Faida 10 za Kuogea Maji ya Baridi - Fahamu Hili
Thursday, February 22Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Faida 10 za Kuogea Maji ya Baridi

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Kuoga

Watu wengi hupenda kuogea maji ya moto, hii ni kutokana na kuogopa baridi au sababu za kimazoea tu. Ingawa mara nyingi umekuwa ukisisitiziwa kuwa maji moto yana manufaa mengi, lakini hata maji ya baridi nayo yana manufaa yake.

Je uko tayari kuongeza maarifa au hata kubadili mtazamo wako? Karibu nikushirikishe faida 10 za kuogea maji ya baridi.

1. Huongeza utayari

Maji ya baridi hukufanya uchangamke, hili ni tofauti na maji ya moto. Mara nyingi mtu anapoogea maji ya baridi hasa baada ya kuamka humfanya awe katika hali nzuri ya kuwa tayari kuendelea na majukumu yake.

Kumbuka hata wakati wa kuogea maji baridi kasi ya upumuaji hubadilika na kukufanya kuongeza kiasi cha oksijeni kinachoingia mwilini.

2. Hulainisha ngozi na nywele

Maji moto huchubua ngozi na nywele, hasa kwa kuondoa mafuta laini yanayolinda ngozi na nywele na kuvifanya viwe vikavu sana.

Kwa kuogea maji ya baridi, ngozi na nywele zako havitapaushwa bali vitasafiwa na kuachwa katika hali nzuri ya kupendeza.

3. Huboresha kinga mwili

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Thrombosis Research Institute, ulibainisha kuwa watu wanaoogea maji ya baridi wanaongeza uzalishaji wa seli nyeupe za damu.

Utafiti huu unaeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha metaboli mwili unapojaribu kujipasha moto, ndipo seli hizi nyeupe ambazo hupambana na maradhi zinapozalishwa.

4. Huhamasisha kupunguza uzito

Kupunguza uzito? Ndiyo kupunguza uzito. Baada ya binadamu kula vyakula, kiasi fulani huhifadhiwa mwilini kama mafuta. Baadhi ya mafuta haya huyeyushwa na kutumiwa kuupasha mwili joto.

Hivyo kuogea maji ya baridi kutawezesha aina fulani ya mafuta kuyeyushwa ili kuzalisha joto mwilini, jambo ambalo litapelekea kupungua kwa uzito.

5. Huchangia katika afya ya misuli

Wanamichezo wanafahamu kuwa kuogea maji baridi baada ya michezo au mazoezi huwafanya wajisikie vizuri mapema. Hili ni kutokana na maji baridi kuhamasisha mzunguko wa damu ambao huiwezesha misuli kujijenga tena upya vyema.

6. Huondoa msongo wa mawazo

Utafiti uliofanyika kwenye chuo cha tiba Virginia, ulibaini kuwa kuogea maji baridi huzalisha kemikali ya noradrenaline ambayo husaidia kukabili msongo wa mawazo.

7. Hulinda afya ya uzazi ya wanaume

Utafiti uliofanyika umebainisha kuwa wanaume wanaoogea maji ya moto kwa muda wa nusu saa hupungukiwa mbegu za kiume kwa kiasi kikubwa baada ya kipindi cha miezi sita. Hili ni kutokana na mbegu za kiume kuwa rahisi sana kuathiriwa na joto.

Utafiti huo unaongeza kuwa wanaume walioacha kuogea maji ya moto kati ya hao waliochunguzwa, kiasi cha mbegu za kiume kiliongezeka kwa asilimia 491. Je bado huoni manufaa ya maji ya baridi? Naamini sasa umeshaaza kuyaona.

8. Hukusaidia kulala vyema

Je umeshawahi kuogea maji baridi ukiwa umechoka sana au umefanya kazi ngumu? Kama umeshawahi kuogea maji baridi ni wazi kuwa ulijisikia vizuri na ukalala vizuri pia.

Hili ni tofauti na maji ya moto kwani badala ya kukupooza na kukufanya ulale vyema yatakufanya uchemke na kuchoka zaidi.

Soma pia: Njia 13 za Kupata Usingizi Mzuri/Kulala Vizuri.

9. Huboresha mzunguko wa damu

Mtu anapokuwa anaoga kwa maji baridi mapigo ya moyo huenda kasi na kusababisha damu kuzunguka vyema kwenye maeneo mbalimbali ya mwili.

Mzunguko mzuri wa damu utaondoa vile visivyotakiwa na kuleta vile vinavyotakiwa kwenye viungo na sehemu mbalimbali za mwili wako.

10. Hurudisha nguvu za mwili

Mara nyingi mtu anapokuwa amechoka, kwanza huhitaji kuoga ili ajisikie vizuri. Ni wazi kuwa mtu anapooga hasa kwa maji baridi hujisikia kurudiwa na nguvu au hali nzuri kuliko ile aliyokuwa nayo kabla ya kuoga.

Ikiwa umechoka na unatokwa na jasho, hebu jaribu kuogea maji baridi nawe utashuhudia swala hili.

Neno la Mwisho

Naamini umepata maarifa juu ya faida za kuogea maji baridi. Naamini sasa hakuna haja ya kuongeza foleni za maji jikoni wakati unaweza kuogea maji ya baridi na ukapata manufaa yaliyoelezwa hapa.

Kumbuka!

Ikiwa una tatizo la msingi la kiafya kama vile maradhi yatokanayo na baridi au tatizo lingine la kiafya linaloathiriwa na baridi, ni vyema ukaogea maji ya moto au ya uvuguvugu.

Je una swali au maoni yoyote? Tafadhali tushirikishe kwa kutuandikia hapo chini. Karibu uwashirikishe wengine makala hii pamoja na kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

 

2.9 9 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

5 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Denis jongo
Denis jongo
5 years ago

Nimekupenda bure ndugu

Eston J.
Admin
Reply to  Denis jongo
5 years ago

Nashukuru sana ndugu; nami pia nakupenda sana msomaji wangu. Karibu tena Fahamuhili.com

Nsajigwa Mwakyusa
Nsajigwa Mwakyusa
3 years ago

Kwanza kabisa nawashukuru kwa elimu mliyo itoa bure kwa kipindi hiki cha watu walio kosa utu busala,wengi wetu tumeweka maslai mbele kuliko kuwasaidia watu ili waweze kujikwamua Katika matatizo mbalimbali,Mungu awabariki muendelee kutuelimisha naamini hadhina yenu ipo na Mungu atawalipa.Napenda sana nakala zenu sijui mnapatikana wapi?

Fanuel
Fanuel
1 year ago

Usalama wa kuoga maji baridi kutokana na vimelea wadudu ambao naamini huangamizwa kwa maji kupata moto limekaaje?

5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x