Mambo 5 ya Kujifunza Kutoka kwa Reginald Mengi - Fahamu Hili
Friday, April 26Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Mambo 5 ya Kujifunza Kutoka kwa Reginald Mengi

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Reginald Mengi

Kwa mijibu wa jarida la Forbes linaeleza kuwa Reginald Mengi ni miongoni mwa watu maarufu katika tasnia ya habari kupitia kampuni yake ya IPP; ambayo ni moja kati ya kampuni kubwa za habari Afrika.

Kampuni yake ya IPP ina magazeti 11 na vituo kadhaa vya televisheni pamoja na vyanzo mabalimbali vya kwenye mtandao. Mengi pia anamiliki kampuni ya vinywaji baridi ya Bonite Bottlers, ambayo ni kampuni pekee inayozalisha vinywaji vya jamii ya Coca-Cola kwa kanda ya kaskazini mwa Tanzania. Pia anazalisha maji ya Kilimanjaro yaliyojizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania.

Mengi anajihusisha pia na uchimbaji wa madini kupitia kampuni yake ya IPP Resources yenye kampuni tanzu kadhaa.

Reginald Mengi pia mekuwa akitoa misaada mbalimbali kusaidia makundi ya watoto, vijana, wanawake, wazee, wangonjwa, wajasiriamali n.k.

Tuzo: Reginald mengi amepokea tuzo kadha wa kadha kutokana na mchango wake alioutoa katika jamii kama vile:

  • The Business for Peace Award 2012
  • 2010 Global Leadership and Humanitarian Award
  • The 1st United Nations NGO Lifetime Achievement Award.
  • Martin Luther King Drum Major for Justice Award ( 2008)
  • Most Respected CEO
  • Environmental Leadership Award

Hizi ni baadhi tu, kwani zipo na nyinginezo nyingi (Nyingine).

Kwa ujumla Reginald Mengi ni moja kati ya matajiri na watu waliofanikiwa sana nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Safari ya mafanikio ya Reginald Mengi haikuanza kama ndoto ya mchana, bali ina mambo mengi ambayo mtu yeyote anayetaka kufanikiwa unaweza kujifunza.

1. Alizaliwa na kuanzia katika umaskini

Reginald Mengi alizaliwa katika familia maskini kaskazini mwa Tanzania. Waliishi katika nyumba moja ya tope pamoja na mifugo ya familia yao kama vile mbuzi, ng’ombe, kondoo  na hata kuku. Alikuwa akipata mlo mmoja au kutopata kabisa kwa siku, pia alikwenda shuleni bila viatu.

Pamoja na changamoto hizi, hatimae alifanikiwa kusoma uhasibu huko Uingereza na kurejea Tanzania mwaka 1971 na kuajiriwa na Coopers & Lybrand Tanzania. Mnamo mwaka 1989 aliacha kazi na kuanzisha kampuni yake ya sasa ya IPP.

Hapa ni dhahiri kuwa safari ya mafanikio haianzii kwenye mafanikio bali huanza kwenye shida na changamoto kadha wa kadha. Jiwekee malengo, fanya bidii, jali muda na kwa hakika utafikia mafanikio yako.

2. Kutokukata tamaa

Kukata tamaa kumekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa wajasiriamali au watu wanaojitahidi kufikia malengo yao, kwani changamoto za awali huwasababisha watu kukata tamaa. Jifunze kwa Reginald Mengi jinsi ambayo hakuruhusu hali na mazingira yaliyokuwa yanamzunguka kumrudisha nyuma katika malengo na maono yake. Ni dhahiri kuwa mazingira za miaka hiyo ya 1980 hayakuwa rafiki kama yalivyo hivi leo, lakini hakuruhusu kukata tamaa.

3. Ana udhubutu

Udhubutu ni jambo muhimu sana katika kukuwezesha kufikia malengo yako. Watu wengi wana mawazo mazuri lakini wana hofu ya kuyafanyia kazi. Je unataka kuanzisha biashara lakini unaogopa? Unataka kubuni kitu lakini unaogopa au unatishwa na mazingira? Hakika Reginald Mengi ni mfano mzuri wa mtu mwenye udhubutu. Mengi alidhubutu kuacha kazi yake nzuri na kuanzisha kampuni zake kadhaa ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa hata kuwapa maelfu ya watu ajira. Dhubutu leo na utekeleze wazo lako, kwani kikwazo cha kwanza ni wewe.

4. Kutofautisha siasa na uwekezaji

Siasa ni nyanja isiyoweza kutengwa na binadamu, lakini inapochanganywa na biashara au uwekezaji huweza kuleta matokeo mabaya. Reginald Mengi ni mfano mzuri wa wafanyabiashara ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutenganisha biashara zake na siasa.

Madhara ya kuchangaya biashara na siasa:

  • Kutengeneza makundi na migawanyiko ndani ya biashara au kampuni yako.
  • Migongano kati ya pande tofauti na siasa zilizoko ndani ya kampuni yako.
  • Kuanguka kwa kampuni iwapo siasa zinazoungwa mkono na kampuni zitaanguka.

Hivyo basi ni vyema ukajifunza jambo hili kutoka kwa Reginald Mengi la kutokuonyesha dhahiri kuegemea upande fulani wa siasa. Siasa ibaki kuwa moyoni mwako tu, na sio katika kampuni au biashara zako.

5. Anatambua umuhimu wa kutoa

Kuna siri kubwa sana iliyojificha katika utoaji, watu wengi hawazingatii wala hawajui umuhimu wake. Umekuwa ukiwashuhudia matajiri mbalimbali kama vile Bill Gates, Henry Ford, Warren Buffet wakitoa sehemu ya utajiri wao kusaidia watu; hivi huwa wanapata nini hasa? Kanuni ya kupokea ni kutoa, hivyo Reginald Mengi ni moja kati ya watu wanaotambua kanuni hii vyema. Kwani amekuwa mstari wa mbele kusaidia watu mbalimbali kupitia utajiri wake.

Jifunze na wewe leo kutoa kadri ulivyojaliwa. Kwa njia hii pia hata wale wateja wako watatambua kuwa wewe si mnyonyaji bali ni sehemu yao na unawajali.

Hitimisho

Hapa nimeeleza mambo matano tu ambayo unaweza kujifunza kutoka kwa Reginlad Mengi, lakini naamini yapo mengi zaidi mazuri ya kujifunza. Hivyo  basi, ni jukumu lako kujifunza kwake kwani ni mtu aliyefanikiwa sana. Siku zote epuka kujifunza kwa walioshindwa kwani wamejawa na maneno matupu yasiyokuwa na hili wa lile.

Je una maoni gani kuhusu makala hii? Je umejifunza kitu? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini, kisha washirikishe wengine.

4.5 2 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

6 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NESTORY ISAYA
NESTORY ISAYA
5 years ago

Nimependa hbr menu endeleeni kutujuza mambo Kama hayo has a ss vijana

almachius
almachius
2 years ago

jambo jema kujifunza kwa waliofanikiwa

Johari
Johari
1 year ago

Namba mawazo Zaid mm nahtaj kua mjasilimali lkn CNA mtaji ntapataje…

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x