Blog - Page 2 of 20 - Fahamu Hili
Thursday, April 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Blog

Madhara 6 ya Kutazama Televisheni (TV) Unayopaswa Kuyafahamu

Madhara 6 ya Kutazama Televisheni (TV) Unayopaswa Kuyafahamu

Tija
Miaka ya nyuma televisheni ilikuwa ni kitu adimu sana. Lakini hivi leo takriban kila familia au mtu ana televisheni nyumbani kwake; inaweza kuwa sebuleni, chumbani au hata kwenye simu yake ya kisasa. Hata wale wasiokuwa na televisheni nyumbani kwao bado wanapata nafasi ya kutazama televisheni kwenye migahawa, mabasi au hata kwenye ofisi za kampuni au taasisi mbalimbali. Televisheni imekuwa ni kifaa muhimu kwa ajili ya habari na burudani; hata hivyo televisheni inaweza kuwa na madhara kadha wa kadha kwako ikiwa haitotawaliwa vyema. Basi karibu ufahamu madhara ya kutazama televisheni (TV) 1. Hupoteza muda Unapokaa na kuangalia televisheni ni wazi kuwa unatumia muda mwingi na wa muhimu sana. Hii ni kutokana na sababu kuwa watu wengi hutazama televisheni kwa muda mrefu au hata siku...
Mambo 6 Yatakayokufanya Ufikiri Kama Mshindi Ili Uboreshe Maisha Yako

Mambo 6 Yatakayokufanya Ufikiri Kama Mshindi Ili Uboreshe Maisha Yako

Maendeleo Binafsi
Kila jambo tunaloliona kwenye ulimwengu wa leo lilianza kwanza kwenye fikra. Mwanariadha hawezi kushinda kama hawezi kufikiri na kujiona kuwa mshindi akilini mwake kabla ya kuanza mbio; kadhalika mtu mwingine yeyote hawezi kufanikiwa ikiwa hatoona lile analotaka kulifanya au kulifanikisha akilini mwake kwanza. Ikiwa basi unapenda kuboresha maisha yako kwa kuishi kama mshindi, karibu nikushirikishe mambo 6 yatakayokufanya ufikiri kama mshindi. 1. Amini kuwa kila kitu kinawezekana Hakuna mtu yeyote anayeweza kuwa mshindi bila kuamini kwanza kuwa kila kitu kinawezekana. Ikiwa hauamini kuwa kila kitu kinawezekana, utawezaje kufanya mambo kwa bidii na kwa imani kuwa yatafanikiwa? Hebu fikiri juu ya watu waliofanya safari ya kwanza kwenda mwezini; ni wazi kuwa hakukuwa na safari ...
Nukuu (Quotes) 30 za Uongozi Zitakazokujenga Zaidi

Nukuu (Quotes) 30 za Uongozi Zitakazokujenga Zaidi

Maendeleo Binafsi
Uongozi ni dhamana; tena ni nafasi ya kipekee inayopaswa kutumiwa vyema. Tuna viongozi wengi katika jamii yetu lakini siyo wote ni viongozi bora. Baadhi hutumia uongozi kama silaha, chanzo cha kipato au hata kichaka cha kuficha maovu. Kwa hakika kila kiongozi anatakiwa kujitambua na kupata maarifa stahiki ya uongozi. Ikiwa unapenda kuongeza maarifa yako au unataka kufahamu zaidi kuhusu uongozi; basi karibu nikufahamishe nukuu 30 za uongozi. Soma pia: Sifa 10 Zitakazokufanya Kuwa Kiongozi Bora Je wewe ni kiongozi? Je umejifunza kitu kutokana na nukuu hizi za uongozi? Tafadhali andika maoni yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii.
Faida 10 za Kusafiri Unazotakiwa Kuzifahamu

