Mambo 20 ya Kukushangaza Kuhusu Dhahabu - Fahamu Hili
Thursday, March 28Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 20 ya Kukushangaza Kuhusu Dhahabu

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Dhahabu

Dhahabu ni moja kati ya madini ya thamani duniani. Dhahabu huchimbwa katika sehemu mbalimbali duniani na kisha kutumiwa kutengeneza vitu mbalimbali kama vile fedha, medali, vito vya thamani n.k

Nchi nyingi zimejizolea utajiri mkubwa kutokana na madini haya; pamoja na utajiri huu pia nchi nyingi zimesababishiwa uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na uchimbaji wa dhahabu.

Naamini umewahi kusikia mengi kuhusu dhahabu, lakini sasa fuatilia makala hii nikufahamishe mambo 20 yakushangaza kuhusu dhahabu.

  1. Katika tani moja ya simu za mkononi unaweza kupata dhahabu nyingi zaidi kuliko ambayo ungeipata kutoka kwenye gwangala la dhahabu (gold ore).Simu
  2. Ikiwa utafanikiwa kukusanya dhahabu yote iliyoko baharini, basi kila mtu duniani anaweza kupata dhahabu takriban kilo 4. Inakadiriwa kuwa kuna takriban tani milioni 20 za dhahabu baharini.
  3. Mwanakemia wa Hungary George de Havesy aliyeyusha tuzo za Nobel za wanafizikia wa Kijerumani Max von Laue na James Franck, ili kuzuia utawala wa Kinazi kuzitaifisha. Hata hivyo tuzo hizo za dhahabu ziliundwa tena upya baada ya vita.
  4. Manahodha wengi wa kale walivaa hereni ya dhahabu ili wakizama majini na miili yao itakapookotwa ufukweni, basi hereni hiyo iuzwe ili igaramie garama za mazishi.
  5. Medali ya Olimpiki ina kiasi cha asilimia 1 pekee ya dhahabu.Olimpic
  6. Huko dubai kuna ATM kwa ajili ya kutolea vitofali vya dhahabu. Je wajua kuwa utajiri huweza kuhifadhiwa kwa vipande au vitofali vya dhahabu? Basi huko dubai matajiri wanaweza kutoa vipande hivi kwenye ATM kama watoavyo pesa.ATM za dhahabu
  7. Dhahabu nyingi iliyoko kwenye kokwa (crust) la dunia imetokana na asteroidi zilizoanguka duniani.
  8. Dhahabu nyingi zaidi ipo kwenye kiini cha kokwa la dunia kutokana na kuzama huko wakati dunia inaumbwa.Crust
  9. Waonjaji wa ice cream za bei ghali hutumia vijiko vya dhahabu ili kuhakikisha hawachanganyi ladha kutoka ice cream moja hadi nyingine.Kijiko cha Dhahabu
  10. Mwanasiasa wa Kirumi Gaius gracchus, kichwa chake kilihitajika kwa malipo ya dhahabu sawa na uzito wake. Hivyo atakayemuua na kupeleka kichwa chake angepewa dhahabu sawa na uzito wa kichwa hicho. Hata hivyo dhahabu hii haikulipwa kwa mtekaji kwa sababu alikijaza kichwa hicho madini ya risasi ili kiwe kizito zaidi.
  11. Mansa Musa, kiongozi wa Dola ya Mali, alitumia dhahabu nyingi huko Misri aliyoishusha thamani na kukaribia kuharibu uchumi.Mansa Musa
  12. Wafungwa wa China hulazimishwa kuchimba dhahabu kwa ajili ya shughuli za kijeshi.
  13. Kampuni ya kutengeneza midoli ya plastiki ya LEGO hutoa dhahabu gramu 25.65 kwa wafanyakazi waliotimiza miaka 25 ya utumishi katika kampuni hiyo.
  14. Je unafahamu kuwa kuna aina ya dhahabu inayoweza kuliwa? Ipo aina ya dhahabu laini ambayo inaweza kuliwa.

    Chakula chenye Dhahabu
    Chakula aina ya burger chenye Dhahabu kinachouzwa dola za Marekani 600
  15. Dhahabu ni madini yanayopatikana kwenye kila bara duniani.
  16. Karibu nusu yote ya dhahabu iliyowahi kuchimbwa duniani, imetoka Witwatersrand huko Afrika ya Kusini.

Soma Pia: Mambo 15 ya Kushangaza Kuhusu Afrika.

  1. Aurophobia ni hofu ya kuogopa dhahabu. Watu wenye Aurophobia huogopa mwonekano na maana ya dhahabu (nguvu au kifo). Asili ya neno auro ni neno la Kilatini linalomaanisha dhahabu,  wakati phobia ni neno la Kigiriki linalomaanisha hofu.
  2. Wanawake wa India wanavaa asilimia 11 ya dhahabu yote iliyoko duniani. Hiki ni kiasi cha zaidi ya kilichoko Marekani, Uswisi, Ujerumani na IMF zikijumuishwa kwa pamoja.Mkufu wa India
  3. Kipande au tofali kubwa zaidi la dhahabu duniani lina kilo 250. Tofali hili linamilikiwa na kampuni ya Mitsubishi, na linakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani 3,684,000.Tofali la Dhahabu
  4. Simu ya ghali zaidi duniani ya iphone5 imetengenezwa kwa dhahabu na ina thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 8. Simu hii pia imewekewa almasi nyeupe.iphone

 

Naamini umejifunza mengi; pia naamini umefurahia makala hii. Je una swali au ushauri kuhusu makala hii? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Pia usisahau kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook

2 1 vote
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

2 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Felixlyamuya
Felixlyamuya
2 years ago

Can you tell me how to do and get gold and which chemicals am i sapposed to use couse ihave dat things

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x