Kanuni 15 za Ujasiriamali Ambazo ni Lazima Uzifahamu - Fahamu Hili
Thursday, April 25Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Kanuni 15 za Ujasiriamali Ambazo ni Lazima Uzifahamu

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Ujasiriamali

Ikizingatiwa kuwa upatikanaji wa ajira umekuwa wa shida sana, watu wengi hujikuta wakiwa na chaguo la kuwa wajasiriamali pekee kwenye maisha yao.

Wengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo.

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali.

1. Kuwa mtatuzi wa matatizo

Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu.

Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua, nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.

“Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu”

2. Kuwa na maono

Hakuna ujasiriamali bila maono. Kuwa mjasiriamali bila maono ni sawa na kuendesha gari isiyokuwa na usukani. Maono katika ujasiriamali yatakuwezesha kukuongoza ufanye nini na kwa muda gani. Ni lazima ujiulize kuwa unataka kuwa nani, lini na unataka kufanya nini baadaye? Jonathan Swift alisema maono ni sanaa ya kuona kile ambacho wengine hawaoni. Ni lazima uwe na lengo na ufanye bidii kulifikia.

“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia”

3. Chagua washirika au timu sahihi

Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama mjasiriamali.

Soma pia: Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka.

4. Toa huduma au bidhaa yenye tija

Hivi leo sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri. Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.

Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako.

5. Fahamu na jali wateja

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, basi futa mawazo kuwa wateja wanakuhitaji wewe. Fahamu kuwa wewe kama mjasiriamali, ndiye unaye wahitaji wateja ili ukuze biashara au huduma yako. Hakikisha mambo haya kuhusu wateja:

  • Fahamu wanataka nini.
  • Sikiliza maoni na ushauri wao.
  • Hakikisha unakamilisha mahitaji yao.
  • Tumia lugha nzuri na rafiki kwa wateja.
  • Mfanye mteja aone unamthamini.
  • Mfanye mteja aone kuwa umetanguliza huduma kabla ya pesa.

Naamini kwa kufanya hivi utaweza kujijengea msingi mzuri wa wateja kwa ajili ya huduma au bidhaa zako kila siku.

6. Tumia pesa vyema

Changamoto ya matumizi mabaya ya pesa inawakabili watu wengi kuanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa. Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.

Soma pia: Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema.

Ni wazi kuwa matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.

Unaweza pia kujifunza wewe mwenyewe jinsi ya kutunza na kutumia pesa vyema; unaweza pia kutumia programu za bure za kompyuta kama vile Wave app kutunza mahesabu yako.

7. Jifunze kusema hapana

“Hapana” ni jibu dogo lakini lenye manufaa makubwa. Ikiwa wewe ni mjasiriamali ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kusema hapana kwani itakutenga na mambo au mipango isiyokuwa na ulazima.

Kuna watu, mipango, vitu au hata tabia ambazo zinaweza kukuathiri vibaya sana kwenye ujasiriamali wako. Hivyo kusema hapana kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na mambo haya.

Soma pia: Tabia 10 zitakazobadili maisha yako.

8. Usipuuze nafasi ya teknolojia

Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia, hivyo wewe kama mjasiriamali huwezi kujitenga nao. Kwa kupitia teknolojia kama vile simu na mtandao wa intaneti, unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza mauzo ya huduma au bidhaa zako.

Hakikisha wewe kama mjasiriamali unakuwa karibu na wateja wako ili kutatua shida na mahitaji yao; pia hakikisha unajifunza mbinu bora za kufanya biashara kupitia mtandao.

Soma pia: Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao.

9. Fahamu soko

Kanuni mojawapo ya kuongeza mauzo yako kama mjasiriamali ni kulifahamu soko vyema. Hakikisha huduma au bidhaa unayoitoa inakidhi mahitaji na inafika kwenye soko stahiki.

Kwa mfano ikiwa wewe ni mzalishaji wa mayai, lakini eneo ulilopo soko ni duni, basi tafuta eneo jingine ambalo soko la bidhaa hii ni nzuri. Ikiwa wewe huwezi kwenda, unaweza kutafuta mtu kwenye eneo lenye soko zuri akakuuzia bidhaa yako na ukampa gawio fulani.

Kwa kufanya hivi utaweza kulenga soko na kujiongezea faida zaidi wewe kama mjasiriamali.

10. Ongeza maarifa

Kwanza nikupongeze kwa kusoma makala hii, ni wajasiriamali wachache sana ndiyo hupenda kusoma makala na vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa. Ni muhimu sana kila mara ukajizoesha kujiongezea maarifa, hasa ya ujasiriamali pamoja na kile unachokifanya; hili liitakuwezesha kuwa na tija na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Unaweza kusoma vitabu, majarida na tovuti mbalimbali (kama fahamuhili.com) ili kuongeza maarifa yako.

