Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako - Fahamu Hili
Friday, May 24Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Kijana anawaza

Kila mmoja ana ndoto zake katika maisha yake. Wengine wana ndoto kubwa za kubadilisha ulimwengu huu, huku wengine wakiwa na ndoto za kuishi maisha ya kupata mahitaji yao ya msingi tu.

Wote hawa wanahitaji kuzitimiza ndoto zao; lakini kuna vikwazo na mambo mbalimbali ambayo huwazuia watu wasiishi ndoto zao na kuishia kulamu na kulalamika hasa uzeeni.

Fuatana nami katika makala hii nikueleze dondoo tano za msingi zitakazokuwezesha kuishi ndoto zako.

1. Tambua kinachokuvuruga

Maisha yetu ya kila siku yamejaa vitu na shunguli mbalimbali lakini si zote huturuhusu kuishi katika ndoto zetu. Inawezekana unapenda kitu au tabia fulani kiasi kwamba imetawala au imekuwa ya kwanza kwenye maisha yako. Nitajuaje kitu au tabia imetawala/imekuwa ya kwanza katika maisha? Jibu ni rahisi, kile unachokipa muda mwingi ndicho cha kwanza.

Inawezekana unapenda mpira wa miguu kiasi kwamba hata kama ulitakiwa ufanye kitu gani swala la mpira likitokea utakatisha; au mwingine inawezekana ni TV, pombe, marafiki, filamu, mziki (disko n.k)

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakiwavuruga watu wengi wasiweze kuishi ndoto zao hasa kuanzia katika ngazi ya masomo hadi maisha ya kawaida.

Mambo ya kufanya:

 • Epuka kupoteza muda kwenye vitu visivyokuwezesha kuishi au kufikia ndoto zako.
 • Pangilia muda kwa kujiwekea ratiba utakayoifuata.
 • Ondoka katika mazingira yanayokushawishi kufuata vitu hivyo.
 • Jiwekee malengo.
 • Weka vipaumbele sahihi katika maisha yako.

Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

2. Tathimini upya marafiki zako

Kila mtu ana marafiki katika maisha yake, lakini si wote wana manufaa kwako. Je ulishawahi kujiuliza ni marafiki wangapi uliokuwa nao shule ya msingi au sekondari na bado wanakufaa hadi sasa? Marafiki wanatakiwa wakuinue unapoanguka au unapozama wakuokoe na si kukuzamisha zaidi.

Je ni marafiki gani wa kuwaepuka?

 • Marafiki wasiojali muda na wavivu.
 • Marafiki wanopenda starehe na anasa.
 • Marafiki wasiopenda elimu na maarifa.
 • Marafiki wasiokuwa na malengo na maono ya mbeleni.
 • Marafiki wasiojua kuweka akiba – wao hutumia kila wanachokipata.
 • Marafiki wasioweza wala kupenda kukushauri na kushauriwa.

Ukiwaepuka hawa hakika utabakia na wale ambao hawatakuwa ni kikwazo kwako wewe kutimiza na kuishi ndoto zako.

Soma pia: Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako.

3. Oa au olewa na mtu sahihi

Je unajua kuwa swala la ndoa lina nafasi kubwa sana katika swala la wewe kuishi ndoto zako? Ukifanya uamuzi mzuri katika swala la ndoa utapa mwenzi ambaye hatokuwa mzigo na kikwazo kwako katika kuishi ndoto zako.

Faida za kuoa au kuolewa na mtu sahihi:

 • Atakujali na kukutia moyo kila wakati.
 • Mtapanga mipango mabali mbali ya maendeleo pamoja.
 • Mtasaidiana na kutiana moyo wakati wa shida.
 • Mtahamasishana ili kuhakikisha manafikia ndoto zenu.
 • Atakusaidia kutimiza majukumu na mipango mbalimbali.

Ikiwa basi hukupata mtu stahiki katika ndoa, faida hizo hapo juu zitakuwa kinyume chake na mtokeo yake utakosa furaha na kuishi masha ya mahangaiko ambayo katu hutofikia ndoto zako.

Soma pia: Kitu Muhimu Mark Zuckerberg Alichokijenga Harvard.

4. Jikite kwenye ratiba ya mafanikio

Tuna mambo mengi sana ya kufanya humu duniani, lakini siyo yote hutuwewezesha kutimiza ndoto zetu. Hakikisha unapanga ratiba yako kwa kuhakikisha unaongeza maarifa na unafanya kitu chochote kwa siku ili kufikia au kutimiza ndoto zako.

Mambo ya kuzingatia katika hili:

 • Tumia muda vyema (Epuka vitu vinavyopoteza muda kama vile facebook, Televisheni n.k).
 • Jifunze kitu kipya kila siku, pia soma vitabu na makala mbalimbali kama hii unayoisoma.
 • Sogeza hatua moja kila siku kuelekea malengo yako.
 • Weka akiba.
 • Linda afya yako (kwa mazoezi, tabia njema na lishe bora).

Soma pia: Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa.

5. Tafuta muda wa kupumzika na kuburudika

Kwa kuwa unatafuta kuishi ndoto zako, haimaanishi hauhitaji kupumzika au kuburudika. Unapopumzika unaupa mwili na ubongo wako nafasi ya kuwa katika hali nzuri zaidi ili uweze kufanya kazi kwa ubora zaidi.

Kwa mfano kama unapenda piano unaweza kupiga piano au ukaenda kutazama mandhari ya asili kama vile milima na wanyama. Kumbuka epuka starehe na anasa zisizokuwa na maana kama vile pombe na uzinzi.

Soma pia: Faida 10 za Kupumzika.

Hitimisho

Hapa nimeeleza dondoo tano ambazo zitakuwezesha kuishi ndoto zako kama utazitilia maanani. Nakusisitiza kuwa wakili mzuri wa muda pamoja na rasilimali ulizonazo kama vile fedha. Jiwekee malengo na  uyafuate katika maisha yako.

Je umenufaika kutokana na makala hii? Je una swali lolote? Tafadhali tuandikie maoni yako pia washirikishe wengine makala hii.

3.7 6 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

4 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Hamismalimi
Hamismalimi
4 years ago

Malengo yangu ni kuanzisha biashara lakini nilishashindwa nianzishe ipi mnanisaidisje

Cheedy
Cheedy
1 year ago

Ndoto yangu kuwa mcheza mpila lakini nashindwa fika pale napo pataka mananisaidiaje

4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x