Faida 10 za Kusafiri Unazotakiwa Kuzifahamu

Usafiri na Safari
Najua umeshajiuliza faida za kusafiri? Ndiyo, kusafiri kuna faida nyingi unazopaswa kuzifahamu. Swala la kusafiri au kutembelea maeneo mbalimbali halijazoeleka sana kwetu waafrika kama ilivyo kwa wenzetu wazungu. Kusafiri siyo lazima kwenda nchi nyingine, bali hata safari za ndani ya nchi au za ndani ya eneo lako zina maana kubwa. Kwa hakika zipo sababu kuntu zinazowafanya wenzetu wa magharibi kusafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani. Ikiwa basi unataka kufahamu faida za kusafiri ili uzifanyie kazi, basi karibu nikushirikishe faida 10 za kusafiri. 1. Kujifunza mambo mbalimbali Unaposafiri unajifunza mambo mbalimbali ambayo isingekuwa rahisi kujifunza mambo hayo ukiwa nyumbani. Unaposafiri utajifunza jografia, utamaduni au hata mtindo wa maisha wa watu wa eneo utakalotembelea. ...
Faida 7 za Kuwa na Uvumilivu Unazotakiwa Kuzifahamu

Faida 7 za Kuwa na Uvumilivu Unazotakiwa Kuzifahamu

Hamasa
Maisha yana milima na mabonde, kipindi cha raha na shida. Katika kipindi cha shida au wakati mtu anapokutana na changamoto swala la uvumilivu linahitajika sana, tena sana. Kukosa uvumilivu kumewafanya wengi kushindwa kufanya maamuzi sahihi na kujikuta wakitumbukia kwenye shida zaidi. Haijalishi unapitia magumu mengi kiasi gani, kuvumilia ni lazima. Ikiwa unataka kujifunza faida au umuhimu wa uvumilivu, basi fahamu faida 7 za uvumilivu katika maisha yako. 1. Hukuwezesha kufanya maamuzi sahihi Ndani ya uvumilivu kuna subira, ikumbukwe kuwa wahenga walisema subira yavuta heri. Hii ina maana kuwa kufanya maamuzi mara ukutanapo na changamoto kunaweza kukusababishia kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Kwa mfano hebu fikiri mtu ameachwa na mchumba wake ghafla naye mara moja anataka kupa...
Vitu 10 Ambavyo Wanaume Waliokomaa Hawavifanyi

Vitu 10 Ambavyo Wanaume Waliokomaa Hawavifanyi

Maendeleo Binafsi
Je mwanaume aliyekomaa ni yupi? Je ni mwenye miaka zaidi ya 18? Kwa kawaida kuna makundi makuu mawili ya wanaume, wanaume wachanga na wanaume waliokomaa. Kama kulivyo na tofauti kubwa kati ya mtoto mchanga na mtu mzima au aliyekomaa ndivyo ilivyo pia kwa makundi haya mawili ya wanaume. Mwanaume aliyekomaa ni yule ambaye maamuzi na matendo yake yanahusisha busara, hekima pamoja na utafiti wa kutosha. Ikiwa unapenda kuwa au kumfahamu vyema mwanaume aliyekomaa basi karibu nikufahamishe vitu 10 ambavyo wanaume waliokomaa hawavifanyi. 1. Hawaruhusu hofu kuwazuia kufikia furaha na malengo yao Kwa hakika ni kweli kabisa hofu ni adui mkubwa wa mafanikio yetu. Wanaume waliokomaa wanafahamu madhara ya hofu maishani mwao hivyo hawaruhusu hofu hasa ile ya kushindwa iwatawale. Wanaum...
Vitu 10 Ambavyo Kila Mzazi au Mlezi Anatakiwa Kumfundisha Mtoto Wake

Vitu 10 Ambavyo Kila Mzazi au Mlezi Anatakiwa Kumfundisha Mtoto Wake

Mahusiano na Familia
Mzazi au mlezi ndiye mwalimu namba moja wa mtoto wake. Kwa kiasi kikubwa sana mtoto hujifunza na kuiga vitu au mambo mbalimbali kutoka kwa wazazi au walezi wake. Hivyo ni muhimu sana mzazi kuhakikisha anamfundisha mtoto wake mambo muhimu anayopaswa kujifunza ili akue katika malezi bora na awe na baadaye (future) njema. Kwa kutambua umuhimu wa mzazi au mlezi kumfundisha mtoto wake mambo kadhaa muhimu; karibu ufahamu vitu au mambo 10 ambayo kila mzazi au mlezi anatakiwa kumfundisha mtoto wake. 1. Matumizi mazuri ya muda Matumizi ya muda ni swala muhimu kwa kila mtu, tena ni msingi wa mafanikio kwa kila mtu. Hivyo mzazi au mlezi anapaswa kumfundisha mtoto wake matumizi ya muda tangu akiwa mtoto ili akue akiwa na tabia hiyo. Mzazi au mlezi anapaswa kumfundisha mtoto wake maswala...
Faida 10 za Kusoma Nje ya Nchi

