Faida 25 za Kutembea kwa Miguu - Fahamu Hili
Friday, May 24Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Faida 25 za Kutembea kwa Miguu

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Kutembea

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo.

Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii.

Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida 25 za kutembea kwa miguu.

 1. Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
 2. Huimarisha mifupa.
 3. Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
 4. Husaidia kupunguza uzito.
 5. Huzuia saratani ya utumbo mpana.
 6. Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua.
 7. Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance).
 8. Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta uwiano wa urefu na uzito – BMI; jambo litakalokukinga na aina ya pili ya kisukari (Type 2 Diabets).
 9. Hukabili shinikizo la damu.
 10. Huondoa msongo wa mawazo.
 11. Huongeza utayari.
 12. Hukufanya ujifunze mambo mbalimbali kwa kuona.
 13. Hukuokolea gharama za nauli au mafuta.
 14. Hupunguza lehemu mbaya mwilini (cholesterol)
 15. Huimarisha misuli.
 16. Husaidia mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri.
 17. Huwezesha kinga mwili kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
 18. Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
 19. Hukujengea mahusiano ya kijamii. Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
 20. Huzuia kuzeeka. Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
 21. Hukuweka katika hali nzuri (mood).
 22. Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka mazoezi ni chanzo cha usingizi mzuri.
 23. Huboresha afya ya uzazi hasa kwa wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya uzazi.
 24. Huzuia kuharibika kwa mimba. Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo zoezi rahisi na jepesi kwake ni kutembea.
 25. Huboresha mwonekano wa mwili. Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya mwili wako uonekane katika umbo zuri. Hivyo kutembea kama aina mojawapo ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.

Neno la mwisho

Naamini umeona jinsi ambavyo kutembea kwa miguu kuna manufaa makubwa sana kwenye afya, uchumi na hata mahusiano yako ya kijamii.

Inashauriwa kuhakikisha unatembea kwa miguu angalau dakika 30 kila siku. Kwa njia hii utapata manufaa mengi yaliyotajwa hapo juu.

Je wewe huwa unatembea kwa miguu? Je kuna manufaa mengine unayoyapata?

Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini. Usisahau kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3.7 3 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x