11. Jifunze kutokana na makosa

Moja ya kanuni inayozingatiwa na wajasiriamali waliofanikiwa ni kujifunza kutokana na makosa. Makosa ni shule nzuri sana kwa kila mtu hasa wajasiriamali. Ikiwa uliwekeza ukapata hasara, basi jifunze nini hasa kilikuwa chanzo cha hasara ili mbeleni uweze kukiepuka. Usikubali kukwamishwa na makosa, bali yawe ni hamasa kwako ya kuendelea mbele zaidi.

“Uzoefu ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo”

Bill Ackman

12. Jifunze kwa waliofanikiwa

Watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwenye maisha yao kwa sababu wanajifunza kwa walioshindwa. Walioshindwa wana maneno mengi, hasa ya kukatisha tamaa kama vile hili haliwezekani, hili linahitaji pesa nyingi sana, mimi lilinishinda, linachosha, lina faida ndogo, kuna wengi wanaolifanya, fulani alishindwa n.k.

Wewe kama mjasiriamali, epuka watu hawa na ujifunze kwa waliofanikiwa, fahamu walitatua vipi changamoto walizokabiliana nazo pamoja na mipango waliyoitumia hadi wakafika hapo walipo.

13. Tumia muda vizuri

Hakuna mtu mwenye zaidi ya saa 24 duniani; lakini mwingine muda unamtosha wakati mwingine analalamika  muda haumtoshi. Ni wazi kuwa mpangilio au matumizi mabaya ya muda ndiyo husababisha changamoto hii. Wewe kama mjasiriamali ni muhimu ukaondoa mambo yasiyokuwa na ulazima kwenye ratiba yako. Tambua ni kitu gani ni cha muhimu zaidi na ukifanye kwa wakati.

Soma: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

14. Weka vipaumbele

Wewe kama mjasiriamali, ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kujiwekea vipaumbele; vipaumbele vitakuwezesha kubaini ni kipi kianze na ni kipi kifuate kutokana na umuhimu wake.

Kwa mfano ikiwa kuna wateja walipata shida kupata huduma au bidhaa yako, maliza kwanza swala hili kabla ya kuendelea kuweka jitihada za kuuza bidhaa mpya. Kwa kufanya hivi utaweza kufanya mambo kutokana na umuhimu wake, jambo ambalo litakuwezesha kukua.

15. Usikate tamaa

Ni wazi kuwa katika safari ya ujasiriamali utakutana na changamoto mbalimbali. Jambo la msingi ni kukumbuka kanuni hii kuwa usikate tamaa. Tumia changamoto kama chachu ya kukuhamasisha kufanya bidii zaidi na usirudi nyuma.

Changamoto zipo leo na kesho lakini keshokutwa hazitakuwepo tena; jambo unalotakiwa kufanya ni kutazama lengo lako na kufanya bidii kila kukikucha kuzikabili changamoto husika ili ufikie lengo lako.

“Siri ya mafanikio yetu ni kutokukata tamaa”

Wilma Mankiller

Soma pia: Hatua 7 za Maumivu Zisizoepukika Kabla ya Kufanikiwa.

Hitimisho

Naamini umefahamu kuwa kuna kanuni muhimu ambazo wewe kama mjasiriamali unatakiwa kuzizingatia ili uweze kufanikiwa. Ni wazi kuwa bidii, mipango mizuri na kutokukata tamaa kutakuwezesha kufikia lengo lako la kufanikiwa kama mjasiriamali.

Je una swali, maoni au changamoto ambayo ungependa kutushirikisha? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini nasi tutafurahi kukuhudumia. Pia unaweza kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook pamoja na kuwashirikisha wengine makala hii.

4 9 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

58 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mwl Shija
Mwl Shija
6 years ago

Ni vitu gan vya kuzingatia kabla hujaanza ujasiriamali

imanuemgawe
imanuemgawe
Reply to  Kornelio Maanga
4 years ago

samahani naitwa ima naomba mnijuze kuhusu ujasiriamali

Saitoti
Saitoti
Reply to  imanuemgawe
1 year ago

Kazi nzuri, keep it up!

Warren Blassio Chobya
Warren Blassio Chobya
5 years ago

ahsante sana kwa mafunzo haya ni dalasa tosha, mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha TUMAINI MAKUMIRA ARUSHA. ninalenga kuanzisha kituo cha kufundisha kuanzia ngazi ya sekondari hadi advance..naomba ushauri nifanye nn kufanikisha lengo langu

Samson nkwande
Samson nkwande
4 years ago

je ujasiliamali unahitaji kuwa na elimu stage gani?