Faida 10 za Kusoma Nje ya Nchi

Maendeleo Binafsi
Watu wengi wamekuwa wakitamani kusoma nje ya nchi, labda ni kutokana na kupata safari nyingi za ndege au fedha za udhamini wa masomo. Kwa hakika kusoma nje ya nchi kuna manufaa makubwa sana zaidi ya kusafiri kwa ndege pamoja na kupata fedha za udhamini wa masomo. Ikiwa unataka kuongeza maarifa au unataka kusoma nje ya nchi, basi fahamu faida 10 za kusoma nje ya nchi. 1. Kuongeza uwezo wako wa lugha Kusoma kwenye nchi nyingine itakulazimu kujifunza lugha ya nchi husika ili uweze kuwasiliana na kuitumia kujifunza mambo mbalimbali. Kwa mfano watu wengi wanaosoma nchi za ulaya huongeza uwezo wao wa kuzungumza kiingereza zaidi. Hivyo kusoma nchi za kigeni kutakuwezesha kujifunza na kuongeza uwezo wako wa lugha za kigeni kama vile Kichina, Kifaransa, Kijapani, Kiingereza, Kijer...
Vitu 10 Ambavyo Wazazi Wawajibikaji Wanavifanya

Vitu 10 Ambavyo Wazazi Wawajibikaji Wanavifanya

Mahusiano na Familia
Malezi ni swala linalohusisha pande kuu tatu, yaani wazazi, mtoto na jamii. Hivyo wazazi wanapaswa kuwajibika kusimamia nafasi yao ya malezi ya watoto ili watoto wao wakue kwenye misingi bora ya maadili. Hili linatupa makundi mawili ya wazazi, yaani wale wanaowajibika na wale wasiowajibika katika familia na malezi. Ikiwa wewe ni mzazi au unatarajia kuwa mzazi, basi fahamu vitu 10 ambavyo wazazi wawajibikaji wanavifanya katika malezi ya familia zao. 1. Wanafanya kwa matendo kuliko maneno Wazazi wawajibikaji wanafanya kwa matendo kuliko maneno, yaani wao kama wanawaagiza watoto wafanye kazi kwa bidii, nao utawakuta kila wakati wanafanya kazi kwabidii. Ikiwa wanawahamasisha watoto wao kumcha Mungu au kuwa na maadili mema kwenye jamii, basi nao utawakuta wakiwa mstari wa mbele kuya...
Faida 6 za Kufundisha Watu Wengine Kile Unachokijua

Faida 6 za Kufundisha Watu Wengine Kile Unachokijua

Maendeleo Binafsi
Sio watu wengi wanaopenda au wanafahamu umuhimu wa kuwafundisha watu wengine kile wanachokifahamu. Wengi huona kuwa kufundisha watu wengine ni kazi duni ambayo haiwezi kuwanufaisha kwa njia yoyote ile. Ukweli ni kuwa kufundisha watu wengine ni swala lenye manufaa mengi ambayo watu wasiofanya hivyo wanayakosa. Ikiwa unapenda kuwa bora zaidi pamoja na kuongeza maarifa yako, basi karibu nikufahamishe faida 6 za kufundisha watu wengine. 1. Hukuongezea maarifa Kufundisha wengine ni njia bora ya kuongeza maarifa yako. Kwanza kabisa utahitajika kujiandaa kwa kusoma na kujifunza mambo mbalimbali ili uweze kufundisha vyema, hili litakuongezea kiwango kikubwa cha maarifa. Pili wakati wa kufundisha utajifunza mambo mbalimbali kutoka kwa yule unayemfundisha au wale unaowafundisha kwani...