Je wajua kuwa kuna viwanja vya ndege vinavyopokea ndege zaidi ya 400 kwa siku lakini bado vinamudu kufanya kazi kwa ubora na ufanisi wa juu? AirHelp.com hivi karibuni imetoa orodha ya viwanja bora vya ndege duniani kwa kutegemea vigezo vitatu ambavyo ni: kufanya kazi kwa kuzingatia muda, ubora wa huduma na kuridhika kwa wasafiri.
Fuatana nami katika makala hii ili kuona orodha ya viwanja bora zaidi vya ndege duniani.
1. Uwanja wa ndege wa Changi Singapore
Uwanja wa ndege wa Changi unakadiriwa kuwa takriban ndege 450 huruka katika uwanja huu kila siku, na kuufanya kuwa uwanja wa ndege wa sita wenye shughuli nyingi Asia na wa 17 duniani. Pamoja na hayo inasemekana kuwa ni aslilimia 12 pekee ya ndege hizo huchelewa kwa zaidi ya dakika 15 – na hili huufanya uwanja huu kuwa bora kabisa duniani.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.8/10 (Daraja: 4)
- Ubora wa huduma: 10/10 (Daraja: T-1)
- Kuridhika kwa wasafiri: 6.1/10 (Daraja: 24)
2. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Munich
Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Munich una kiwango kikubwa kidogo cha kuchelewa kwa ndege ambacho ni asilimia 18.4, lakini katika changamoto hii ni asilimia 0.16 pekee ya safari husitishwa au hucheleweshwa zaidi ya saa 3
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.2/10 (Daraja: 27)
- Ubora wa huduma: 10/10 (Daraja: T-1)
- Kuridhika kwa wasafiri: 4.8/10 (Daraja: 40)
3. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hong Kong
Uwanja wa ndege wa Hong Kong ni moja katika ya viwanja bora 10 duniani (uwanja wa saba wenye shughuli nyingi duniani), pamoja na haya uwanja huu umepata alama nzuri katika maswala ya usafi, miundombinu ya wasafiri, usalama, n.k.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 7.5/10 (Daraja: 55)
- Ubora wa huduma: 10/10 (Daraja: T-1)
- Kuridhika kwa wasafiri: 5.6/10 (Daraja: 29)
4. Uwanja wa ndege wa Kastrup Copenhagen
Uwanja huu ni moja kati ya viwanja vya kijamii ulimwenguni, uwanja huu ulianzishwa mwaka 1925. Pamoja na kuwa na umri mrefu lakini bado umekuwa na huduma bora sana duniani.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.6/10 (Daraja: 10)
- Ubora wa huduma: 8/10 (Daraja: T-4)
- Kuridhika kwa wasafiri: 5.7/10 (Daraja: 27)
5. Uwanja wa ndege wa Vantaa – Helisinki
Uwanja wa ndege wa Helsinki ni uwanja wenye alama za juu katika kuwaridhisha wasafiri. Maoni yaliyokusanywa kwa njia ya mtandao wa twitter yanadhihirisha hili.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.0/10 (Daraja: 35)
- Ubora wa huduma: 8/10 (Daraja: T-4)
- Kuridhika kwa wasafiri: 8.4/10 (Daraja: 6)
6. Uwanja wa ndege wa Cincinnati Kentucky Kaskazini
Huu ndio uwanja pekee wa Marekani uliofanikiwa kuingia kwenye viwanja bora duniani.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.6/10 (Daraja: 11)
- Ubora wa huduma: 8/10 (Daraja: T-4)
- Kuridhika kwa wasafiri: 4.8/10 (Daraja: 39)
7. Uwanja wa ndege wa El Prat – Barcelona
Asilimia 21 ya safari za ndege katika uwanja wa Barcelona zilichelewa zaidi ya dakika 15, ambayo ni chini ya wastani, lakini asilimia 0.42 ya safari hizo zilizitishwa au kuchelewa zaidi ya saa tatu. Ikumbukwe kuwa hili haliondoi ratiba yake bora na kuridhisha wasafiri kwa kiasi kikubwa kulikofanya uwanja huu kuingia kwenye kumi bora.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 7.9/10 (Daraja: 39)
- Ubora wa huduma: 8/10 (Daraja: T-4)
- Kuridhika kwa wasafiri: 7.6/10 (Daraja: 9)
8. Uwanja wa ndege wa Adolfo Suarez-Barajas Madrid
Uwanja wa Madrid unakuja baada ya ya ule wa Barcelona kwa sababu ya kuwa na alama ndogo za ubora wa huduma, lakini unazingatia muda kuliko Barcelona pamoja na kuwa na wasafiri wengi zaidi.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.7/10 (Daraja: 8)
- Ubora wa huduma: 7/10 (Daraja: T-23)
- Kuridhika kwa wasafiri: 7.4/10 (Daraja: 12)
9. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Auckland
Uwanja wa ndenge wa Auckland una alama ndogo kuliko viwanja vyote 76 vilivyopata alama katika swala la kuwaridhisha wasafiri. Swali ni je, kwanini umeingia katika kumi bora? Ni kwa sababu ya kiwango cha kuzingatia muda pamoja na ubora wa huduma.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.6/10 (Daraja: 12)
- Ubora wa huduma: 8/10 (Daraja: T-4)
- Kuridhika kwa wasafiri: 3.3/10 (Daraja: 54)
10. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Frankfurt
Uwanja huu ni wa nne kati ya viwanja vyenye shughuli nyingi Ulaya. Uwanja huu umekuwa wa kumi kutokana na kupata alama ndogo zaidi kuliko viwanja vingine kwenye kumi bora.
- Utendaji kwa kuzingatia muda: 8.4/10 (Daraja: 23)
- Ubora wa huduma: 8/10 (Daraja: T-4)
- Kuridhika kwa wasafiri: 3.8/10 (Daraja: 52)
Kwa orodha zaidi unaweza kutembelea (Airhelp.com)
Je una maoni gani kuhusu orosha hii? Je viwanja vyetu viko wapi? Je vitaingia lini katika orodha? Tafadhali toa maoni yako kisha washirikishe wengine.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Natamani siku moja uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere nchini Tanzania angalau uingie katika orodha hizi, lakini wenzetu wanaelewa nini maana ya uwekezaji na kutambua ni tija zipi zitapatikana katika kitu wanachokiamini.
Ni kweli kabisa ndugu @junioursanga:disqus itakuwa ni jambo jema kiwanja cha JNIA kikiingia kwenye orodha hii. Tunashukuru sana kwa mchango wako mzuri mno. Karibu tukufahamishe zaidi.