Hassanikaimite
Hassanikaimite
4 years ago

Elimu nzur sana

WINANI DANIEL
WINANI DANIEL
Reply to  Kornelio Maanga
4 years ago

KAMA KAWA

Onesmo
Onesmo
4 years ago

Nafurah Sana kusoma nakala hii pia imenifunza

Ila mimi ninatatizo la kutokujua lipu nkfanye na kwawakati gani naomba msaada

Josephine
Josephine
4 years ago

Jinsi gan nawez kupata mtaji

Polycarp
Polycarp
4 years ago

Nawezaje kupata mtaji

KHAMIS KAFUKU
KHAMIS KAFUKU
4 years ago

Nimefurahi Sana na nimejifunza vitu vikubwa viwili, MUDA, KUJIFUNZA KWA ALIYE FANIKIWA

GELARD MASAMI
GELARD MASAMI
4 years ago

Kwanza nakushukru sana Bwn K. Maanga kwa kuchukua mda wako tuwapa watanzania elimu ya ujasiliamali.
Sasa ndg yangu kuna changamoto ya mtaji. Mtu unaweza kuwa nawazo la kuwekeza mradi flani lkn changamoto ikawa mtaji.
Sasa kwa mtu mwenye upungufu wa mtaji anaweza kutumia njia zipi kufikia malengo yake.

GELARD MASAMI
GELARD MASAMI
Reply to  Kornelio Maanga
4 years ago

Aya asante ssns

Joseph nicco
Joseph nicco
4 years ago

Nmemalza kdato cha nne mwak jan nmefaul kwango cha div.3 bht mby au nzur xjachaguliw kuendlea na masom unanixhaur nfanyaje

Micle darl
Micle darl
4 years ago

Yes

Isihaka issa msangi
Isihaka issa msangi
4 years ago

Habari ya leo nashukuru kwa elimu nzuri sana kwa wanajamii nzima kwa kupoteza muda wako kutuelimisha tunashkuru kwa hilo…..

Jambo langu ni dogo lakini kubwa sana kwa upande wangu nimeanzisha biashara dogo ya ubunifu na kiasi chake nimejitahidi kuweka bidhaa yangu kwenye ubora mzuri kiasi chake na baadhi ya watumishi nilio washirikisha kunishauri wamenishauri vzr pia….Ila swali nalo liomba kushauri ni namna ya kupata masoko soko la bidhaa yangu bado ni duni sasa nashindwa kuelewa ni mkoa niliopo ndo tatizo la kuto kukua kwa biashara yangu au la naomba ushauri wako nifanye nini kufanya bz yangu iwe kubwa

markus mwalongo
markus mwalongo
3 years ago
  1. nashukuru sana kwa elimu nzuri, natamani sana kufanya biashara ya mafuta ya alizeti, kikwazo nipo kwenye ajira nitawezaje kumudu changamoto hii ya kukosa muda na biashara ikiwa bado ngeni?
AJUAYE
AJUAYE
3 years ago

About self development

AJUAYE
AJUAYE
3 years ago

Naitwa AJUAZY PHENSON
Nifate njia zipi I’ll kuzikabili changamoto zinazotokana na mabadiliko ya hewa na ulimwengu kwa ujumla .
Mfano nilikuwa mkulima wa mazao ya chakula 🌽 🌽 ila kutokana na janga la CORONA kilimo hiki kimekufa kutokana na kwamba niliwekeza mtaji mkubwa kwenye kilimo lakini mwisho masoko yalikosekana..
He nifanye nin kujikinga na athari kama hizi??# @ajuzy@

Ifande
Ifande
3 years ago

Nakubali kujiunga

Godfrey
Godfrey
2 years ago

Kwanza nikupongeze kwa makala Yako,Naitwa Godfrey Niko mwanza naitaji kuanzisha Biashara ya viungo karibu

Mawe budidi
Mawe budidi
2 years ago

Nice

New ndabilah
New ndabilah
2 years ago

Samahan ingawa nimechelewa kuisoma , Napenda sana ujasiriamali lakin tatizo lang ni nakuwa na malengo mengi kichwani ndan ya mwaka mmoja,alafu nakuja kujikuta mwaka umeisha kila lengo nimeairisha

Vitus komva
Vitus komva
1 year ago

Nataka kujua kanuni za biashara ndogondogo

Eliya
Eliya
1 year ago

Naitwa eliya sanya kutoka dodom mada namba Saba tabia zitazobadisha Maisha yako hujamaliziaa kaka

Damas nestori
Damas nestori
1 year ago

Good

Chriss
Chriss
1 year ago

Very nice

Mustaph
Mustaph
1 year ago

Hi naomba mni ad kwenye whatsapp group tafadhali

Jàzr abdul
Jàzr abdul
1 year ago

Jinsi ya kujua wateja wanahitaj nn?

Binti Bori
Binti Bori
11 months ago

Mimi nina tatizo la jinsi gani nitatumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yangu kama instagram

Isaka
Isaka
9 months ago

Nipe kwenye email

58
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x