Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara
Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii. Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako. Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara.
1. Chagua wazo unalolipenda Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto. Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa.
2. Chagua wazo unalolifahamu na kulimu...