Malengo Archives - Fahamu Hili
Thursday, March 28Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tag: Malengo

Mambo 20 Yakushukuru Kwa Ajili Yake Kwenye Maisha

Mambo 20 Yakushukuru Kwa Ajili Yake Kwenye Maisha

Hamasa
Wakati mwingine tunatazama tu mambo ambayo hatuna kwenye maisha, kuliko yale tuliyo nayo. Mara nyingi huwa hatutambui umuhimu wa kitu hadi pale tunapokikosa. Niwazi kuwa wapo watu wanaotafuta vile tunavyoviona ni vidogo lakini hawavipati. Ni muhimu kutenga muda wa kukumbuka yale mambo yote ambayo tunapaswa kushukuru kwa ajili yake. Kama una chochote kati ya hivi basi yakupasa kushukuru. Afya njema Mara nyingi hatutambui kuwa na afya njema pekee ni jambo muhimu na kubwa sana. Kuna wengi wanaotamani kuwa na afya kama ya kwako lakini hawana; hivyo yakupasa kushukuru kwa afya njema. Pesa ulizonazo Unaweza kufikiri kiasi cha pesa ulizonazo ni kidogo sana hivyo hauhitaji kushukuru. Kuna mahali pengine wewe ni tajiri mkubwa sana. Wapo wasiokuwa na pesa wala chochote kile wanachow...
Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako

Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako

Maendeleo Binafsi
Ni mara ngapi umejiambia kuwa kesho itakuwa siku nzuri na unatamani kuiona na kuiishi? Ni mara chache sana. Hofu na mashaka vimetawala na kuchukua nafasi katika kesho za watu wengi. Jambo zuri kwenye maisha ni kuwa una nafasi ya kutawala mambo mengi yanayotokea katika maisha yako. Kama kesho inafanana na leo hakuna maana; ikiwa leo ulikuwa na huzuni basi angalau kesho iwe na furaha. Hivyo kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya leo na kuhakikisha kuwa kesho inakuwa nzuri. Hapa kuna mambo 12 ambayo unayoweza kuyafanya na kuifanya kesho yako kuwa nzuri na yenye tija. 1. Panga kwa ajili ya kesho. George anatukumbusha  kuwa maandalizi bora ya kesho hufanywa leo. Kuwa na mpango wa kesho leo kutakuwezesha kufanya mambo kwa kutegemea mwongozo na mpangilio uliopo badala ya kuamka na kufan...
Vitu 15 Vinavyofanywa na Watu Werevu (Smart)

Vitu 15 Vinavyofanywa na Watu Werevu (Smart)

Tija
Unaweza kujiuliza ni mambo gani yanayomfanya mtu kuwa mwerevu (smart). Je ni wingi wa maarifa anayoyafahamu? Au je ni kiwango cha wastani au cha juu cha kufikiri kwake? Ukweli ni kuwa ni werevu ni uwezo wa kufanya maamuzi yatakayofaa wakati wote; au ni kuweza kuibua kitu kizuri katika kitu kibaya au wakati mbaya. Watu werevu huweza kufanya maamuzi ambayo yanazingatia matokeo ya mbeleni ya maamuzi hayo. Ni dhahiri kuwa watu werevu (smart) ni tofauti na watu wengine kutokana na yale wanayoyafanya au kutofanya. Fahamu mambo 10 ambayo watu werevu hawayafanyi. 1. Hawapuuzi uwekaji akiba Katika maisha ya kiuchumi kuna vipindi viwili; kipindi cha mavuno(shibe) na kipindi cha ukame(njaa). Ni watu wachache sana ndio wanaoweza kuishi katika vipindi hivi viwili bila shida. Watu werevu hawapu...
Kitu Muhimu Mark Zuckerberg Alichokijenga Harvard

