma.

Mara nyingi ni vyema zaidi kununua web host kutoka kwa wamiliki halisi badala ya wauzaji wa pili (resellers) ili kuokoa gharama.

4. Msaada kwa wateja

Unapoendesha tovuti au blog yako unaweza kukutana na changamoto mbalimbali zinazohusiana na web host yako. Hivyo ni vyema kuhakikisha web host unayoichagua ina huduma nzuri kwa wateja wake saa 24 na kwa siku 7.

Ninaipenda sana Smart Host UK kwa sababu watoa msaada wake wana ujuzi mzuri na wanatatua matatizo ya wateja bila shida.

5. Mrejesho wa wateja wengine

Kamwe usijiunge na huduma za web host yoyote kabla ya kufahamu wateja au watumiaji wengine wanasema nini kuhusu web host hiyo. Jipe muda wa kutosha kuitafiti web host husika kwa kina kabla ya kujiunga nayo.

6. Uwezo wa kujitanua

Ni muhimu uweze kubaini kama web host unayotaka kuichagua inauwezo wa kukupa huduma zaidi mara utakapozihitaji.

Kwa mfano umeanzisha blog ndogo baadaye ikakuwa na kuwa na maelfu ya watembeleaji kwa siku, ni wazi utahitaji huduma kubwa zenye nguvu zaidi. Je web host unayotaka kuichagua itakuwa na uwezo huo?

7. Upatikanaji (Uptime)

Uptime ni muda ambao web host inapatikana kwenye mtandao. Mara nyingi kuna wakati web host duni hazipatikani, hivyo huzifanya pia website zote zisipatikane mara zinapotembelewa.

Ni muhimu kuhakikisha kuwa web host unayoichagua ina uptime ya 99.9% kabla ya kujiunga nayo.

8. Miundombinu

Miundombinu ni kitu muhimu sana ili web host iwe bora. Web host nyingi hazina miundombinu bora; zinatumia intanet yenye kasi ndogo, seva zenye ubora mdogo, mifumo ya usalama na backup duni.

Hakikisha kuwa web host imejijenga na kuwekeza sawasawa kwenye biashara na huduma wanayoitoa. Kwa mfano web hosti ya Smart Host UK niliyoitaja awali inatumia intaneti yenye kasi ya zaidi ya GB 10 kwa sekunde, hili linaifanya iwe na kasi kubwa sana.

9. Usalama

Moja kati ya vyanzo vya kudukuliwa kwa tovuti mbalimbali ni kutokuzingatia matumizi ya web host bora. Web host zisizo salama zina virusi na ni rahisi kwa wadukuzi kuziingilia.

Hivyo hakikisha unalinda usalama wa tovuti au blog yako kwa kuchagua web host bora.

Soma pia: Makosa 25 ya Kuepuka Unapotengeneza Tovuti (website) au Blog

Je wewe unatumia web host bora ? Je una swali au shida yoyote kutokana na web hosting? Tafadhali tuandikie hapo chini tukusaidie. Usisahau kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x