
Mambo 20 Yakushukuru Kwa Ajili Yake Kwenye Maisha
Wakati mwingine tunatazama tu mambo ambayo hatuna kwenye maisha, kuliko yale tuliyo nayo. Mara nyingi huwa hatutambui umuhimu wa kitu hadi pale tunapokikosa. Niwazi kuwa wapo watu wanaotafuta vile tunavyoviona ni vidogo lakini hawavipati. Ni muhimu kutenga muda wa kukumbuka yale mambo yote ambayo tunapaswa kushukuru kwa ajili yake. Kama una chochote kati ya hivi basi yakupasa kushukuru. Afya njema
Mara nyingi hatutambui kuwa na afya njema pekee ni jambo muhimu na kubwa sana. Kuna wengi wanaotamani kuwa na afya kama ya kwako lakini hawana; hivyo yakupasa kushukuru kwa afya njema.
Pesa ulizonazo
Unaweza kufikiri kiasi cha pesa ulizonazo ni kidogo sana hivyo hauhitaji kushukuru. Kuna mahali pengine wewe ni tajiri mkubwa sana. Wapo wasiokuwa na pesa wala chochote kile wanachow...