Ndege Archives - Fahamu Hili
Thursday, February 22Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tag: Ndege

Viwanja Bora Zaidi vya Ndege Duniani

Viwanja Bora Zaidi vya Ndege Duniani

Usafiri na Safari
Je wajua kuwa kuna viwanja vya ndege vinavyopokea ndege zaidi ya 400 kwa siku lakini bado vinamudu kufanya kazi kwa ubora na ufanisi wa juu? AirHelp.com hivi karibuni imetoa orodha ya viwanja bora vya ndege duniani kwa kutegemea vigezo vitatu ambavyo ni: kufanya kazi kwa kuzingatia muda, ubora wa huduma na kuridhika kwa wasafiri. Fuatana nami katika makala hii ili kuona orodha ya viwanja bora zaidi vya ndege duniani. 1. Uwanja wa ndege wa Changi Singapore Uwanja wa ndege wa Changi unakadiriwa kuwa takriban ndege 450 huruka katika uwanja huu kila siku, na kuufanya kuwa uwanja wa ndege wa sita wenye shughuli nyingi Asia na wa 17 duniani. Pamoja na hayo inasemekana kuwa ni aslilimia 12 pekee ya ndege hizo huchelewa kwa zaidi ya dakika 15 - na hili huufanya uwanja huu kuwa bora kabisa...