Chakula Archives - Fahamu Hili
Tuesday, October 3Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tag: Chakula

Njia 12 za Uhakika za Kuacha Pombe

Njia 12 za Uhakika za Kuacha Pombe

Mtindo wa Maisha
Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari mbalimbali kiafya na kisaikolojia. Wengi baada ya kuathiriwa na pombe hutamani kuacha matumizi ya pombe lakini ni wachache tu ndiyo hufanikiwa katika hili. Ikiwa unataka kuacha au kumsaidia mtu mwingine kuacha pombe, basi fuatilia njia 12 za uhakika za kuacha pombe. 1. Epuka watu watakaokushawishi kunywa pombe Mara nyingi kama wewe unapenda kunywa pombe utakuwa na marafiki wanaokunywa pombe pia. Ni wazi kuwa marafiki wanaokunywa pombe watakuhimiza kunywa hata kwa kukununulia au hata pengine kukukebehi na kukubeza juu ya uamuzi wako wa kuacha pombe. Hivyo ikiwa unataka kuacha kunywa pombe ni lazima uepuke marafiki au watu wanaoweza kukushawishi kunywa pombe. Unaweza kutafuta ma...
Aina 9 za Vyakula  Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona

Aina 9 za Vyakula Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona

Mtindo wa Maisha
Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti. Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona. 1.Samaki Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3. 2.Mboga za majani Watu ...
Njia 12 za Kuondoa Sumu Mwilini

Njia 12 za Kuondoa Sumu Mwilini

Afya
Asilimia kubwa ya maradhi yanayowasumbua watu hivi leo yanatokana na sumu zilizopo katika miili yao. Inawezekana umewahi kusikia mambo mengi kuhusu sumu kwenye mwili, lakini hufahamu chazo halisi cha sumu hizi. Mabadiliko ya mazingira na mtindo wa maisha hupelekea kutengenezeka na kuingia kwa sumu nyingi ndani ya mwili wa binadamu. Sumu hizi hutokana na vyakula, vinywaji na hata mazingira tunayoishi. Sumu hizi huweza kuleta madhara makubwa mwilini kama vile kushindwa kufanya kazi kwa viungo vya mwili na hata aina mbalimbali za saratani. Ni vyema ukafahamu njia bora za kuondoa sumu mwilini mwako ambazo unaweza kuzifanya wewe mwenyewe bila gharama za ziada. 1. Kula vyakula vya asili Hivi leo watu hufikiri kula vyakula vya asili ni kupitwa na wakati. Wengi husifu vyakula vya vi...
Faida 7 za Kula Mayai Wakati wa Kifungua Kinywa

Faida 7 za Kula Mayai Wakati wa Kifungua Kinywa

Mtindo wa Maisha
Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao. Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai. Fuatana nami katika makala hii ili nikueleze faida 7 za kula mayai wakati wa kifungua kinywa. 1. Hutunza shibe Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano. 2. Husaidia kupunguza uzito Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilingani...
Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Mtindo wa Maisha
Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya na wauzaji wa maziwa wamekuwa wakieleza faida kadha wa kadha za kunywa maziwa. Je umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokanazo na unywaji wa maziwa? Ni wakati wako sasa wa kujiuliza kwa kina juu ya faida zitokanazo na unywaji wa maziwa. Fuatana nami katika makala hii nikueleze faida 10 zitokanazo na unywaji wa maziwa. 1. Hujenga na kulainisha ngozi Je unamfahamu Cleopatra? Cleopatra alikuwa ni malikia wa Misri anaesadikiwa kuwa mzuri sana. Inaaminikia uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kuogea maziwa mara kwa mara. Hivyo basi, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku. 2. Hu...