Kitu Muhimu Mark Zuckerberg Alichokijenga Harvard

Hamasa
Mark Zuckerberg akiwa chuoni Harvard Ukimuuliza Mark Zuckerberg juu ya alichokikamilisha alipokuwa akisoma chuoni Harvard jibu lake linaweza kukushangaza. Unaweza kufikiri ni Facemash ambayo baadaye ilikuja kuwa Facebook lakini siyo. "Priscilla ni mtu muhimu zaidi katika maisha yangu, na jambo muhimu zaidi nililojenga wakati wangu hapa." Zuckerberg alisema hayo kuhusu mke wake wakati wa hotuba ya ufunguzi wa mahafali huko kwenye chuo cha Harvard mwaka huu. Mkurugenzi huyu mkuu wa Facebook mwenye miaka 33 alitumia kiasi kikubwa cha muda wake wakati wa hotuba hiyo akionyesha jinsi alivyokutana na Priscilla Chan, daktari wa watoto ambaye hatimaye walifunga ndoa mwaka 2012. Mark Zuckerberg na mke wake Priscilla Chan Zuckerberg alikutana na Chan kwenye sherehe na akampenda. Chan ...
Mambo 5 ya Kujifunza Kutoka kwa Reginald Mengi

Mambo 5 ya Kujifunza Kutoka kwa Reginald Mengi

Hamasa
Kwa mijibu wa jarida la Forbes linaeleza kuwa Reginald Mengi ni miongoni mwa watu maarufu katika tasnia ya habari kupitia kampuni yake ya IPP; ambayo ni moja kati ya kampuni kubwa za habari Afrika. Kampuni yake ya IPP ina magazeti 11 na vituo kadhaa vya televisheni pamoja na vyanzo mabalimbali vya kwenye mtandao. Mengi pia anamiliki kampuni ya vinywaji baridi ya Bonite Bottlers, ambayo ni kampuni pekee inayozalisha vinywaji vya jamii ya Coca-Cola kwa kanda ya kaskazini mwa Tanzania. Pia anazalisha maji ya Kilimanjaro yaliyojizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania. Mengi anajihusisha pia na uchimbaji wa madini kupitia kampuni yake ya IPP Resources yenye kampuni tanzu kadhaa. Reginald Mengi pia mekuwa akitoa misaada mbalimbali kusaidia makundi ya watoto, vijana, wanawake, wazee, ...
Hatua 7 za Maumivu Zisizoepukika Kabla ya Kufanikiwa

Hatua 7 za Maumivu Zisizoepukika Kabla ya Kufanikiwa

Hamasa
Mafanikio ni safari ndefu. Katika safari ya mafanikio kuna mengi, milima na mabonde yasiyotabirika. Wengi huanza safari ya mafanikio wakiwa na malengo makubwa, lakini wanasahau kuwa kufanikiwa ni kupambana na changamoto bila kukata tamaa huku ukiyatazama malengo na maono yako. Kama unalenga kufanikiwa katika maisha yako ni vyema ukazifahamu hatua hizi saba za maumivu zisizoepukika katika safari hiyo. 1. Utahisi maumivu Kila mtu aliyefanikiwa amepitia kwenye safari yenye maumivu; ikumbukwe kuwa kupita njia yenye changamoto ndiko hutuelekeza kwenye mafanikio. Jifunze kutumia changamoto na maumivu kuwa kama hamasa ya kufanya juhudi zaidi kufikia mafanikio. Hakuna haja ya kulalamika na kukata tamaa bali anzia ulipo kwenda mbele ili kukamilisha malengo yako. 2. Kutamani kukata tamaa m...
Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako

Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako

Maendeleo Binafsi, Tija
Kila mmoja ana ndoto zake katika maisha yake. Wengine wana ndoto kubwa za kubadilisha ulimwengu huu, huku wengine wakiwa na ndoto za kuishi maisha ya kupata mahitaji yao ya msingi tu. Wote hawa wanahitaji kuzitimiza ndoto zao; lakini kuna vikwazo na mambo mbalimbali ambayo huwazuia watu wasiishi ndoto zao na kuishia kulamu na kulalamika hasa uzeeni. Fuatana nami katika makala hii nikueleze dondoo tano za msingi zitakazokuwezesha kuishi ndoto zako. 1. Tambua kinachokuvuruga Maisha yetu ya kila siku yamejaa vitu na shunguli mbalimbali lakini si zote huturuhusu kuishi katika ndoto zetu. Inawezekana unapenda kitu au tabia fulani kiasi kwamba imetawala au imekuwa ya kwanza kwenye maisha yako. Nitajuaje kitu au tabia imetawala/imekuwa ya kwanza katika maisha? Jibu ni rahisi, kile una...