Mambo 10 ya Kuzingatia Unapochagua Anwani ya Mtandao (Domain) - Fahamu Hili
Friday, September 29Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 10 ya Kuzingatia Unapochagua Anwani ya Mtandao (Domain)

Washirikishe Wengine Makala Hii:
anwani mtandao
Chanzo cha picha: http://top5-hostingsites.com

Anwani mtandao ni muhimu sana kwa ajili ya utambulisho wa tovuti au blog ya kile unachokifanya. Inawezekana unamajina mengi ambayo unataka uyatumie kama anwani ya mtandao ya tovuti au blog yako; lakini ni muhimu kufahamu kuwa ukifanya makosa kwenye kuchagua anwani ya mtandao utaathirika kwa kiasi kikubwa.

Madhara ya kukosea kuchagua anwani ya mtandao (domain)

  • Kutokutambulisha vyema kile unachokifanya
  • Kukosa nafasi kwenye injini pekuzi
  • Kupoteza wasomaji au watembleaji
  • Kuingia kwenye migogoro ya kisheria ikiwa utatumia anzwani inayofanana na za wengine.

Ikiwa unataka kufungua website au blog kwa ajili yako binafsi au bishara yako, basi fahamu mambo 10 ya kuzingatia unapochagua anwani ya mtandao (domain).

1. Upekee

Hakikisha unapochagua domain ni ya kipekee sana na inajitambulisha yenyewe. Usichague anwani ya mtandao kwa sababu kuna nyingine iinayokaribiana nayo, bali chagua ile ambayo itasimama peke yake kwenye domain nyingine.

2. Kuvutia na kueleweka

Anwani ya mtandao inatakiwa iwe inavutia na kueleweka vyema. Hakikisha huchagui anwani ya mtandao ambayo ni ngumu kutamkwa, kukumbukwa au kueleweka kwa mtu anayeiona.

Kwa mfano:

  • www.pesazakoltdtz.com – Ni anwani ya mtandao mbaya
  • www.habari24hrsleo.com – Ni anwani ya mtandao mbaya

Badala yake zingeweza kuwa:

  • www.pesazako.com, www.pesazakoltd.com, www.habari24hrs.com au www.habari24.com

Naamini umeona mifano hiyo hapo juu ilivyokiuka swala la kuvutia na kueleweka vyema.

3. Usitumie namba na alama ambazo siyo herufi

Anwani ya mtandao nzuri haitakiwi kuwa na namba au alama ambazo siyo herufi kwani itawachanganya watumiaji pamoja na kutokupata nafasi vyema kwenye injini pekuzi.

Mifano ya domain ambazo zimetumia namba na alama nyingine.

www.chakula2953.com, www.nguo-za_watoto-na-vijana.com.

Ni wazi kuwa anwani kama hizi ni vigumu kukuwezesha kufikia lengo lako kupitia tovuti au blog yako.

4. Fikiri matumizi ya mbeleni

Usinunue anwani ya mtandao amabayo haitoweza kukufaa miaka kadhaa ijayo. Epuka kuweka vitu vinavyopita, matukio au watu kwenye anwani ya tovuti au blog yako, kwani vikipita na anwani yako itakuwa imekosa thamani.

Kwa mfano: www.kanumbashop.com, www.prisonbreakmobiles.com, n.k ni baadhi anwani mbaya.

5. Usitumie jina lako kama siyo lazima

Watu wengi hupenda kutumia majina yao kama vile www.johjuma.com, www.rosemoshe.net, n.k. kwenye anwani za tovuti au blog zao, lakini jambo hili siyo zuri sana.

Je jina lako ndilo jina la kampuni au kile unachokifanya? Je watu wanaotafuta vitu kwenye injini pekuzi kama google watatafuta jina lako ili liwawezeshe kufikia tovuti yako, je ni blog binafsi?

Ikiwa majibu ya maswali yaliyoulizwa hapa ni hapana, basi hakuna haja ya kutumia jina lako kwenye anwani ya tovuti au blog yako.

6. Kutambuisha biashara au kile unachokifanya

Kama nilivyoeleza kwenye hoja zilizopita, hakikisha unachagua anwani ambayo inatambulisha vyema kile unachokifanya.

Kumbuka tovuti au blog iliyotengenezwa vyema inaweza kuwa chanzo chako cha kile unachokifanya kufahamika vyema na hatimaye kuongeza mauzo na faida.

Kwa mfano kama unafanya biashara ya chakula unaweza kuwa na anwani kama vile: www.chakulabora.com, www.msosimurwa.com, www.onjamapishi.com, n.k

7. Usiige za wengine

Kuna watu wanafikiri kuiga anwani za tovuti au blog kubwa ndiko kufanikiwa lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

Unapoiga anwani ya tovuti nyingine unaonyesha kuwa huna uwezo mzuri wa ubunifu na pili unaweza kuingia kwenye migogoro ya kisheria  kati yako na wale uliowaiga.

Kwa mfano ukisajili anwani inayoitwa www.facebook.co.tz au co.ke utaingia kwenye mgogoro na Facebook hata kama umeilipia pesa.

8. Chagua anwani fupi

Anwani ndefu ni vigumu kukumbukwa au kuandikwa kwa usahihi. Hivyo ni muhimu kuzingatia kuchagua anwani fupi na nzuri inayoeleweka.

Epuka anwani kama vile www.nunuagarizurikwaajiliyako.com au www.patahabarimotomotokilawakati.com.

9. Gharama

Mara nyingi anwani za mtandao huanzia gharama ya dola 5 hadi 500+. Hivyo ni muhimu kuhakikisha unachagua anwani ya mtandao ambayo unamudu gharama zake.

10. Vikamilisho vya anwani

Kila anwani ya mtandao ina kikamilisho chake kama vile .com, .net, .org, .info, n.k. na kila kimoja kina maana yake kulingana na mahitaji ya mwenye tovuti au blog.

Ikumbukwe pia vikamilisho vya anwani ya mtandao ndivyo huamua bei ya anwani husika.

Hakikisha unachagua kikamilisho ambacho kinaendana na kile unachokifanya ili anwani yako ikuelezee vyema.

Soma pia: Makosa 25 ya Kuepuka Unapotengeneza Tovuti (website) au Blog

Hitimisho

Kuchagua anwani ya mtandao siyo jambo dogo la kukurupuka, linahitaji utulivu na utafiti wa kina ili uweze kupata anwani bora.

Unapochagua anwani kumbuka kutumia huduma kama vile WHOis ili kubaini kama anwani hiyo imeshanunuliwa na mtu mwingine.

Je unahitaji tovuti au blog? Je unahitaji kusajiliwa anwani yako bila shida yoyote na kwa gharama nafuu? Tafadhali wasiliana nasi kwa fahamuhili@gmail.com.

Usisahau kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi pamoja na kuwashirikisha wengine makala hii.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x