
Mambo 6 Usiyoyafahamu Kuhusu Pesa
Inawezekana unabeba pesa kwenye pochi au mfuko wako au pengine umezitunza benki, lakini ni kwa kiasi gani unafahamu kuhusu pesa? Ni dhahiri kuwa unaweza kuzitumia pesa hadi mwisho wa maisha yako bila hata kujua mambo fulani yanayozihusu. Fuatilia makala hii nikufahamishe mambo 6 usiyoyafahamu kuhusu pesa.
1. Pesa ya noti siyo karatasi
Watu wengi wanafikiri kuwa pesa ya noti imetengenezwa kwa karatasi lakini si kweli. Malighafi zilizotengenezea pesa ya noti, mojawapo ni pamba. Imetengenezwa hivi ili iwe imara zaidi na yenye kukabiliana na mambo kama vile vimiminika na uchafu.
2. Wazo la ATM liliibuka bafuni
Mgunduzi John Shepherd-Barron alipata wazo la kuweka ATM bafuni manamo miaka ya 1960 akiwa bafuni. 3. Pesa zina virusi vya mafua na cocaine
Utafiti umebaini kuwa kutokana n...